Fei TotoFei Toto

KIVUMBI cha Ligi Kuu Tanzania Bara kinarejea na wababe wanatarajiwa kushuka uwanjani katika dakika 90 za nguvu kusaka pointi tatu msimu wa 2024/25, sio Yanga, Simba, Azam FC pekee bali mpaka Namungo nao watakuwa kazini.

Ni muda wakuvuna mkwanja mrefu kupitia mechi hizi ambazo zimekuwa na ushindani mkubwa kupitia SportPesa.

Safari ya Singida
Farid Mussa kiungo mshambuliaji wa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi. Source: Yanga.

Hapa tunakuletea ratiba ilivyo kwa mechi ambazo zinasubiriwa kwa shauku na mashabiki, wachezaji wanacheza uwanjani ushindi unakuwa kwenye simu yako na SportPesa ukibashiri.

PAMBA JIJI V NAMUNGO

Pamba Jiji v Namungo, Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza inatarajiwa kupigwa saa 8:00 mchana.Kwenye msimamo Pamba Jiji ipo nafasi ya 13 baada ya kucheza mechi 23 ambazo ni dakika 2,070 imekusanya jumla ya pointi 22 kibindoni ilipata ushindi kwenye mechi 5 iliambulia sare 7 na ilipoteza jumla ya mechi 11.

Safu ya ushambuliaji ya Pamba Jiji imetupia jumla ya mabao 14 ikiwa na wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 147 na ukuta umeruhusu jumla ya mabao 25 ina wastani wakufungwa bao moja kila baada ya dakika 82.

Kaseke Pamba
NYOTA wa Pamba Jiji wakiongozwa na Legend, Deus Kaseke jezi namba 13 mgongoni. Source: Pamba Jiji.

 Inakutana na Namungo ambayo safu ya ushambuliaji imetupia mabao 16 ina wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 129 ni mechi 23 ilicheza ambazo ni dakika 2,070 kwenye msimamo ipo nafasi ya 12 na pointi zake kibindoni ni 23. Ukuta wa Namungo umeruhusu jumla ya mabao 28 ukiwa na wastani wakufungwa bao moja kila baada ya dakika 73.

Namungo ilipata ushindi katika mechi 6, sare tano na ilipoteza kwenye mechi 12 msimu wa 2024/25 hivyo wababe hawa wanatarajia kukutana uwanjani kwenye dakika 90 za kuvuja jasho la kusaka pointi tatu muhimu.

TABORA UNITED V YANGA

Tabora United v Yanga mchezo huu wa mzunguko wa pili unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora unatarajiwa kuchezwa saa 10:15 jioni.

Ikumbukwe kwamba Novemba 7 2024 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Yanga 1-3 Tabora United, pointi tatu ziliyeyuka mazima kwa mabingwa watetezi wa ligi zama za Miguel Gamondi.

Tabora United kwa sasa ipo chini ya Genesis Mang’ombe huyu ni kocha anatarajiwa kukaa benchi Aprili 2 2025 baada ya kuchukua mikoba ya Anicet Kiazmak aliyekuwa benchi kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wakati Yanga ikipoteza pointi tatu mazima.

Chikola
NYOTA wa Tabora United Offen Chikola jezi namba 10 alimtungua Diarra kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza, Azam Complex. Source: Tabora United.

Kwenye msimamo Tabora United ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 37 baada ya mechi 23, ushindi ni kwenye mechi 10. Ilipoteza mechi 6 ikiambulia sare kwenye mechi 7 ndani ya msimu wa 2024/25 na safu ya ushambuliaji imetupia mabao 27 ukuta umeruhusu mabao 28.

Tabora United inakutana na safu namba moja kwa kufunga mabao mengi ndani ya ligi ambayo ni 58 na Yanga ni vinara kwenye ligi wakiwa na pointi 58 kibindoni baada ya kucheza jumla ya mechi 22.

KMC V TANZANIA PRISONS

KMC v Tanzania Prisons, Uwanja wa KMC Complex, Dar inatarajiwa kupigwa saa 10:15 jioni kwa wababe hawa kushuka uwanjani kwenye msako wa pointi tatu muhimu. KMC kwenye msimamo ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 24. Ushindi kwa KMC ni mechi sita sawa na idadi ya sare ambazo inazo kibindoni ilipoteza jumla ya mechi 11.

Inawakaribisha Tanzania Prisons walio nafasi ya 15 kibindoni wana pointi 18 baada ya kucheza mechi 23 ambazo ni dakika 2,070. Timu hii ipo kwenye mstari wakushuka daraja mazima.

FOUNTAIN GATE V SINGIDA BLACK STARS

Fountain Gate v Singida Black Stars, Uwanja wa Tanzanite, Kwara Manyara inatarajiwa kupigwa saa 10:15 jioni. Issa Liponda maarufu kama Mbuzi ambaye ni Ofisa Habari wa Fountain Gate amebainisha kuwa ambacho wanahitaji kwenye mchezo wao ni pointi tatu muhimu.

“Tunatambua ushindani ni mkubwa tupo tayari kwa mchezo wetu ukizingatia kwamba tutakuwa nyumbani, kikubwa ni kuvuna pointi tatu mbele ya wapinzani wetu.”

Hussen Masanza, Ofisa Habari wa Singida Black Stars amebainisha kuwa wamefanya maandalizi mazuri na wanahitaji pointi tatu mbele ya Fountain Gate.

APRILI 3 KETE ZITAKUWA NAMNA HII

JKT Tanzania v Dodoma Jiji, Uwanja wa Isahmuhyo, Dar inatarajiwa kuchezwa saa 10:00 jioni.

Ken Gold v Azam FC, Uwanja wa Sokoine, Mbeya inatarajiwa kuchezwa saa 10:00 jioni.

Kagera Sugar v Coastal Union, Uwanja wa Kaitaba, Kagera inatarajiwa kuchezwa saa 1:00 jioni.

Kibu Prosper
Kibu Prosper kiungo mshambuliaji wa Simba, chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids. Source: Simba.

MNYAMA NI MEI

Simba V Mashujaa hii inatarajiwa kuchezwa Mei 2 2025, Uwanja wa KMC Complex, Dar. Aprili 2 2025 Simba itakuwa na kazi kimataifa dhidi ya Al Masry mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya robo fainali na robo fainali ya pili itakuwa Uwanja wa Mkapa, Aprili 9 2025.

Share this: