Ally Kamwe - Ofisa Habari YangaAlly Kamwe - Ofisa Habari Yanga
YANGA
Clatous Chama wa Yanga na walinzi wa CBE SA (Source-Yanga)

Mara baada ya kupata ushindi muhimu wa bao 1-0 ugenini dhidi ya CBE SA ya Ethiopia kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, uongozi wa Yanga umetangaza kuwa wamejiandaa kufanya balaa kubwa kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumamosi kwenye Juwanja wa Amaan, Zanzibar.

Akizungumzia maandalizi yao kuelekea mchezo huo, Ofisa habari wa Yanga ambao wanadhaminiwa na Kampuni bora ya ubashiri ya SportPesa, Ali Kamwe amesema: “Kwa pamoja na Wazee wetu Hapa Zanzibar Tumekubaliana kuwa siku ya Ijumaa tutafanya Dua kubwa sana kwa ajili ya Mambo Makubwa matatu;

1: Kuwaombea wachezaji wetu Mwenyezi Mungu awaepushe na Majeraha, awape nguvu na kheri ya kufanikiwa katika kila jambo wanapokuwa uwanjani.

2: Tutawaombea kwa Mwenyezi Mungu makocha wetu wapate Afya na Maarifa zaidi katika kila wanachokiwaza kiwe na kheri ndani yake.

3: Kujiombea Kinga mashabiki wa Yanga tuepushwe na Husda na Roho mbaya za wapinzani wetu mitaani wanaotamani kuishi kwa Raha kama sisi. Baada ya dua tutakwenda kutoa msaada katika kituo cha watoto Yatima na Kisha Tutakunywa Supu Tena. Huu msimu hatucheki na watu. Jumamosi wachezaji wetu wataingia Uwanjani wakiwa ‘CLEAN’ KABISAA IN SHAA ALLAH na Tutapata Burudani kubwa mno.”

YANGA WANAHITAJI SARE TU, KUTINGA MAKUNDI

Wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Yanga baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya CBE SA ya Ethiopia ambapoi kwa matokeo hayo, Yanga sasa ni kama wametanguliza hatua moja kuelekea hatua ya makundi ya mashindano hayo na sasa wanahitaji angalau matokeo ya sare tu, katika mchezo wa marudiano ili kujihakikishia tiketi ya kucheza hatua ya makundi.

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Ethiopia, goli pekee la Yanga lilifungwa na straika wa kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube mwishoni mwa kipindi cha kwanza. Katika mchezo huo Yanga walicheza kwa kasi ya chini kulinganisha na kawaida yao, lakini walifanikiwa kutawala sehemu kubwa ya mchezo huo na kufanikiwa kutengeneza nafasi zaidi ya tano za wazi ambazo wachezaji; Clatous Chama, Stephanie Aziz Ki, Prince Dube, Maxi Nzengeli walishindwa kuzitumia wakikosa mabao ya wazi na kufanya mchezo umalizike kwa ushindi huo mwembamba wa bao 1-0.

SIMBA KURUDI JUMATANO KUANDAA UBAYA UBWELA WA WALIBYA

Mara baada ya wawakilishi wengine wa Tanzania kimataifa Simba Jumapili usiku kupata matokeo ya suluhu ugenini dhidi ya Al Ahly Tripoli kikosi cha timu hiyo kinatarajia  kuanza safari ya kurudi nchini Jumanne hii ambapo watapitia Uturuki kabla ya kutua Dar es Salaam, Alfajiri ya Jumatano.

Simba wanarejea nchini kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa marudiano dhidi ya Al Ahly Tripoli ambao ni mchezo wa mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambao unatarajiwa kupigwa siku ya Jumapili.

HIKI HAPA KIKOSI CHA SIMBA KITAKACHOTUA DAR ES SALAAM JUMATANO ASUBUHI

YANGA
Kikosi cha Simba (Source – Simba)

Makipa

  1. Aishi Manula
  2. Moussa Camara
  3. Ally Salim

 

Walinzi

  1. Shomari Kapombe
  2. Kelvin Kijiri
  3. Mohamed Hussein
  4. Valentin Nouma
  5. Che Malone Fondoh
  6. Karaboue Chamou
  7. Abdurazack Hamza

 

Viungo

  1. Augustine Okejepha
  2. Debora Fernandes
  3. Awesu Awesu
  4. Yusuph Kagoma
  5. Joshua Mutale
  6. Edwin Balua
  7. Fabrice Ngoma
  8. Jean Chalres Ahoua
  9. Kibu Denis

 

Washambuliaji

  1. Steven Mukwala
  2. Leonel Ateba
  3. Valentino Mashaka

 

ALICHOSEMA AHMED

YANGA
Ahmed Ally

Kuelekea mchezo huo dhidi ya Al Ajly Tripoli, Meneja wa habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amewaomba mashabiki wa Simba wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao kwa kuweka wazi kuwa wao ndio wana nafasi kubwa ya kutumika kama funguo ya kuipeleka Simba hatua ya Makundi.

“Wanasimba natumai mmeamka salama nasi huku Libya tumeamka salama sana wote tupo katika hali nzuriiii, kikosi kitaanza safari Jumanne Mchana kupitia Uturuki na tutafika Dar Es Salaam Jumatano Alfajiri Insha Allah. Tunaanzia hapa Wanasimba, wao waliingia Uwanjani Mashabiki 50,065 kwa idadi ya Uwanja wao hiyo ilikua ni full house. Septemba 22, tunatakiwa kuilipa hii kwa full house ya 60,000 kwa Mkapa.”

 

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.