Simba Vs Al MasrySimba Vs Al Masry

Kikosi cha klabu ya Simba tayari kimewasili salama nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji wao Al Masry ya Misri mchezo ambao unatarajiwa kupigwa siku ya Jumatano ya Aprili 2, mwaka huu huku kuonekana kwa kipa, Moussa Camara aliyekuwa majeruhi kukishtua kukiibua shangwe kwa mashabiki wa timu hiyo.

Simba imetua Misri na kikosi cha wachezaji 22 tayari kwa ajili ya mchezo huo wa hatua ya Robo Fainali ya kwanza ambapo ikumbukwe Simba ndio wawakilishi pekee wa Tanzania ambao wamesalia katika mashindano ya kimataifa msimu huu mara baada ya timu nyingine tatu kutolewa.

Camara kwenye mazoezi ya Simba Misri
Camara kwenye mazoezi ya Simba Misri

Kumbuka unaweza kujishindia mamilioni ya pesa kwa kuendelea kuweka ubashiri wako wa mchezo huu na mingine mingi kupitia Kampuni bora ya kubashiri ya Sportpesa ambayo inakupa ‘odds’ kubwa na za kipekee. Tembelea sasa www.sportpesa.co.tz.

KUHUSU SAFARI YA SIMBA

Jean Charles Ahoua
Jean Charles Ahoua; Source Simba

Kikosi cha Simba kiliondoka nchini usiku wa kuamkia jana Ijumaa tayari kwa ajili ya mchezo huo ambapo wachezaji walioambatana na kikosi ni;

Makipa:

Moussa Camara, Ally Salim na Hussein Abel

Mabeki:

Karaboue Chamou, Abdurazak Hamza, Mohamed Hussein, Shomari Kapombe, Valentine Nouma, David Kameta na Kelvin Kijili

Viungo:

Yusuphu Kagoma, Fabrice Ngoma, Elie Mpanzu, Debora Fernandes, Ladaki Chasambi, Kibu Denis Joshua Mutale, Augustine Okejepha, Jean Charles Ahoua na Awesu Awesu.

Washambuliaji:

Leonel Ateba na Steven Mukwala.

KOCHA SIMBA ATOA TAMKO ZITO!

Kuelekea mchezo huo kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amekiri kuwa wanautarajia mchezo mgumu hasa kutokana na ubora wa wapinzani wao wanapokuwa katika uwanja wao wa nyumbani lakini ameweka wazi kuwa anaamiki kikosi chake kimepokea maelekezo waliyopewa kwenye Uwanja wa mazoezi na ana matumaini watapata matokeo bora.

Fadlu pia ameweka wazi kuwa matokeo ya jumla ya mchezo miwili ndo yataamua hatima Simba kutinga hatua ya Nusu Fainali kwa mara ya kwanza tangu mfumo mpya wa mashindano hayo ulivyozinduliwa.

“Mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry ni muhimu na tuko hapa kuhakikisha tunapata matokeo muhimu, lakini haijalishi tutakutana na matokeo ya aina gani hapa ugenini hatima ya nani anaenda Nusu Fainali itaamuliwa katika mechi ya pili itakayopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Tutajitahidi kuhakikisha tunapata bao la ugenini na kujilinda ili tusirihusu bao au mabao mengi. Ni kweli mara kadhaa tumeishia Robo Fainali lakini ni malengo yetu msimu huu kuvuka na Kwenda mbali zaidi na kwa ukuaji wa maendeleo ya kikosi chetu hili linawezekana,” amesema Fadlu.

SEMAJI AHMED LATAMBA

n
Semaji, Ahmed na CEO wa klabu, Zubeda kwenye droo ya Robo Fainali; Source Simba

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amesema baada ya kikosi kufika nchini Misri usiku kilianza mazoezi kujiandaa na mchezo huo ambao unatarajiwa kupigwa Jumatano ya wiki ijayo.

Ahmed amesema mazoezi ya timu yatakuwa yanafanyika usiku kwenye muda ule ule ambao mchezo utachezwa ili kuwafanya wachezaji kuzoea hali ya hewa ambayo ni baridi.

USHINDI DHIDI YA BIGMAN WAIPA JEURI SIMBA

Simba inauendea mchezo huu ikiwa na kumbumbu ya matokeo mazuri katika mchezo uliopita ambapo walifanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya CRDB Federation Cup baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Bigman katika mchezo uliopigwa Uwanja wa KMC Complex.

Katika mchezo huo ni, Joshua Mutale ndiye aliipatia bao la kwanza dakika ya 15 kwa shuti la mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Valentine Nouma.

Leonel Ateba alitupatia bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 30 kufuatia Elie Mpanzu kufanyiwa madhambi ndani ya 18. Joseph Mussa aliwapatia Bigman bao la kwanza dakika ya 45 kwa shuti nje ya 18 baada ya kuwazidi ujanja walinzi.

Kipindi cha pili twenyeji walitengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini Bigman walikuwa makini kuhakikisha hawafanyi makosa ambayo yangewagharimu.

Kikosi cha Simba kilichoivusha na kutinga Robo Fainali ya CRDB ni;

Abel, Kijili (Chamou 62′) Duchu, Kazi, Ngoma, Mpanzu (Chasambi 40′), Deborah (Okajepha 81′) Ateba (Mukwala 81′), Ahoua (Awesu 81′), Mutale

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.