POINTI tatu muhimu za Merseyside Derby, Liverpool imekomba jumlajumla mbele ya Everton katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Anfield wakiendeleza kampeni yao kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England ambapo kwa sasa wanatakiwa kushinda mechi nne ambazo ni pointi 12 kujihakikishia nafasi ya kutwaa taji hilo.
Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa huku rekodi ya Kocha Mkuu wa Everton, David Moyes kuongoza kikosi kwenye mechi 9 mfululizo bila kufungwa ikikomea hapo na mchezo wa 10 rekodi ilivunjwa kwa Liverpool kuvuna pointi tatu muhimu.

Mechi zote kali ambazo zinachezwa uwanjani ni fursa kwako kukunja mkwanja kupitia SportPesa ambapo baada ya mchezo kukamilika unakunja shilingi zako.
Shukrani kwa Diogo Jota ambaye alifunga bao la ushindi kwenye mchezo huo kipindi cha pili dakika ya 57 likadumu mpaka mwisho wa mchezo huo huku Everton wakiamini kwamba mfungaji alikuwa kwenye eneo la kuotea.
Ushindi huo unaifanya Liverpool kukusanya jumla ya pointi 73 wakiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu England. Kwenye mechi 30 ambazo wamecheza ushindi ni katika mechi 22, wamepoteza mchezo mmoja na kuambulia sare katika mechi 7 ndani ya uwanja kwenye msako wa pointi tatu muhimu.
Chini ya Kocha Mkuu, Arne Slot, Liverpool imekuwa katika mwendo mzuri na sasa wanahitajika kushinda mechi nne ambazo ni pointi 12 kujihakikishia nafasi ya kutwaa ubingwa, awali walikuwa wanapaswa kushinda mechi tano, ushindi dhidi ya Everton umepunguza mzigo.

Liverpool walicheza kwa mpago kazi mkubwa kusaka ushindi kwenye mchezo huo ikiwa ni ushindi wao wa 100 dhidi ya Everton kwenye mechi za ushindani.
Kwa upande wa mabeki wa Everton walikula sahani moja na mshambuliaji namba moja wa Liverpool, Mohamed Salah ambaye alikwama kufunga bao katika mchezo huo ambao ulimalizwa na bao la Jota dakika ya 57.
MANCHESTER CITY WATEMBEZA KIPIGO
Manchester City wao kazi yao ilikuwa nyumbani na walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Leicester City ambayo haijawa kwenye mwendo mzuri ndani ya uwanja katika mechi za ushindani.

Wakiwa nyumbani City walianza kuandika bao la mapema dakika ya 2 likipachikwa na Jack Grealish ambaye alianza kuwatuliza wapinzani wao hao waliokuwa na mpango kazi wakupata pointi ugenini jambo ambalo mwisho halikutimia.
Kwenye mchezo huo bao la pili lilipachikwa na Omar Marmoush dakika ya 28 lilitosha kuwapa pointi tatu mazima City huku nyota wa City, Nicolas Gonzalez akionyeshwa kadi ya njano dakika ya 80.
Upande wa Leicester City ni James Justin dakika ya 71, Luke Thomas dakika ya 76 na Oliver Skipp dakika ya 89 hawa walionyeshwa kadi ya njano kila mmoja Uwanja wa Etihad.
Matokeo hayo yanaifanya City kufikisha pointi 51 nafasi ya 4 kwenye msimamo baada ya mechi 30 safu ya ushambuliaji imetupia mabao 57 ikiwa imepata ushindi katika mechi 15 poteza 9, sare 6.
Leicester City nafasi ya 19 ina pointi 17 baada ya mechi 30, ushindi ni kwenye mechi 4 poteza mechi 21 na sare 5 msimu wa 2024/25 ambao ushindani wake ni mkubwa na Liverpool inapewa nafasi kubwa kutwaa taji hilo.
WAKALI CHELSEA KUSHUKA UWANJANI
Chelsea watakuwa Uwanja wa Stamford Bridge kuvaana na Tottenham katika mchezo wa Ligi Kuu England ikiwa ni wiki ya 30 na wanapewa asilimia 57 za ushindi wakiwa nyumbani huku Tottenham wakipewa asilimia 21.
Kwenye msimamo Chelsea ipo nafasi ya 6 ikiwa na pointi 49 baada ya mechi 29 safu ya ushambuliaji imetupia mabao 53 na ukuta umeruhusu mabao 37.
Wapinzani wao Tottenham wapo nafasi ya 14 wakiwa na pointi 34 baada ya mechi 29 na safu ya ushambuliaji imetupia mabao 55 ukuta ukiruhusu mabao 43.
Kutoka kikosi cha Chelsea kinara wakutupia mabao ni Cole Palmer ambaye ametupia mabao 14 kibindoni na mkali wa pasi za mwisho za mabao kwa wababe hawa wawili ni Son Heung-min wa Tottenham akiwa ametoa pasi 9.
SOURCE: MAIL ONLINE, PREMIER LEAGUE, LIVERPOOL

