YANGA YATUPA KOMBORA ZITO SIMBA KUELEKEA DABI OKTOBA 19 2024

ByLunyamadizo Mlyuka

October 14, 2024
Dube- AzizDube- AzizDube- Aziz

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa watani zao wa jadi Simba kuelekea kwenye Kariakoo Dabi Oktoba 19 2024 Uwanja wa Mkapa wasianze kubadili maneno bali waendelee na sera zao ambazo walianza nazo mwanzo wa msimu wa 2024/25. Hivyo hilo ni sawa na kombora zito kuelekea kwa watani zao wa jadi Simba.

Ipo wazi kwamba Yanga inayodhaminiwa na SportPesa msimu wa 2023/24 kwenye mechi mbili za ligi ambazo ni dakika 180 walikomba pointi zote sita mazima kwenye uwanja huku wakifunga mabao mengi kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza.

Ali Kamwe
Ali Kamwe Ofisa Habari wa Yanga kuelekea Kariakoo Dabi Oktoba 19 2024, Uwanja wa Mkapa. Source: Yanga.

Ni Uwanja wa Mkapa mchezo ulichezwa baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 1-5 Yanga na pointi tatu zikawa Jwangwani na mzunguko wa pili ilikuwa Yanga 2-1 Simba na pointi tatu nazo zikaelekea mazima Jangwani.

Safu ya ushambuliaji ya Yanga ilifunga mabao 7 na ile ya Simba ilifunga mabao mawili watupiaji kwa Simba ni mkandaji Kibu Dennis kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza na Michel Fred maarufu kama fungafunga kwenye mchezo wa mzunguko wa pili.

HUYU HAPA SEMAJI WA YANGA

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa amewasikia wapinzani wao kwenye redio namna ambavyo wameanza kuwa na heshima kwa wakati huu ikiwa ni muda mchache umebaki kabla ya Kariakoo Dabi jambo ambalo hawajalizoea kuona linakuwa hivyo.

“Nilikuwa kwenye gari hapo kuna rafiki yangu alikuwa anasikiliza michezo na mimi nikatega sikio ili nijue kinachoendelea, hakika nilishangazwa na nilichosikia eti leo wanasema Yanga ni timu kubwa, tunawaheshimu wapinzani wetu! Haya yameanza lini hatujazoea tunataka waendelee na maneno yao yaleyale.

“Walipoanza msimu walikuwa wanakuja na ile sijui ubaya unini sijui sasa naona hawaitumii wanasema Yanga timu kubwa, wakubwa wenzetu tangu lini? Inajulikana Yanga timu kubwa lakini wao walikuwa hawasemi hivyo sasa waendelee na maneno ambayo walianza nayo mwanzo wa msimu.

“Wamebadilika kweli, wamekuwa na adabu kwa sasa haitabadili kitu sisi tunaendelea na maandalizi yetu na ile kauli mbiu yao tunaitaka waendelee kuitumia siku zote mpaka tutakapokutana nao. Waambieni ukweli kwamba Yanga wanatambua wao ni timu kubwa na maandalizi yanaendelea siku zote.”

MAXI HUYU HAPA ATOA NENO

 

MAXI
MAXI Nzengeli kiungo wa Yanga 2024/25. Source: Yanga.

Maxi Nzengeli kiungo mshambuliaji wa Yanga ambaye ni kinara kwenye utupiaji wa mabao ndani ya kikosi hicho akiwa katupia mabao matatu amebainisha kuwa mchezo dhidi ya Simba sio mwepesi huwa unakuwa mgumu siku zote.

“Ni Kariakoo Dabi unajua na tunakwenda kuwakabili wapinzani wagumu. Kila mchezo unahitajika kuwa na mpango kazi wa kutafuta pointi tatu na usisahau kwamba ligi ina ushindani mkubwa na kila timu inapambana kusaka ushindi uwanjani.

“Hakuna hofu ambayo ipo zaidi ni maandalizi mazuri na kuwa tayari kupata matokeo kwenye mchezo wetu ambao unakuja mbele, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwenye kutafuta matokeo inawezekana.”

MWENDO WA YANGA UPO HIVI

 

BACCA
ibrahim Bacca beki wa Yanga ametupia mabao mawili ndani ya ligi 2024/25. Source: Yanga.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi baada ya kucheza mechi nne ambazo ni dakika 360 imekomba ushindi mechi zote nne za Ligi Kuu Bara inayodhaminiwa na NBC.

Kwenye msako wa pointi 12 zote zimewekwa kibindoni mazima kwa mabingwa hao watetezi wa ligi. Safu ya ushambuliaji ya Yanga imefunga mabao 8 na ukuta haujaruhusu kufungwa ndani ya uwanja katika mechi za ushindani.
MATOKEO YA MECHI ZA YANGA
Mchezo wa kwanza Yanga ilikuwa ugenini baada ya dakika 90 ubao ulisoma Kagera Sugar 0-2 Yanga mchezo huu ulichezwa Uwanja wa Kaitaba, Agosti 29 2024 na mtupiaji wa bao la kwanza ni Maxi Nzengeli ndani ya Yanga kwenye ligi.

 

GAMONDI
MIGUEL Gamondi kocha mkuu wa Yanga 2024/25. Source: Yanga.

Mchezo wa pili ilikuwa Ken Gold 0-1 Yanga huu ulikuwa mchezo wa pili kwa Yanga ugenini ilikuwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya mtupiaji alikuwa ni Ibrahim Bacca ambaye alitumia pasi ya Aziz Ki Septemba 25 2024 wakisepa na pointi tatu ugenini.

Yanga 1-0 KMC, mchezo wa kwanza wakiwa Uwanja wa Azam Complex msimu wa 2024/25 ilikuwa Septemba 29 2024. Mchezo wan ne ilikuwa Yanga 4-0 Pamba Jiji ushindi mkubwa kwa Yanga ndani ya 2024/25 walikuwa Azam Complex  ilikuwa Oktoba 3 2024.

 

Share this: