- Yanga SC vs Simba SC Fainali ya Muungano Cup 2026 mshindi ni mmoja na atakayepoteza vilevile
- Mwamuzi Mkenya akabidhiwa kuamua mchezo wa Kariakoo Dabi
- Uwanja wa New Amaan Complex Aprili 29, 2026 mchezo unaofuata Mei 3, 2026 Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo NBC Premier League
- Yanga SC 0-0 Simba SC ni matokeo ya mchezo uliopita leo watakabana koo
Hamna namna Yanga SC vs Simba SC Fainali ya Muungano Cup 2026 mshindi ni mmoja na atakayepoteza mmoja. Mchezo huo utapigwa leo 29/4/2026, Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Hii ni Kariakoo dabi, inasubiriwa kwa shauku kubwa kwa wababe hawa kusaka mshindi.
SOMA TAARIFA HII: Yanga SC vs Simba SC uso kwa uso Fainali Muungano Cup 2026 | h2h, Ratiba, Matokeo, Takwimu
Je, wajua? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini

Yanga SC vs Simba SC Fainali ya Muungano Cup 2026 mshindi ni mmoja

Ipo wazi kuwa Yanga SC vs Simba SC Fainali ya Muungano Cup 2026 mshindi ni mmoja na atakayepoteza ni mmoja. Hii ni kutokana na uhalisia kwamba fainali lazima mshindi apatikane. Ni Wananchi walitangulia fainali kwa matokeo ya Yanga SC 2-1 Azam FC, Mnyama aliwafuata kwa kuibomoa Mlandege FC 0-3 Simba SC hatua ya Nusu Fainali.
Mchezo wa leo wanasema hakuna kujivunja. Ikifika saa 2:15 usiku kazi inaanza. Atakayepoteza leo ana kibarua kingine Mei 3, 2026 Uwanja wa Meja Isahmuyo, Kariakoo Dabi katika NBC Premier League.
Wiki lipo na shughuli kwelikweli kutokana na mechi kubwa mbili. Aprili 29, 2026 Yanga SC vs Simba SC, Muungano Cup Fainali wenyeji ni mabingwa watetezi. Mei 3, 2026 Simba SC vs Yanga SC hapa ni ndani ya ligi namba nne kwa ubora.
SOMA HII: Muungano Cup 2026 | Ratiba, Simba SC, Yanga SC kukiwasha Robo Fainali

Yanga SC wamefikaje hatua ya fainali

Yanga iliwafungashia virago Muembe Makumbi kwenye robo fainali kwa ushindi wa magoli 4-0. Azam FC nusu fainali ilipata kipigo cha magoli 2-1. Kinara wa ufungaji ni Prince Dube mwenye magoli 3.
Huyu hapa Simba SC mpaka fainali

Simba SC ilianza na Mafunzo SC kwenye robo fainali kwa goli 1-0.Ikawapiga Mlandege 3-0. Kinara wa utupiaji ni Seleman Mwalimu mwenye magoli 2.
Mwamuzi Kariakoo Dabi
Kamati ya Mashindano ya Muungano imemtangaza mwamuzi kutoka Kenya kuamua Fainali Yanga SC vs Simba SC. Kamati ikishirikiana na Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) imemtangaza Dickes Mimisa. Huyu ni raia wa Kenya atasaidiwa na Ally Mbwana atakayekuwa msaidizi wa kwanza, Yusuf Shombe msaidizi wa pili, hawa wanatoka Zanzibar na Isihaka Mwalile ni mwamuzi wa nne wa mezani anatoka Tanzania Bara huku Ramadhan Kibo akiwa kamishna wa mechi.
SOMA HII: Muungano Cup 2026 | Gueye, Oura, Mpanzu wa Simba SC kutikisa Zanzibar, ratiba na matokeo
Hitimisho
Yanga SC vs Simba SC Fainali ya Muungano Cup 2026, mshindi ni mmoja na atakayepoteza nis awa. Lazima apatikane bingwa kwenye fainali. Wananchi wanalitaka taji lao na Mnyama hataki unyonge. Je nani atakuwa bingwa? Endelea kufuatilia Blog ya SportPesa kwa matokeo zaidi.

