Simba SC (3) vs Mlandege FC (0)Neo Maema
  • Simba SC (3) vs Mlandege FC (0) Muungano Cup 2026 Aprili 26, 2026
  • Seleman Mwalimu afunga goli la ufunguzi, Anicet Oura na Neo Maema watakata
  • Mnyama amelipa kisasi dhidi ya Mlandege FC dakika 90 Muungano Cup, New Amaan Complex
  • Kariakoo Dabi ndani ya Zanzibar fainali Aprili 29, 2026

Simba SC (3) vs Mlandege FC (0) ni matokeo rasmi Muungano Cup nusu fainali ya 2026. Magoli yote yalifungwa kipindi cha pili na Seleman Mwalimu dakika ya 61, Anicet Oura dakika ya 76 na Neo Maema dakika ya 89 ambaye alichaguliwa kuwa Man of The Match. Kariakoo Dabi harufu imetimia fainali ni Yanga SC vs Simba SC, Aprili 29, 2026.

SOMA HII: Yanga SC vs Simba SC | Dabi ya Kariakoo hatihati kupigwa Fainali Muungano Cup 2026, Ratiba, matokeo, kuwagonganisha

SportPesa Aviator Challenge

Simba SC (3) vs Mlandege FC (0) Kariakoo Dabi imetimia

Simba SC (3) vs Mlandege FC (0)
Seleman Mwalimu mshambuliaji wa Simba SC.

Ushindi wa Simba SC (3) vs Mlandege FC (0) katika nusu fainali ya pili Muungano Cup unatimiza harufu ya Dabi ya Kariakoo. Ikumbukwe kwamba mwanzo wa mashindano haya jambo hili lilitarajiwa. Blog ya SportPesa iliandika dondoo muhimu kuhusu Muungano Cup, ratiba mpaka kunukia kwa Kariakoo Dabi.

Yote haya ilitokana na mashindano kuwa ni mtoano na kila timu kushinda mechi zake. Mabingwa watetezi Yanga SC walianza kutinga hatua ya fainali baada ya ushindi dhidi ya Azam FC. Magoli ya Prince Dube dakika ya 9 na Maxi Nzengeli dakika ya 24 huku Azam FC mfungaji akiwa Feisal Salum dakika ya 78.

H2H Simba SC vs Mlandege FC

Simba SC (3) vs Mlandege FC (0)
Ellie Mpanzu winga wa Simba SC.
TareheMashindanoMatokeo
26 Aprili 2026Nusu Fainali Muungano CupSimba SC 3 – 0 Mlandege
13 Januari 2024Fainali Kombe la MapinduziMlandege 1 – 0 Simba
3 Januari 2023Kombe la MapinduziMlandege 1 – 0 Simba
7 Januari 2022Kombe la MapinduziSimba 0 – 0 Mlandege
17 Oktoba 2020Mechi ya KirafikiSimba 3 – 1 Mlandege
9 Januari 2019Kombe la MapinduziSimba 1 – 0 Mlandege

Simba SC imeshinda mara 3 (2026, 2020, 2019). Mlandege FC imeshinda mara 2 (2024, 2023).  Mara moja wametoka sare (2022) wababe hawa wawili.

SOMA HII: Muungano Cup 2026 | Ratiba, Simba SC, Yanga SC kukiwasha Robo Fainali

SportPesa Aviator Challenge

Matokeo ya Muungano Cup 2026

Matokeo ya Yanga SC Muungano Cup 2026

Aprili 21, 2026, Yanga SC 4-0 Muembe Makumbi

Aprili 25, 2026, Yanga SC 2-1 Azam FC

Matokeo ya Azam FC, Muungano Cup 2026

Simba SC (3) vs Mlandege FC (0)
Yanga SC vs Azam FC, Muungano Cup 2026.

Aprili 22, 2026, KVZ 0-2 Azam FC

Aprili 25, 2026, Yanga SC 2-1 Azam FC

Matokeo ya Simba SC Muungano Cup 2026

Aprili 23, 2026, Simba SC 1-0 Mafuzo SC

Aprili 26, 2026, Mlandege FC 0-3 Simba SC.

Matokeo ya Mlandege SC Muungano Cup 2026

Aprili 23, 2026, Mlandege SC 2-1 Singida Black Stars

Aprili 26, 2026, Mlandege FC 0-3 Simba SC.

SOMA HII: Simba SC vs Mafunzo SC Muungano Cup 2026 hatua ya robo fainali

Hitimisho

Simba SC (3) vs Mlandege FC (0) Muungano Cup 2026 kisasi kimelipwa. Ikumbukwe kwamba mara ya mwisho wababe hawa walipokutana mnyama alipoteza. Kariakoo Dabi ndani ya Zanzibar katika mchezo wa fainali, nani atabeba ubingwa? Endelea kufuatilia blog ya SportPesa tutakujuza matokeo.

Share this: