Atletico Madrid vs ArsenalAtletico Madrid vs Arsenal
  • Atletico Madrid vs Arsenal kinawaka kesho Jumatano 29/4/2026 jijini Madrid, ni mchezo mkali wa Nusu Fainali ya Ligi yaMabingwa Ulaya (UEFA Champions League).
  • Mechi hii itapigwa pale katika dimba la Estadio Metropolitano, ambapo Atletico Madrid watakuwa wenyeji wakiikaribisha Arsenal.
  • Mshindi wa Jumla wa mechi hii, atakutana na mshindi wa jumla wa mchezo wa Paris Saint-Germain vs Bayern Munich.
  • Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa 21/10/2025 katika Ligi ya Mabingwa ambapo matokeo yalikuwa Arsenal 4-0 Atletico Madrid.

Atletico Madrid vs Arsenal kinawaka kesho Jumatano 29/4/2026 jijini Madrid, ni mchezo mkali wa Nusu Fainali ya Ligi yaMabingwa Ulaya (UEFA Champions League). Mechi hii itapigwa pale katika dimba la Estadio Metropolitano, ambapo Atletico Madrid watakuwa wenyeji wakiikaribisha Arsenal. Mshindi wa Jumla wa mechi hii, atakutana na mshindi wa jumla wa mchezo wa Paris Saint-Germain vs Bayern Munich. Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa 21/10/2025 katika Ligi ya Mabingwa ambapo matokeo yalikuwa Arsenal 4-0 Atletico Madrid.

SOMA HII PIA: Barcelona vs Atletico Madrid UEFA Champions League: Live Score, h2h, Lineups, prediction na habari za timu

Je, wajua? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa

Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Aviator game promotional banner featuring a red propeller plane and a jackpot of 800,000,000.
Aviator: High-flying wins up to 800,000,000.

Atletico Madrid vs Arsenal h2h

Timu hizi zimekutana katika michezo 3 ambapo kila timu imefanikiwa kushinda mechi 1, huku mechi 1 iliyosalia ikiisha kwa matokeo ya sare. Arsenal wanashikilia rekodi ya kufunga magoli mengi kwenye makutano yao ambapo wamefunga mabao 5, huku Atletico wao wakifunga mabao 2 pekee. Mara 2 kati ya mikutano hii mitatu iliyopita ilikuwa katika mashindano ya UEFA Europa League, huku mchezo mmoja uliosalia ukiwa ni wa UEFA Champions League.

Fomu ya Timu kwenye UEFA Champions League

Atletico Madrid

DWWLWL

Arsenal

WWDWWD

Vikosi vinavyotarajiwa kuanza Atletico Madrid vs Arsenal

Atletico Madrid

Kikosi cha Atletico Madrid (-)
Kikosi cha Atletico Madrid

Kipa: Oblak

Walinzi: Molina, Le Normand, Lenglet, Ruggeri

Viungo: Simeone, Koke, Cardoso, Gonzalez

Washambuliaji: Griezmann, Alvarez

Arsenal

Kikosi cha Arsenal (-)
Kikosi cha Arsenal (-)

Kipa: Raya

Walinzi: White, Saliba, Gabriel, Hincapie

Viungo: Odegaard, Zubimendi, Rice, Saka

Washambuliaji: Gyokeres, Martinelli

SOMA HII ZAIDI: Real Madrid vs Atletico Madrid ‘Madrid derby’ – Live score, lineups, h2h, utabiri wa matokeo na habari za timu

Habari za timu

UEFA
UEFA

Atletico Madrid wanajiandaa kucheza nusu fainali yao ya saba ya Kombe la UEFA Champions League, na ya kwanza tangu msimu wa 2016/17. Hii ni baada ya kuiondoa Barcelona kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2 katika hatua ya Robo fainali. Kwa muda mrefu wakijulikana kama timu inayojilinda zaidi chini ya kocha Diego Simeone, Atletico wamebadili utambulisho wao na kuwa timu inayofunguka ambapo wamefunga mabao 34. Msimu huu wamevunja rekodi yao ya mabao waliyoiweka msimu wa 2013/14 ambapo walifunga mabao 26.

Lakini Arsenal wanatarajiwa kuwa mfupa mgumu kwa Atletico, hasa baada ya kushudia matokeo ya Arsenal 4-0 Atletico Madrid kwenye Uwanja wa Emirates katika hatua ya ligi msimu huu. Kwa upande wa Arsenal hii ni mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo, wamefika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa misimu miwili mfululizo. Katika ujumla Arsenal imefikia hatua hiyo mara 4 tu. Arsenal waliitoa Sporting Lisbon, kwa ushindi wa jumla wa bao 1-0 katika robo fainali.

Taarifa za majeruhi

Atletico

Ademola
Ademola

Atletico Madrid watamkosa, Pablo Barrios mwenye majeraha ya misuli ya nyuma ya paja, huku Jose Gimenez na Ademola Lookman wote wana changamoto ya misuli. David Hancko ana jeraha la kifundo cha mguu, na wako hatarini kukosa mchezo huu na wanatarajiwa kufanyiwa vipimo vya mwisho. Julian Alvarez, ambaye anahusishwa na Arsenal, pia ana mashaka madogo kutokana na kutokuwa vizuri kimwili.

Johnny Cardoso, Rodrigo Mendoza au Marcos Llorente wanaweza kurejeshwa kuchukua nafasi ya Barrios katika kiungo cha kati sambamba na Koke. Llorente pia anaweza kuanza kama beki wa kulia, ingawa Nahuel Molina ana nafasi nzuri zaidi kuanza. Hivyo kazi iko kwa kocha Simeone.

Arsenal

Kwa upande wa Arsenal, Mikel Merino ana jeraha la mguu, Jurrien Timber (kifundo cha mguu), na hata Riccardo Calafiori ana mashaka ya kucheza. Kai Havertz, Eberechi Eze (wote misuli) pamoja na Martin Zubimendi (kuugua), watafanyiwa tathmini baada ya kutolewa dhidi ya Newcastle. Eze amesema kuwa yuko sawa na alitolewa kama tahadhari tu, lakini Arteta anaweza kumrudisha Gabriel Martinelli au Leandro Trossard kuanza upande wa kushoto. Viktor Gyokeres anaonekana kuwa tayari kuchukua nafasi ya Havertz katika safu ya ushambuliaji.

SOMA HII PIA: 5 Epic Moments to Anticipate in Arsenal vs. Tottenham: Ultimate Derby Showdown Awaits!

Utabiri na hitimisho

Atletico Madrid vs Arsenal unatarajiwa kuwa mchezo mgumu zaidi, na wenye uchache wa mabao kutokana na muundo wa kiuchezaji wat imu hizi siku za karibuni. Kila timu inasaka ubingwa wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa udi na uvumba. Presha ni kubwa kwa makocha wote wawili, hasa baada ya kila timu kupoteza nafasi ya kushinda ubingwa wa mashindano mengine katika mechi za fainali.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.