Jana Jumanne ilikuwa siku ngumu kwa Watanzania wote nah ii ni mara baada ya kushudia timu yetu ya Taifa, Taifa Stars ikikubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya DR Congo katika mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), huku joto la mchezo wa Dabi ya Kariakoo kati ya Simba dhidi ya Yanga likizidi kupanda.

Stars ambao waliingia katika mchezo huo wakihitaji matokeo ya ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu walipoteza kwa kipigo cha mabao mawili ambayo yote yalifungwa kipindi cha pili.
MCHEZO ULIKUWAJE?
Stars ilianza mchezo kwa umiliki mzuri wa mpira na kufanikiwa kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini washambuliaji hawakuzitumia. Mpaka mapumzikotimu hizo zilikuwa hazijafungana kabla ya DR Congo kurejea kipindi cha pili na kuimaliza mechi
WACHAMBUZI WAMTETEA KOCHA HEMED MOROCCO

Licha ya sehemu kubwa ya mashabiki wa Stars kumlaumu kocha, Hemed Morocco lakini baadhi ya wachambuzi wameonyesha kuamini kuwa bado Stars ina nafasi ya kupambana na kufuzu na kuweka wazi kuwa kwa kiasi kikubwa daraja la ubora wa DR Congo ndio liliamua matokeo ya mchezo huo.
Akiuchambua mchezo huo mchambuzi, George Ambangile amesema: ‘’Mpira wa miguu kimsingi ni mchezo wa Mabox mawili ( Unafanya nini katika Box lako kuzuia na unafanya nini katika Box la mpinzani katika kumalizia nafasi zako . Kwa Lugha nyepesi DR Congo wamefanya hayo mambo mawili kwa ufanisi na ndio maana wana haki ya msingi wa kukusanya alama zote tatu.
‘’Tulipambana sana, tumejaribu kucheza kwenye half yao, mpira ukipotea tulihakikisha Congo hawakai nao muda mrefu / kulazimisha makosa kwa muda mrefu tulizuia vizuri kasoro mara tatu tu ambazo mbili tumeadhibiwa na moja Mayele kumiss 1v1. Upande wa pili wa Uwanja kwenye lango la Congo:-
1: Maamuzi sahihi kuna nyakati yalituangusha hasa kwenye zile counter attacks
2: Uzuiaji wa DR Congo ulikuwa mzuri sana (Physically wapo sawasawa, wana kasi, hawapaniki katika nyakati ngumu , kwenye kupambania mpira wapo aggressive haswa )
3: Nafikiri Vijana wetu wamejaribu mpaka pale walipoishia, ni vile tumpe pongezi mpinzani kuna vitu vingi alifanya kwa usahihi dhidi yetu.
Tuna mechi mbili za mwisho muhimu sana . LETS DO IT BOYS, Hii imeisha , focus katika Ethiopia na Guinea .
Naye mchambuzi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu ya JKT Tanzania, Jemedari Said amesema: ‘’Ukocha kazi ngumu sana, unatukanwa na watu hawana hata wanalojua kuhusiana na soka kabisa, hawajasomea mpira, hawajacheza, hawajui lolote kwenye soka hata kuingia dressing room kama kit-manager hajawahi, lakini msikilize mechi kama hii anavyoporomosha matusi kwa, Hemed Morocco tena na mifano ya formation za soka anatoa.
‘’Tofauti ya timu kubwa na ndogo ni matumizi ya nafasi, maamuzi sahihi ya mwisho na ubora mtambuka (wanaocheza na waliopo kwenye benchi).
‘’Mechi yetu tumefungwa na wale walitokea benchi, mpaka kabla ya mabadiliko hakukua na timu iliyoizidi nyingine, ingawa sisi tulitengeneza minor chances ambazo kwa udogo wetu hatukuzifanya kuwa mabao, wenzetu walipozipata tena kupitia kwa watokea benchi wakatumaliza.
‘’Kuna wakati unamuonea huruma kocha Morocco anaangalia mstari wake wa mbele wote wako hoi kwa kuchoka, Kibu, Popa, Mzize na Muda, options zake kwa ushambuliaji ni Selemani Mwalimu wa Fontain Gate FC, Kachwele (kinda)!
‘’Yote kwa yote Congo DR ni wakubwa na wana ubora sana, kwa namna intensity ya match ilivyokuwa na work rate ambayo wachezaji wa Stars waliyokuwa nayo leo kama tungecheza na timu ya kawaida tungeibuka na ushindi, lakini wakubwa Congo DR wamevumilia mwisho wametuua kwa kupata fresh legs zenye quality kutoka bench.
‘’Ubora umeamua mechi bila kujali mifumo wala mpango kazi tumwache Morocco na benchi lake wafanye kazi.
SASA NI SIMBA Vs YANGA JUMAMOSI

Mara baada ya kumalizika kwa majukumu hayo ya kitaifa sasa homa imerejea rasmi kwenye pambano la Dabi ya Kariakoo kati ya Simba ambao wataikaribisha Yanga wanaodhaminiwa na Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa Jumamosi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Simba wataingia kama timu mwenyeji huku wakiwa na rekodi mbaya ya upoteza michezo yao mitatu mfululizo iliyopita. Mchezo huo ni wa pili kwa Simba na Yanga kukutana msimu huu mara baada ya mchezo wa ngao ya Jamii. Uongozi wa Simba umetamba kuwa umejipanga kufanya makubwa Jumamosi.

