LALA Salama-Ligi kuuazizi-ki-pic

REKODI zinaandikwa ili zivunjwe na kuna wachezaji ambao kila iitwapo leo wanaandika rekodi mpya na kuzivunja wenyewe ndani ya uwanja kwenye kuvuja jasho. Hilo tupa kule kuna miamba wawili msimu wa 2023/24 walifanya kazi kwa kuandika rekodi zao tamu.

Ni Aziz Ki wa Yanga inayodhaminiwa na SportPesa na Feisal Salum maarufu kama Fei Toto wa Azam FC, wote walikuwa kwenye ubora na watakuwa ndani ya ligi kwa mara nyingine msimu wa 2024/25 huku swali ikiwa watavunja rekodi zao.

Kwenye upande wa kucheza na nyavu rekodi ziliandikwa na mwamba Aziz kuwa mfungaji bora akiwa na mabao 21 mshindani wake wa karibu Feisal Salum wa Azam FC alikuwa namba mbili alifunga mabao 19.

Hizi hapa rekodi zao ambazo zinasubiriwa kuvunjwa kwenye kila kipengele kwa mastaa hao msimu mpya ambao una ushindani mkubwa kwa kila timu kupambania kufikia malengo namna hii:-

Aziz KI Yanga
Aziz KI rekodi yake ni mkali wa kutumia mguu wa kushoto. Source: Yanga.

MABAO YA MGUU WA KUSHOTO

Kila mchezaji ana mguu wake wenye nguvu na hapa Aziz Ki wa Yanga kwenye eneo alikuwa ni namba moja ambapo alitumia mguu huo kufunga jumla ya mabao 17. Feisal Salum wa Azam FC hakuwa nyuma na alifanikiwa kufunga jumla ya mabao 4.

Kinara alikuwa ni Aziz kwenye kutumia mguu wa kushoto kwa kuwa tofauti ya idadi ya mabao 13 ili kufanikiwa kuwa naye sambaba kwenye idadi hiyo. Kikubwa ambacho kinasubiriwa msimu mpya ni nani atakuwa shujaa kwenye kuvunja rekodi hizo.

UBABE UPANDE WA MGUU WA KULIA

FEI
Kiungo Fei Toto ni mkali kwenye rekodi upande wa kutumia mguu wa kulia. Source: Azam FC.

Feisal hakuwa mnyonge kwenye upande wa mguu wa kulia hapa nguvu zake ziliegemea kweli ambapo kwenye eneo la mguu wa kulia Feisal alikuwa namba moja alipofunga mabao 13.

Wakati Feisal akifunga mabao hayo 13 Aziz Ki ni mabao matatu alifunga. Alikuwa tofauti ya mabao 10 kwa upande wa mguu wa kulia ambao ulikuwa na nguvu kwa kiungo wa Azam FC, Feisal.

NDANI YA 18

Hapa wote walikuwa wakali wakiwa ndani ya 18 lakini Feisal alikuwa na hatari zaidi ambapo alifunga jumla ya mabao 17 akiwa kwenye eneo hilo. Mwamba Aziz Ki yeye alifunga jumla ya mabao 15 akiwa ndani ya 18. Hivyo alizidiwa mabao mawili pekee kwenye ukali wa kutupia mabao ndani ya 18.

NJE YA 18

Aziz Ki katupia mabao sita akiwa nje ya 18. Miongoni mwa timu aliyofunga akiwa nje ya 18 ilikuwa dhidi ya Tabora United alipofunga bao lake la 10 ndani ya ligi ilikuwa kwa pigo huru akitumia mguu wake wa kushoto. Kiung Feisal alitupia mabao mawili akiwa nje ya 18. Bao lake la19 la kufungia msimu alipachika akiwa nje ya 18 dhidi ya Geita Gold walipokomba pointi tatu ugenini.

KUTENGENEZA PASI ZA MABAOA

 

Aziz Ki
Kinara wa utupiaji ndani ya ligi msimu wa 2023/24 akiwa na rekodi ya kufunga mabao mengi. Source: Yanga.

 Aziz Ki alitengeneza jumla ya pasi 8 za mabao ndani ya ligi. Pasi yake ya kwanza aliitoa dakika ya 64 kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Uwanja wa Azam Complex akiwa nje ya 18.

Feisal alitengeneza jumla ya pasi 7, alitoa pasi ya kwanza kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa, Uwanja wa Lake Tanganyika dakika ya 68. Kwenye mchezo huo walisepa na pointi tatu ugenini na alitoa pasi mbili ile ya pili alitoa dakika ya 72 mchezo ulichezwa Novemba Mosi 2023.

REKODI YA MABAO WALIYOHUSIKA

Aziz Ki alihusika kwenye mabao 29 kati ya 71 yaliyofungwa na Yanga ambao ni mabingwa wa ligi msimu wa 2023/24. Ipo wazi kwamba Yanga ni namba moja kwa timu ambazo zilifunga mabao mengi na safu yao ya ushambuliaji kuruhusu mabao machache ambayo ni 14.

 

FEI TOT
Kiungo wa Azam FC, Feisal Salum mwenye rekodi ya kuwa mzawa mwenye mabao mengi 2023/24. Source: Azam FC.

Feisal alihusika kwenye mabao 26 ikiwa ni rekodi yake kati ya 63 yaliyofungwa na timu hiyo ikiwa ni namba mbili kwa timu zilizofunga mabao mengi. Ukiweka kando kuwa namba mbili kwa safu kali ya ushambuliaji na ile ya ulinzi ni namba mbili ikiwa imeruhusu mabao 21.

Tayari kasi kwa msimu mpya imeanza huku kila mchezaji akiwa na mipango yake na kila timu ikiwa na malengo mapya ndani ya uwanja 2024/25 tusubiri na tuone nani atakuwa nani.

Share this: