- KMC FC inaburuza mkia 2025/26 ipo kwenye hatari ya kushuka daraja
- Mechi iliyopita matokeo yalikuwa KMC FC 1-1 Tanzania Prisons, Uwanja wa KMC Complex
- Ipo nafasi ya 16 ikipata ushindi katika mechi 2 kati ya 19, vipigo mechi 14, sare 3 NBC Premier League
- Kocha Maximo alifungashiwa virago mrithi wa mikoba yake Bares naye akafuata
KMC FC inaburuza mkia 2025/26 katika msimamo wa NBC Premier League. Haijawa na matokeo mazuri katika mechi za ushindani. Mchezo uliopita ikiwa nyumbani ubao ulisoma KMC FC 1-1 Tanzania Prisons. Ipo katika hatari ya kushuka daraja.
SOMA HII: KMC 0-2 Simba SC, Umeona msimamo wa Ligi Kuu, ratiba ya NBC?
Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

KMC FC inaburuza mkia 2025/26, haya hapa matokeo yake

KMC FC inaburuza mkia 2025/26 kwenye msimamo wa NBC Premier League. Baada ya mechi 19 imepata ushindi mechi 2 pekee ikipoteza mechi 14. Ina sare 3 ni timu inayoongoza kwa kupokea vipigo kwenye mechi nyingi.
Inaweza kushuka daraja ikiwa haiatapata matokeo mazuri kwenye mechi zilizobaki mzunguko wa pili. Ikiwa itaendelea kupoteza ama kupata sare itakwenda kushiriki Championship. Inatumia Uwanja wa KMC Complex kwa mechi za nyumbani.
Haya hapa matokeo ya KMC FC 2025/26
| Tarehe | Mechi | Matokeo |
| Aprili 14, 2026 | KMC FC vs Tanzania Prisons | 1-1 |
| Aprili 8, 2026 | Singida Black Stars vs KMC FC | 1-0 |
| Aprili 3, 2026 | Mbeya City vs KMC FC | 3-2 |
| Feb 22, 2026 | KMC FC vs Azam FC | 0-2 |
| Feb 11, 2026 | KMC FC vs Simba SC | 0-2 |
| Feb 8, 2026 | Dodoma Jiji FC vs KMC FC | 2-1 |
| Feb 3, 2026 | KMC FC vs Mashujaa FC | 1-0 |
| Jan 31, 2026 | Namungo FC vs KMC FC | 1-0 |
| Jan 27, 2026 | Coastal Union vs KMC FC | 1-1 |
| Jan 23, 2026 | TRA United vs KMC FC | 3-0 |
| Nov 25, 2025 | Pamba Jiji FC vs KMC FC | 3-0 |
| Nov 25, 2025 | KMC FC vs Mtibwa Sugar | 0-0 |
| Nov 21, 2025 | KMC FC vs JKT Tanzania | 0-1 |
| Nov 9, 2025 | Yanga SC vs KMC FC | 4-1 |
| Okt 25, 2025 | Fountain Gate vs KMC FC | 1-0 |
| Okt 18, 2025 | KMC FC vs Mbeya City | 0-3 |
| Sep 27, 2025 | Tanzania Prisons vs KMC FC | 1-0 |
| Sep 23, 2025 | KMC FC vs Singida Black Stars | 0-1 |
| Sep 17, 2025 | KMC FC vs Dodoma Jiji FC | 1-0 |

Mechi alizopata ushindi KMC FC

| Tarehe | Mechi | Matokeo |
| Feb 3, 2026 | KMC FC vs Mashujaa FC | 1-0 |
| Sep 17, 2025 | KMC FC vs Dodoma Jiji FC | 1-0 |
Kocha afungashiwa virago
Aprili 3, 2026 KMC FC ilifikia makubaliano ya kusitisha mkataba wa Abdalah Mohamed maarufu kwa jina la Bares. Mchezo wa mwisho kwa benchi la ufundi kuongoza ilikuwa Mbeya City 3-2 KMC FC. Imani Mwalupetelo anaongoza benchi la ufundi kwa sasa.
Anakuwa ni kocha wa pili kufutwa kazi. Mwanzo wa msimu ni Marcio Maximo alianza kukinoa kikosi hicho raia wa Brazil. Mkataba wake ulisitishwa rasmi Desemba 6, 2025.
SOMA HII:Yanga SC haijafungwa mechi 19 NBC Premier League 2025/26 | Matokeo na msimamo
Hitimisho
KMC FC inaburuza mkia 2025/26 katika ligi namba 6 kwa ubora Afrika. Safu ya ushambuliaji imefunga magoli 8 ambayo ni machache kuliko timu zote. Ukuta umeruhusu kufungwa magoli 30.

