Kamwe Caf -Kamwe Caf -
YANGA
Fei Toto

Huku kukiwa na taarifa zisizo rasmi za kumhusu staa wa kikosi cha Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ kuwaniwa chini chini na wababe wa Kariakoo, klabu za Simba na Yanga, hatimaye uongozi wa Yanga wanaodhaminiwa na kampuni bora ya kubashiri ya SportPesa kupitia kwa Ofisa habari wa timu hiyo, Ali Kamwe ametoa tamko zito kuhusu hatima ya Fei Toto kuvaa tena jezi ya Yanga

ISHU IMEANZIA WAPI?

Mara baada ya kuwa na mafanikio makubwa katika msimu wake wa kwanza akiwa na kikosi cha klabu ya Azam akifanikiwa kuibuka mfungaji bora namba 2 nyuma ya Aziz Ki baada ya kufunga mabao 19 zikaibuka taarifa kjwenye dirisha kubwa la usajili juu ya kuwepo mpango wa Simba kumhitaji Fei Toto kama mbadala wa Chama aliyekuwa ametimkia ndani ya kikosi cha timu ya Yanga na licha ya kuthibitika kuwepo mazungumzo kati ya Simba na Fei Toto lakini staa huyo amesalia ndani ya Azam.

FEI TOTO AFICHUA WAMEMALIZANA NA INJINIA

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Fei Toto amenukuliwa akisema licha ya hapo awali kuwepo kwa sintofahamu kati yake na Rais wa Yanga, Injinia Hersi lakini kwa sasa wawili hao wana mahusiano mazuri na amekuwa akipokea ushauri mwingi kutoka kwa kiongozi huyo.

YANGA WATOA MSIMAMO

YANGA
Ali Kamwe

Kufuatia ishu hiyo, Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe ametumia jukwaa la akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram kulitolea ufafanuzi ambapo aliandika ujumbe ufuatao: “Nimemsikia FeiToto akisema Hana shida ya Eng Hersi Said. Wanaongea na anapokea pia ushauri mwingi kutoka kwake. Feitoto pia kasema yuko tayari kucheza tena ndani ya Jezi Bora aipendayo ya Yanga.

“Nimemsikia yule winga Sillah akionyesha tamaa yake ya kutaka kuja Yanga. Binafsi haijanishtua sana. Hivi sasa ni ndoto ya kila mchezaji kuvaa jezi ya Yanga ili afikie kilele cha ubora wake. Kauli za hao wachezaji wawili kutoka Chamazi, zimeonyesha ni kwa kiasi gani daraja la UTU wa viongozi na UBORA wa Kikosi chetu ulivyo hivi sasa.

“Niseme tu, tajiri  GSM ameshasikia kilio cha Sillah na Wananchi Tumeshamsamehe FEITOTO. Hawa ni wachezaji wazuri wanaostahili kucheza CAF CHAMPIONS LEAGUE kwenye Hatua kubwakubwa na kufaidi Bonus ya Hela ya Rais wa Nchi. Nichukue fursa hii KUMKARIBISHA FEITOTO na SILLAH waje New Amaan Complex kuungana na Wananchi tukiishangilia timu yetu.

“Tiketi za Ndege, gharama za Hotel, kula na kunywa ni juu yetu sisi, wao jukumu lao ni kutoroka tu kule Mbande na Kuja kula Raha Zanzibar. Mwenzao, Dube alianzaga kushangilia Jukwaani sasa tunamshangilia Yeye.”

AZAM WATHIBITISHA KUPOKEA OFA

YANGA
Hasheem Ibwe

Kupitia kwa msemaji wa Azam, Hashim Ibwe ameweka wazi kuwa ni kweli wamewahi kupokea ofa kadhaa kutoka kwa timu kubwa hapa Tanzania na nje ya nchi, lakini akaweka wazi kuwa hakuna timu Tanzania inayoweza kumnunua Fei Toto kwa sasa.

JUMAMOSI NI YANGA ZANZIBAR, JUMAPILI SIMBA KWA MKAPA

YANGA
Ahmed Ally

Ukiachana na stori hiyo kubwa ya Fei Toto, ikumbukwe Wikiendi hii  Dar es Salaam inatarajiwa kuwa bize sana kuandaa michezo miwili mikubwa yenye maana kubwa kwa ushiriki wa Tanzania kimataifa msimu huu.

Wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Yanga baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya CBE SA ya Ethiopia, Jumamosi watakuwa na kibarua cha kumaliza mkia baada ya kula ng’ombe mzima pale watakapowaalika CBE SA katika mchezo wa marudiano wa mashindano hayo utakaopigwa Uwanja wa New Amaan Complex.

Kufuatia matokeo yua mchezo wa mkondo wa kwanza, Yanga sasa ni kama wametanguliza hatua moja kuelekea hatua ya makundi ya mashindano hayo na sasa wanahitaji angalau matokeo ya sare tu, katika mchezo wa marudiano ili kujihakikishia tiketi ya kucheza hatua ya makundi.

Wakati Jumamosi Yanga wakimalizana na Waethiopia Zanzibar, watani zao Simba Jumapili watashuka Uwanja wa, Benjamin Mkapa kuvaana na Al Ahly Tripoli katika mchezo wa marudiano. Ikumbukwe mchezo wa kwanza Simba walipata suluhu, hivyo kwenye mchezo huu wanahitaji matokeo ya ushindi wowote ili kufuzu hatua ya makundi.

 

 

 

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.