Enzo FernandezEnzo Fernandez

London ni ya Bluu ndio usemi unaotamba kwenye jiji la London mara baada ya jana usiku Chelsea kufanikiwa kuibuka na ushindi muhimu wa bao 1-0 katika mchezo wa Dabi ya London dhidi ya mahasimu wao Tottenham Hotspurs.

n
Mapambano ya London Dabi jana usiku

Chelsea iliwashinda mahasimu wao wa London, Spurs kwa bao la ushindi lililofungwa na kiungo wa kimataifa wa Argentina, Enzo Fernández ambapo ushindi huo umewarudisha Blues nafasi ya nne kwenye Premier League, na kuongeza matumaini yao ya kurejea kwenye Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Fernández alifanikiwa kuifungia Chelsea goli hilo mara baada ya kuunganisha kwa kichwa dakika ya 50 akimalizia krosi nzuri kutoka kwa Cole Palmer, ambaye alirejea uwanjani katika mchezo huo mara baada ya kukaa nje kwa muda kutokana na majeraha.

n
Enzo akishangilia goli: Source Chelsea

Chelsea wangeweza kuibuka na ushindi wa mabao mawili mara baada ya kiungo, Moisés Caicedo kufunga goli ambalo baadae lilikataliwa baada ya ukaguzi wa VAR kugundua kwamba alikua katika eneo la kuotea.

Spurs nao liliwakuta tukio la namna hiyo nah ii ni mara baada ya shuti la, Pape Sarr la dakika ya 69 kutoka nje ya kisanduku kutinga wavuni lakini VAR ikalikataa kutokana na kuwepo kwa madhambi wakati wa ujenzi wa shambulio hilo.

Ushindi huo umeirudisha Chelsea katika nafasi ya nne, pointi moja mbele ya Manchester City walioko nafasi ya tano na pointi mbili mbele ya Newcastle United walioko nafasi ya sita lakini wakiwa na mechi moja pungufu, huku mbio za kuwania ufanisi wa Ligi ya Mabingwa zikiendelea kuiva.

Kipigo hiko kimeifanya Spurs sasa kuwa na rekodi mbaya ya kushinda mara moja tu katika mechi 40 za ligi kwenye Uwanja wa  Stamford Bridge ambapo pia matokeo hayo yanawafanya kusalia katika nafasi ya 14, huku matumaini yao ya kushiriki mashindano ya Europa msimu ujao yakitegemea uwezo wao wa kushinda Ligi ya Europa msimu huu,

Kocha wa Chelsea, Enzo Maresca, alishangilia kwa furaha na kuwakumbatia wasaidizi wake baada ya filimbi ya mwisho, ikiwa ni ishara wazi ya kupumua baada ya mfululizo wa matokeo duni, ikiwa ni pamoja na kipigo cha 1-0 kutoka kwa Arsenal katika mechi ya mwisho ya ligi.

Spurs, ambao walishindwa kutengeneza shuti lolote lililoenda langoni katika kipindi cha kwanza kwa mechi ya pili mfululizo, wangeweza kupata angalau pointi moja katika dakika ya 89, lakini kipa wa Chelsea, Robert Sánchez, alijitosa kwa nguvu kando ya lango lake na kumkatalia Son Heung-Min kwenye shambulizi la hatari.

n
Song Heung Min; Source Spurs

Mashabiki wa Spurs walionyesha hasira zao dhidi ya umiliki wa klabu na kocha Ange Postecoglou, ambaye alionekana kutania maandamano yao alipoweka mkono wake kwenye sikio lake wakati ilipoonekana kwamba Sarr alikuwa karibu kuipa timu hiyo sare.

Alipoulizwa kuhusu majibu hasi kutoka kwa mashabiki kuhusu mabadiliko yake, Postecoglou aliiambia Talksport: “Si mara ya kwanza. Mashabiki nadhani wanatoa maoni yao. Hiyo ni sawa na lazima niikubali.”

Naye mlinzi wa Chelsea, Levi Colwill, alisema kuwa Blues walilazimika kupambana ili kupata ushindi huo.

“Tunahitaji kushinda mechi mwishowe. Tunapigania nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa. Ili kushinda mechi, lazima tubadilishe mtindo wakati mwingine,” aliiambia Sky Sports

MATUKIO MENGI TATA

n
Robert Sanchez; Source Spurs

Kama ilivyotarajiwa mchezo huu ulikuwa na matukio mengi yenye utata kama ilivyokawaida kwa wapinzani hawa wa jadi, huku kocha wa Spurs, Ange Postecoglou alionekana kupitia wakati mgumu zaidi hasa baada ya kumtoa, Lucas Bergvall na kumuingiza, Pape Sarr dakika ya 64. Kama wachezaji wengine wa Spurs, Bergvall amekuwa hapati nafasi kubwa ya kucheza lakini mashabiki wanampenda.

“Hujui unachofanya,” walimwambia Postecoglou. Hali ambayo ilimfanya kocha huyu mwenye kiburi kuonyesha ishara ya kebehi muda mfupi baadaye alipoona, Sarr akimwibia mpira, Moisés Caicedo na kupiga risasi ya chini kutoka mbali, ambayo kipa wa Chelsea, Robert Sánchez, aliruhusu ipite kwake bila ya kueleweka na kuwa bao ambalo lilikataliwa na VAR.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.