- Hatimaye mashindano ya Muungano Cup 2026 yamezinduliwa rasmi jana Aprili 19, 2026 huko visiwani Zanzibar.
- Mashindano hayo kwa mwaka huu yanahusisha timu 8, ambapo timu 4 zinatoka Tanzania Bara, huku 4 nyingine zikitoka Tanzania visiwani.
- Timu hizo ni; Yanga SC, Muembe Makumbi City, KVZ FC, Azam FC, Mlandege FC vs Singida BS, Simba SC vs Mafunzo SC
- Uzinduzi huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Mashindano ya Muungano Cup 2026 yamezinduliwa rasmi jana Aprili 19, 2026 huko visiwani Zanzibar. Uzinduzi huo ulifanyika kutoka Ukumbi wa Mikutano wa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Mashindano hayo kwa mwaka huu yanahusisha timu 8, ambapo timu 4 zinatoka Tanzania Bara, huku 4 nyingine zikitoka Tanzania visiwani. Timu hizo ni; Yanga SC, Muembe Makumbi City, KVZ FC, Azam FC, Mlandege FC vs Singida BS, Simba SC vs Mafunzo SC.
SOMA HII PIA: KVZ FC vs Yanga patachimbika Muungano Cup 2025
Je, wajua? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Kuhusu mashindano ya Muungano Cup 2026

Mashindano ya Muungano Cup 2026, ni sehemu ya sherehe ya kitaifa ya kumbukumbu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ili kupata Taifa la Tanzania. Hii ndiyo sababu inahusisha timu nne za kila upande. Mashindano haya huendeshwa kwa mfumo wa mtoano, yaani kuanzia hatua ya Robo Fainali hadi Fainali.
Unaweza kufuatilia matokeo, ratiba na takwimu za Muungano kupitia SportPesa blog
Ratiba ya Muungano Cup 2026
Mashindano ya Muungano Cup 2026 yanatarajiwa kupigwa kuanzia Aprili 21, mpaka Aprili 29, mwaka huu ambapo Aprili 21 na 22, mwaka huu kutakuwa na mchezo mmoja kila siku. Aprili 23, mwaka huu zinatarajiwa kupigwa mechi 2 za Robo Fainali. Michezo ya Nusu Fainali inatarajiwa kupigwa Aprili 25 na 26, mwaka huu huku Fainali ikipangwa kuchezwa Aprili 29, 2026, ratiba hii imethibitishwa na Katibu wa Kamati ya Mashindano hayo, Kassim Mohamed Abdallah.
Ratiba rasmi ya mashindano ya Muungano Cup 2026 ipo hivi;
| Tarehe & Saa | Mechi | Hatua | Maelezo Mafupi |
|---|---|---|---|
| Aprili 21, 2026 – 1:15 usiku | Yanga SC vs Muembe Makumbi City | Robo fainali | Yanga wanaonekana kuwa na uzoefu mkubwa, lakini wapinzani wanaweza kushtua. |
| Aprili 22, 2026 – 1:15 usiku | KVZ FC vs Azam FC | Robo fainali | Azam wanaingia kama wababe kwenye makaratasi, huku KVZ wakisaka ushindi wa kihistoria. |
| Aprili 23, 2026 – 10:15 jioni | Mlandege FC vs Singida BS | Robo fainali | Mchezo wenye ushindani mkali, timu zote zikiwa na nafasi sawa. |
| Aprili 23, 2026 – 2:15 usiku | Simba SC vs Mafunzo SC | Robo fainali | Simba wanabebwa na ubora wa kikosi, lakini Mafunzo wanaweza kuwashangaza kama watapambana kwa nguvu. |
| Tarehe & Saa | Mechi | Hatua | Maelezo Mafupi |
|---|---|---|---|
| Aprili 25, 2026 – 2:15 usiku | KVZ/Azam vs Yanga/Muembe Makumbi | Nusu fainali | Mechi inayobeba tiketi ya fainali kutoka kwa washindi wa Robo Fainali. |
| Aprili 26, 2026 – 2:15 usiku | Mlandege/Singida BS vs Simba/Mafunzo | Nusu fainali | Timu mbili zitavaana hatua hii, na ni zile ambazo zitakuwa zimeonyesha kiwango cha juu kuzidi nyingine. |
| Tarehe & Saa | Mechi | Hatua | Maelezo Mafupi |
|---|---|---|---|
| Aprili 29, 2026 – 2:15 usiku | Mshindi Nusu fainali ya kwanza vs Mshindi Nusu Fainali ya pili | Fainali | Fainali itakayotoa bingwa mpya, au kuthibitisha ubabe wa bingwa mtetezi. |
Zawadi Muungano Cup 2026 zaongezwa

Taarifa iliyotolewa na mgeni rasmi wa tukio la uzinduzi, ambaye alikuwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera na Uratibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Hamza Hassan Juma imethibitisha ongezeko la mashindano hayo. Kwa mwaka huu mshindi wa kwanza anapata kitita cha Tsh Milioni 150. Hii ni mara 3 ya Zawadi ya mshindi wa kwanza mwaka jana.
“Mshindi wa kwanza mwaka jana alipata Tsh. milioni 50, lakini mwaka huu atapata milioni 150. Mshindi wa pili mwaka jana alipata milioni 30, mwaka huu atapata Tsh. milioni 100,” amesema Mhe. Hamza.
SOMA HII ZAIDI: JKU 0-1 Yanga SC: Yanga bingwa Muungano Cup 2025
ZFF wafunguka kuhusu Muungano Cup 2026

Kwa niaba ya Shirikisho la soka Zanzibar (ZFF), Katibu Mkuu wa ZFF. Hussein Ahmada Vuai amesema: “Kwa nature ya nchi yetu, tunahitaji kuwa na mashindano kama haya. Tangu kuanzishwa kwake kumekuwa na mwitikio mzuri, hali ambayo imeboresha udhamini wa mashindano ya mwaka huu.”
Kwa niaba ya wadhamini, Shabani Mwanga bnaye alisema: “Haya ndiyo mashindano pekee yanayokutanisha uwezo wa wachezaji wa daraja A, na wachezaji wa daraja A Chanya. Hapa ndipo vipaji vya wachezaji wa Kimataifa kutoka nje ya Tanzania (Daraja A chanya), vinapokutana na vipaji vya wachezaji wa Kimataifa kutoka ndani ya Tanzania (Daraja A),”
SOMA HII PIA: Zimamoto vs Yanga SC Aprili 29 nusu fainali Muungano Cup
Hitimisho
Mashindano ya Muungano Cup 2026 yanatarajiwa kuwa na mvuto mkubwa zaidi, hii ni kutokana na ushiriki wa timu zote kubwa. Kwa mwaka jana baadhi ya timu kubwa hazikushiriki mashindano hayo, hii ni Pamoja na Simba SC. Swali ni je, nani ataibuka kidedea msimu huu.

