Leeds 1-1 BrentfordDominic

Leeds 1-1 Brentford
Kevin nyota wa Brentford

Ijue ratiba na usajili Premier League:Premier League: Ratiba, Usajili, Vikosi, Matokeo na Mubashara

Leeds 1-1 Brentford ni matokeo ya mchezo wa Premier League 2026/27. Uwanja wa Elland Road ulipigwa mtanange huu mkali. Dominic Calvert-Lewin alisawazisha bao dakika ya 79 baada ya Kevin Schade kuanza kufunga bao kwa Brentford dakika ya 41. Wageni walianza kupata bao la kuongoza kipindi cha kwanza. Dominic aliweka usawa katika kipindi cha pili na kuwafanya wenyeji kupata pointi moja.

Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa

Una nafasi yakushinda mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa. Rubani makini anapaa angani akiwa na uhakika. Mwanzo wa wiki muda sahihi kuvuna mamilioni. Bofya hapa chini ushinde sasa hivi.

Leeds 1-1 Brentford taarifa muhimu

Tukio Maelezo
Timu Wenyeji Leeds United
Timu Wageni Brentford
Uwanja Elland Road
Tarehe Agosti 30, 2026
Matokeo Leeds 1-1 Brentford
Mashindano Ligi Kuu Uingereza 2026/27

Leeds 1-1 Brentford takwimu

Mabao 1-1
Mashuti 12-22
Mashuti yaliyolenga lango 2-5
Umiliki 46.6%-53.4%
Pasi zilizofanikiwa 282-333
Pasi ndefu 59-48
Kona 5-6

Takwimu za hapo awali (head-to-head) na fomu ya sasa

Historia ya michezo kati ya Leeds United na Brentford imeonyesha ushindani mkali. Katika msimu uliopita wa 2025/26, timu hizi zilitoka sare ya 0-0 Uwanja wa Elland Road, ikionyesha jinsi michezo yao inavyokuwa migumu.

Maoni ya makocha

Kocha Mkuu wa Leeds Daniel Farke wachezaji wake waliandika rekodi ya kupiga mashuti huku wenyeji wakipiga mashuti 12. Uwepo wa mshambuliaji Lukas Nmecha katika kipindi cha pili uliongeza nguvu katika mashuti. Calvert-Lewin alikuwa ni shujaa aliyebadili usomaji wa matokeo kwa upande wa timu ya nyumbani.

Kocha huyo amesema anajivunia wachezaji wake. Ameongeza kuwa ulikuwa ni mchezo mgumu. Kuhusu wapinzani wake walikuwa bora kipindi cha kwanza.

“Ninajivunia kwa namna wachezaji wanavyofanya kazi. Mchezo wetu ulikuwa mgumu kama ambavyo tulitarajia. Walikuwa bora kwetu hada kipindi cha kwanza na walistahili kuongoza. Tulijitahidi kubadilisha kila kitu, tulibadili mfumo kipindi cha pili na mwisho tukapata bao,”.

Kwa upande wa Brentford, Kocha Mkuu, Keith Andrew amesema ulikuwa ni mchezo wa tofauti. Aliongeza kuwa walifanya mabadiliko na kutengeneza nafasi.

“Tulicheza hapa Machi ilikuwa 0-0 huu ulikuwa mchezo tofauti. Tulikuja na mbinu nyingine. Tulikuwa na kipindi cha kwanza kilichokuwa na upekee,”

Mfungaji wa bao la kusawazisha

Mshambuliaji wa Leeds Dominic Calvert-Lewin amesema kuwa anafurahi kuandika rekodi hiyo. Ameongeza kuwa ni furaha kuwa na timu hiyo.

“Ninafurahia kuwa hapa. Imekuwa ni safari ndefu kutoka nilipokuwa mpaka hapa. Ninajisikia vizuri na ninafurahia kucheza. Tuna jukumu la kufanya na kuangalia yalitotokea msimu uliopita n kujenga timu hatua kwa hatua,” amesema kupitia Sky Sports.

Nafasi

Brentford nafasi ya 5 pointi 4
Leeds nafasi ya 8 pointi 4

Hitimisho

Leeds 1-1 Brentford matokeo ambayo yameonyesha faida ya kuwa nyumbani. Timu zote mbili zimefikisha jumla ya pointi 4 kibindoni. Burudani ya wababe hawa ilikuwa ndani ya Uwanja wa Elland Road.

Share this: