- Paris Saint-Germain vs Bayern Munich, mechi kali itakayopigwa leo Jumanne usiku, katika Nusu Fainali ya UEFA Champions League.
- Mchezo huu ni wa Nusu Fainali ya kwanza ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Parc des Princes jijini Paris, Ufaransa.
- Wafaransa hao wametinga hatua hii mara baada ya kuwaondosha Liverpool kwa matokeo ya jumla ya PSG 4-0 Liverpool, huku Bayern wao wakiiondosha Real Madrid kwa matokeo ya jumla ya Bayern Munich 6-4 Real Madrid.
Paris Saint-Germain vs Bayern Munich watavaana leo Jumanne usiku, katika mechi kali ya Nusu Fainali ya UEFA Champions League. Mchezo huu ni wa Nusu Fainali ya kwanza ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Parc des Princes jijini Paris, Ufaransa. Wafaransa hao wametinga hatua hii mara baada ya kuwaondosha Liverpool kwa matokeo ya jumla ya PSG 4-0 Liverpool, huku Bayern wao wakiiondosha Real Madrid kwa matokeo ya jumla ya Bayern Munich 6-4 Real Madrid.
Unaweza kubashiri ‘kuweka mkeka’ kwenye mechi hii na kushinda kupitia odds kubwa kwa kubonyeza hapa Paris Saint-Germain vs Bayern Munich na endelea kufuatilia mwenendo ya mashindano ya UEFA Champions League na mashindano mengine, na uweke ubashiri wako kupitia mechi za Odds kubwa kwa kubonyeza wino huu wa bluu SportPesa.
Je, wajua? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Paris Saint-Germain vs Bayern Munich h2h

PSG vs Bayern Munich ni mechi ambayo imerekodiwa mara 16, ambapo mpaka sasa Bayern Munich anaongoza kwa rekodi akishinda mechi 9. PSG wao wameshinda mechi 7 pekee, na hakujawahi kutokea matokeo ya sare timu hizo zinapokutana. Hii ni nafasi nyingine ya kuona timu ikiwa NBayern wataendeleza ubabe, au PSG watakataa kuwa wateja.
SOMA HII PIA: Fuatilia timu zinazoongoza Ujerumani kwa kubashiri Bundesliga.
Fomu ya Paris Saint-Germain vs Bayern Munich kwenye UEFA Champions League
WDWWWW
Bayern Munich
WWWWWW
Vikosi Vinavyotarajiwa Paris Saint-Germain vs Bayern Munich
Paris Saint-Germain

Kipa: Safonov
Walinzi: Hakimi, Marquinhos, Pacho, Mendes
Viungo: Ruiz, Vitinha, Neves, Doue,
Washambuliaji: Dembele, Kvaratskhelia
Bayern Munich
Kipa: Neuer
Walinzi: Stanisic, Upamecano, Tah, Laimer
Viungo: Pavlovic, Kimmich, Olise, Musiala,
Washambuliaji: Diaz, Kane
Habari za timu
PSG

PSG wamepata ugumu kutetea ubingwa wao wa Ligue 1, pia walipata misukosuko kadhaa katika hatua ya makundi, na hawaonekani kuwa tishio kama ilivyokuwa msimu wa 2024-25. Licha ya kupungua ubora, lakini PSG wana rekodi nzuri wakicheza mashindano ya UEFA Champions League ambapo wameshinda mechi 4 tena dhidi ya Chelsea na Liverpool na kufunga jumla ya mabao 12. Hii ni Nusu Fainali ya 3 mfululizo kwa PSG katika misimu mitatu. Kwa sasa PSG wanaongoza kwa tofauti ya pointi 6 kileleni mwa Ligue 1.
SOMA HII ZAIDI: Ligue 1 football betting – SportPesa covers the best teams in France
Bayern Munich
Ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Stuttgart Aprili 19, 2026 uliifanya Bayern ya kocha, Vincent Kompany kijihakikishia ubingwa wa Bundesliga. Mara ya mwisho Bayern kufika fainali ya mashindano haya ilikuwa mwaka 2020, ambapo wamejikuta wakitolewa katika hatua ya Robo Fainali mara 4. Hata hivyo, hakuna timu iliyobaki kwenye mashindano yenye rekodi bora ya Ulaya tangu mwaka 2026 ulipoanza kulinganisha na Bayern. Kikosi cha Kompany kimeshinda mechi saba za mwisho za UCL, baada ya ushindi dhidi ya Real Madrid wa 2-1 na 4-3 katika robo fainali.
Habari za majeruhi
PSG
Ushindi wa PSG dhidi ya Liverpool katika mchezo wa marudiano ulionekana kuleta majeraha kwa, Desire Doue na Nuno Mendes ambao walitolewa wakiwa na maumivu huko Anfield. Lakini Nyota hao wote walirejea kwenye mchezo dhidi ya Angers, na wanatarajiwa kuwa tayari kwa mchezo. Pia PSG wanatarajiwa kupata nguvu kwa kurejea kwa kiungo muhimu Vitinha, ambaye alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya kisigino.
Fabian Ruiz naye amerudi baada ya kukaa nje kwa miezi miwili kutokana na tatizo la goti, na ana nafasi kubwa ya kuanza mchezo huu mkubwa baada ya kucheza dakika 45 dhidi ya Angers.
Bayern Munich

Pigo kubwa kwa Bayern Munich ni kukosekana kwa kocha Vincent Kompany, ambaye atakuwa benchi la adhabu baada ya kupata kadi 3 za njano katika ushindi dhidi ya Real Madrid. Kwa upande wa majeruhi, Serge Gnabry (paja), Tom Bischof (misuli), Lennart Karl (paja) na Raphael Guerreiro (hamstring) wote watakosekana. Kipa wa akiba, Sven Ulreich amepona tatizo lake la paja. Joshua Kimmich na Dayot Upamecano wanatarajiwa kurejea kikosini baada ya kupumzishwa dhidi ya Mainz, huku Harry Kane akiingia kutoka benchi na kufunga bao lake la 53 msimu huu.
SOMA HII PIA: PSG vs Real Madrid Julai 9 2025 live: H2H, Vikosi, utabiri, habari za timu
Utabiri na hitimisho
Paris Saint-Germain vs Bayern Munich ni zaidi ya mchezo, ni mechi mbili tu, kati ya nane zilizopita kati ya PSG na Bayern Munich ambazo timu zote zilifunga. Uwepo wa washambuliaji wa kiwango cha dunia ndani ya Parc des Princes, mchezo huu wa kwanza unaonekana kuwa na nafasi kubwa ya mabao mengi. Makocha wote wawili pia walipata nafasi ya kupumzisha nyota wao mwishoni mwa wiki, na hata bila Kompany kuwa pembeni akitoa maelekezo, unatarajiwa kuwa mchezo mgumu.

