- Yanga SC (2) vs Azam FC (1) Muungano Cup Uwanja wa New Amaan Complex, Aprili 25, 2026
- Prince Dube na Maxi Nzengeli wamefunga magoli yaliyoipeleka timu hiyo hatua ya fainali
- Feisal Salum kiungo mshambuliaji wa Azam FC alifunga goli pekee hatua ya nusu fainali
- Mchezo unaofuata ni Aprili 29, 2026 fainali mshindi wa mchezo kati ya Simba SC vs Mlandege FC
Yanga SC (2) vs Azam FC (1) Muungano Cup nusu fainali 2026. Mabingwa watetezi wanatinga hatua ya fainali mbele ya matajiri wa Dar. Magoli ya Prince Dube dakika ya 9 na Maxi Nzengeli dakika ya 24. Goli la Azam FC limefungwa na Feisal Salum dakika ya 78.
Je, wajua? Unaweza kushinda mpaka zaidi ya Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Yanga SC (2) vs Azam FC (1) Muungano Cup, Kariakoo Dabi kupigwa fainali? 29/4/2026?

Yanga SC (2) vs Azam FC (1) Muungano Cup ni matokeo rasmi katika mchezo wa Aprili 25, 2026 Uwanja wa New Amaan Complex. Je Kariakoo Dabi kupigwa fainali 29/4/2026? Ni swali ambalo linasubiri matokeo ya mchezo wa Nusu Fainali ya pili Aprili 25, 2026. Simba SC vs Mlandege FC mshindi atakutana na Yanga SC.
Haya ni mashindano ya mtoano hivyo dakika 90 wababe hawa wakitoshana nguvu mshindi atapatikana kwa penati. Yanga SC tayari wameshamaliza kazi. Wanasubiri mshindi atakayevaana nao katika fainali.
Ile harufu ya Kariakoo Dabi inazidi kunukia kutokana na kila mpinzani kupata matokeo uwanjani. Alianza Yanga SC hatua ya robo fainali kwa ushindi wa magoli 4 dhidi ya Muembe Makumbi. Mwananchi ameshusha kichapo kwa Azam FC goli 2-1. Amekata tiketi hatua ya fainali sasa anasubiri mshindi wa mchezo wa nusu fainali ya pili.
Simba SC alianza kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mafunzo SC. Akishinda dhidi ya Mlandege FC atakata tiketi ya fainali. Hapo Kariakoo Dabi itapigwa, akipoteza fainali itakuwa ni Yanga SC vs Mlandege FC.
SOMA HII: Muungano Cup 2026 | Gueye, Oura, Mpanzu wa Simba SC kutikisa Zanzibar, ratiba na matokeo

H2H Yanga SC vs Azam FC

Katika miaka ya hivi karibuni timu hizi zimekutana katika michezo 13, mingi kati ya michezo hii ikiwa ni ya Ligi Kuu ya NBC. Yanga SC wamekuwa na rekodi bora zaidi wakishinda mechi 7. Azam FC wao wamefanikiwa kushinda mechi 3 tu, huku mechi 3 zilizosalia zikiisha kwa sare.
10 April 2025 Azam FC 1-2 Yanga SC
2 Nov 2024 Yanga SC 0-1 Azam FC
17 March 2024 Azam FC 2-1 Yanga SC
23 Oct 2023 Yanga SC 3-2 Azam FC
25 Dec 2022 Azam FC 2-3 Yanga SC
6 Sep 2022 Yanga SC 2-2 Azam FC
6 April 2022 Azam FC 1-2 Yanga SC
Matokeo ya Muungano Cup 2026

Matokeo ya Yanga SC Muungano Cup 2026
Aprili 21, 2026, Yanga SC 4-0 Muembe Makumbi
Aprili 25, 2026, Yanga SC 2-1 Azam FC
Matokeo ya Azam FC, Muungano Cup 2026
Aprili 22, 2026, KVZ 0-2 Azam FC
Aprili 25, 2026, Yanga SC 2-1 Azam FC
Matokeo ya Simba SC Muungano Cup 2026
Aprili 23, 2026, Simba SC 1-0 Mafuzo SC
Matokeo ya Mlandege SC Muungano Cup 2026
Aprili 23, 2026, Mlandege SC 2-1 Singida Black Stars
SOMA HII: Mlandege FC vs Simba SC |Muungano Cup 2026, Ni Nusu fainali ya kisasi! Ratiba, h2h, matokeo
Hitimisho
Yanga SC (2) vs Azam FC (1) Muungano Cup mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa. Dabi ya Dar ilihamia Zanzibar katika nusu fainali ya kwanza. Je Yanga SC watatetea taji lao kwenye mchezo wa fainali Aprili 29, 2026? Endelea kufuatilia blog ya SportPesa tutakujuza matokeo.

