London Dabi Chelsea Vs SpursLondon Dabi Chelsea Vs Spurs

NI dabi ya London leo Alhamisi, 3 Aprili ambapo mchezo mkali na wa kusisimua unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, jijini London kati ya Chelsea Vs Spurs. Mchezo huo unatarajiwa kuanza majira ya saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

n
Uwanja wa Stamphord Bridge; Source Chelsea

Mchezo huu mara zote umekuwa na ushindani mkubwa ambapo katika mechi zao tatu zilizopita, mabao 14 yamefungwa, huku wastani wa mashuti ukiwa 30 kwa kila mechi. Unaweza kujishindia mamilioni kwa kuweka ubashiri wako wa mchezo huu na mingine mingi na kushinda mamilioni kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa tembelea www.sportpesa.co.tz

Kwanini mahasimu hawa wa London wanazalisha mechi za kasi na ushindani mkubwa?

Ujasiri Bila Mpira

n
Mastaa wa Spurs, Son na Maddison; Source Spurs

Kocha Mkuu wa Chelsea, Enzo Maresca na yule wa Spurs, Ange Postecoglou wote ni waumini wakukwa na wanapendelea mchezo wa kushinikiza kwa nguvu timu pinzani wanapokuwa nje ya umiliki wa mpira, wakitumia mfumo wa mtu kwa mtu ‘Pressing’.

Mbinu hii mara nyingi husababisha makosa ndani ya eneo la adui, na inaweza kuleta faida kubwa kupata nafasi za kufunga.

Timu zote mbili zimekuwa na wastani mzuri wa takwimu za kuzuia Mipira ya Wapinzani msimu huu.

Katika ushindi wa Chelsea wa 4-3 mwezi Desemba, Spurs walifunga bao la kwanza baada ya Marc Cucurella kuteleza, na hii ilitokana na shinikizo ‘pressing’ yao kali ya mtu kwa mtu, lakini mbinu hii pia ni hatari kubwa, hasa dhidi ya timu zinazojua kujinasua na presha.

Mfano mzuri wa namna mfumo huu ni hatari tunaweza kuuona kupitia bao la kusawazisha la Chelsea mwezi Desemba, wakati Chelsea walivuka safu ya juu ya Spurs kupitia pasi fupi na haraka, wakimpa Jadon Sancho nafasi ya kupambana na Pedro Porro moja kwa moja, huku viongozi wa safu ya kati wa Spurs walidanganywa na mbio za Enzo Fernández na Nicolas Jackson, na kumpa Sancho fursa ya kupiga shuti lililozama nyavuni na huenda hali kama hii ikatokea tena Stamford Bridge leo Alhamisi.

SPURS NA CHELSEA WANAPENDA KUCHEZA KUTOKEA NYUMA

n
Ushindi wa mwisho walipokutana kwenye ligi; Source Chelsea

Maresca na Postecoglou ni makocha ambao muda mwingi wa mchezo wamekuwa wakihimiza timu zao kucheza pasi kutoka nyuma, jambo ambalo linaweza kuwa hatari iwapo presha ya mpinzani ni kali ambapo mpaka sasa Spurs wameshuhudiwa wakiwa na wastani wa kupoteza mpira mara 8.8 kwa dakika 90 katika maeneo yao ya ulinzi, huku Chelsea wana wastani wa 6.7 na ni timu ya 13 katika kupoteza mipira kwenye eneo lao.

HATARI YA MASHAMBULIZI YA KUSHTUKIZA

Ingawa Maresca na Postecoglou wanapenda kumiliki mpira, lakini makocha hawa timu zao ni hatari zaidi zinaposhambulia kwa kasi, ambapo Spurs na Chelsea kwa pamoja wamefunga mabao 17, kutokana na mashambulizi ya kushtukiza msimu huu.

Kwa vile mabeki wa Chelsea na Spurs mara nyingi wanapanda kusaidia mashambulizi, kila timu inapaswa kuwa makini ili kuepuka kuadhibiwa kupitia mashambulizi ya kushutikiza.

TUTEGEMEE MCHEZO WA KUSISIMUA!

Licha ya kuwa timu zote haziko katika kiwango bora kwa sasa, Chelsea vs Spurs ni mechi inayohakikisha mabao. Kwa historia ya mabao mengi, na mbinu zao za kushambulia kwa kasi, mechi ya leo ina kila dalili ya kuwa ya kusisimua.

MARESCA ACHARUKA KAMBINI

n
Ratiba ya Chelsea mwezi Aprili; Source Chelsea

Kocha mkuu wa Chelsea, Enzo Maresca amekuwa mbogo mazoezini hasa baada ya kikosi cha wakubwa kukubali kipigo dhidi ya timu ya Vijana wa Chini ya Miaka 21 Katika Mechi ya Mazoezi ambapo timu ya wakubwa ilikubali kipigo cha mabao 3-0 na kupelekea kocha huyo kufuta siku yao ya mapumziko.

Maresca alifikia uamuzi huo baada ya kukasirishwa na viwango duni vya mazoezi na katika mchezo huo ambao ulihusisha wachezaji wa kikosi cha kwanza ambao hawakuwa kwenye majukumu ya kimataifa dhidi ya vijana wa Under-21 kutoka akademi yao.

Katika mchezo mshambuliaji kinda wa U-21 mwenye umri wa miaka 19, Donnell McNeilly alifunga mabao mawili.

SANCHO BADO HANA MCHANGO MKUBWA CHELSEA

Jadon Sancho alikuwa mmoja wa wachezaji waliobaki klabuni wakati wa mapumziko ya kimataifa, akiwa hajafunga bao kwa Chelsea tangu Desemba 8, mwaka jana katika mechi ambayo walishinda 4-3 ugenini.

Sancho ni mmoja wa wachezaji wapya ambao walipewa onyo na Maresca majira ya joto kwamba kama hatofanya kazi kwa bidii wakati wa mazoezi, hatapata nafasi ya kucheza.

Hata hivyo, Maresca alikiri kuwa mechi hiyo ya mazoezi haikuwa rasmi, na baadhi ya nyota wake wakubwa walikosekana, huku wakilazimika kukopa baadhi ya vijana ili kujaza kikosi cha wakubwa.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.