Aziz na mpiraAziz na mpira

KUNA joto la kuelekea Kariakoo Dabi linafukuta inatarajiwa kuwa Oktoba 19 2024 Uwanja wa Mkapa kwa Simba inayofundishwa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids kuikaribisha Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.

KARIAKOO Dabi
Wachezaji wa Simba na Yanga kwenye moja ya mchezo wa Kariakoo, Dabi Uwanja wa Mkapa, 2024. Source: Simba.

Yanga inayodhaminiwa na SportPesa ina wakali kwenye mapigo huru hasa mipira ile iliyokufa na Simba pia sio kinyonge wapo wakali kwenye mapigo huru hivyo kwa timu itakayofanya makosa itaadhibiwa kulingana na utumiaji wa nafasi zitakazotengenzwa.

Hapa tunakuletea wakali wa mapigo huru ndani ya Ligi Kuu Bara 2024/25 kutoka timu mbalimbali Bongo namna hii:-

AZIZ KI

Msimu wa 2024/25 kwenye mechi za awali katoa jumla ya pasi mbili za mabao ilikuwa katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Kaitaba alimpa pasi hiyo Clement Mzize dakika ya 88.

Kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Ken Gold alitoa pasi yake ya pili kwa msimu alimpa Ibrahim Bacca ambaye alipachika bao hilo la ushindi lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo na Yanga kukomba pointi tatu mazima.

Ni mkali kwenye mapigo huru huku mguu wake wenye nguvu ni ule wa kushoto ambao huutumia mara kwa mara kwenye kufunga na kutoa pasi za mabao pia. Kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar alipiga kona ikiwa ni ile aliyopiga dakika ya 19.

CLATOUS CHAMA

Yupo ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi ambapo aliibuka hapo akitokea Simba watani wa jadi wa Yanga. Nyota huyo mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia ambao amekuwa akitumia kutimiza majukumu yake.

Mchezo wake wa kwanza akiwa na uzi wa Yanga kwenye ligi ni dhidi ya Kagera Sugar ulichezwa Agosti 29 alianzia benchi katika mchezo huo na aliingia dakika ya 64 akichukua mikoba ya Pacome Zouzoah.

Chama kwenye mchezo huo alipiga kona dakika ya 75, 80 na alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 80 walipokomba pointi tatu muhimu mazima mchezo wa ligi ugenini.

EDWIN BALUA

 

EDWIN Balua
NYOTA wa Simba Edwin Balua na Ahoua wakishangilia moja ya bao kwenye mchezo wa ushindani 2024/25. Source: Simba.

Ediwin Balua kiungo wa Simba mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia ambapo amekuwa akipewa majukumu ya kupiga mapigo huru kwenye mechi za ushindani ndani ya uwanja.

Rekodi zinaonyesha kuwa kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Fountain Gate uliochezwa Uwanja wa KMC, Mwenge Agosti 25 2024 alikuwa na kazi ya kupiga faulo na kona kwenye mchezo huo.

Ilikuwa dakika ya 7, 16, 37, 41 alipiga kona dakika ya 7 ambapo baada ya dakika 90 kwenye mchezo huo ubao ulisoma Simba 4-0 Fountain Gate mchezo wa kwanza Simba kukusanya mabao zaidi ya matatu bila kufungwa msimu wa 2024/25.

EZEKIEL MWASHILINDI

Nyota wa Tanzania Prisons kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Fountain Gate uliochezwa Uwanja wa Sokoine alipachika bao moja dakika ya 48 kwa pigo huru akiwa nje ya 18 likazama ndani ya nyavu.

Mguu wake wa kulia aliutumia akiwa nje kidogo ya 18 kufunga bao hilo katika mchezo wa kwanza Tanzania Prisons kushinda ilikuwa ni Oktoba Mosi baada ya dakika 90 ubao ulisoma Tanzania Prisons 3-2 Fountain Gate.

NURDIN CHONA

Nurdin Chona wa Prisons kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate alipachika bao moja kwa mkwaju wa penalti ilikuwa dakika ya 22 ilisababishwa na Laulen Makame beki wa kazi ambaye mwamuzi Hance Mabena alitafsri kuwa amecheza faulo ndani ya 18.

Makame kutokana na faulo hiyo alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 23 na bao likafungwa na Chona akitumia mguu wa kulia dakika ya 24 kwenye mchezo wa ligi wa kwanza kwa Prisons kushinda msimu wa 2024/25.

AHOUA

 

JEAN Ahoua
Nyota wa Simba Jean Ahoua kwenye majukumu yake moja wa mchezo wa ligi dhidi ya Fountain Gate. Source: Simba.

Jean Ahoua kiungo wa Simba raia wa Ivory Coast alipewa kazi kwenye pigo huru mbele ya Dodoma Jiji mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa ambapo dakika 45 za mwanzo hakuna timu ambayo ilina lango la mpinzani.

Ni Mohamed Hussen Zimbwe Jr alichezewa faulo na Salmin Hoza dakika ya 60 akiwa ndani ya 18 mwamuzi akaamuru upigwe mkwaju wa penalti na ni Hoza alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 62 ya mchezo huo.

Ahoua alifunga bao hilo dakika ya 63 akitumia mguu wa kulia likiipa pointi tatu Simba muhimu ugenini mbele ya Dodoma Jiji chini ya Kocha Mkuu, Mecky Maxime.

Mbali na kufunga pia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex kiungo huyo alikuwa kwenye majukumu ya kupiga faulo na moja ni ile iliyoleta bao kwa Fabrince Ngoma dakika ya 47 yeye alipiga dakika ya 46 kwa mguu wake wa kulia akiwa nje ya 18, kwenye harakati za kuongoa Ngoma akapachika bao la pili.

MAVAMBO

Fadlu na Mavambo
Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba na Fernadez Mavambo kwenye moja ya mchezo wa ushindani 2024. Source: Simba.

Ni ingizo jipya ndani ya Simba chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids kwenye mechi za ushindani ambapo kakabidhiwa jezi namba 17 aliyokuwa akivaa Clatous Chama alipokuwa Simba msimu wa 2023/24.

Mavambo ana uwezo wa kupiga pasi ndefu na fupi na anacheza nafasi zaidi ya moja uwanjani jambo ambalo linampa nafasi ya kujenga utawala wake kwenye kikosi cha Simba.

Sio pasi tu mpaka mapigo huru mwamba huyu ni mkali ambapo rekodi zinaonyesha kuwa kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate alipewa kazi ya kupiga kona alifanya hivyo dakika ya 38.

Share this: