
Mara baada ya kupumzika nchini Uturuki, kikosi cha wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika Simba kimewasili salama nchini Libya, tayari kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa kwanza wa mashindano hayo dhidi ya wenyeji wao Al Ahly Tripoli.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa nchini Libya siku ya keshokutwa Jumapili Septemba 15, 2024 ambapo unaweza kuvuna mamilioni kwa kuweka bashiri yako na Kampuni bora ya ubashiri ya SportPesa. Kikosi cha Simba kiliondoka nchini usiku wa kuamkia Jumatano na kufika nchini uturuki ambapo walipumzika kabla ya Alhamisi asubuhi kuanza tena safari ya kutoka Uturuki na kuelekea Libya.
MASTAA WA TIMU ZA TAIFA WAMEFIKA
Baadhi ya wachezaji wa Simba ambao walikuwa wameungana na vikosi vya timu za Mataifa yao kwa ajili ya ratiba ya michezo ya kimataifa kusaka tiketi ya kufuzu kushiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), tayari wameungana na wenzao kwa ajili ya mchezo huo, mastaa hao ni; Ally Salim Mohamed Hussein, Edwin Balua waliokuwa na timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars na kipa, Moussa Camara ambaye alikuwa na timu ya Taifa ya Guinea.
KOCHA SIMBA ATENGA SIKU TATU KUWAUA WALIBYA
Baada ya kuwasili Libya wachezaji wa Simba walipata saa chache za kupumzika kabla ya jioni kuanza programu ya mazoezi, ambapo kocha mkuu wa timu hiyo ameandaa program ya siku tatu, kabla ya kukutana na Al Ahly Tripoli ili kuwafanya wachezaji wake kuzoea hali ya hewa.
AL AHLY TRIPOLI NI TIMU YA AINA GANI?
Akizungumzia ubora wa wapinzani wao, meneja wa habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema wanakabiriwa na kibarua kigumu mbele ya Walibya hao kutokana na ubora wao katika miaka ya karibuni na uwekezaji walioufanya kupitia usajili.
“Wana Simba tumjue vema mpinzani wetu tunaecheza nae mechi ya Kombe la Shirikisho. Ahly Tripoli ni klabu ya pili kwa mafanikio Nchini Libya, lakin ndio klabu yenye mafanikio zaidi kimataifa nchini kwao. Mafanikio yao makubwa ni kucheza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Afrika mwaka 2022 na Robo fainali ligi ya mabingwa Afrika 2017.
“Msimu uliopita walimaliza nafasi ya tatu, Kufuatia kutoridhishwa na matokeo hayo, wakafanya usajili mkubwa ili kurejesha heshima yao. Miongoni mwa usajili wa kushtua walioufanya ni ule wa Mabululu ambae amesajiliwa kwa dau la makadirio ya Bilioni 4 na inatajwa kuwa ndio usajili mkubwa zaidi katika historia ya klabu hiyo. Kwa maelezo haya machache ni ishara kuwa tunaenda kukutana na mpinzani mgumu kweli kweli hivyo basi Wana Simba tuanze kujipanga vema kwa vita hii.
“Mechi ya kwanza ni Septemba 15, Mechi hii ya ugenini tunawategemea zaidi wachezaji wetu wapambane kadri ya uwezo wao. Mechi ya pili ni Septemba 22, mwaka 2024 Benjamin Mkapa hii inatutegemea sisi Mashabiki kuipeleka Simba yetu hatua ya makundi. Katika Matawi yetu, Makundi yetu, Vijiwe vyetu mipango ya kuuvamia Uwanja wa Mkapa ianze sasa. Tuanze kuhamasishana kwenda Uwanjani Sept 22.
“Maamuzi ya kwenda Makundi yapo mikononi mwetu wana Simba, mengi zaidi tutajulishana muda ukifika lakini nimedokeza tuu ila hamasa ianze mapema kwenye maeneo yetu ‘Ubaya Ubwela + Pumzi ya Moto.”
HIKI HAPA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOWAFUATA WALIBYA

Makipa
- Aishi Manula
- Moussa Camara
- Ally Salim
Walinzi
- Shomari Kapombe
- Kelvin Kijiri
- Mohamed Hussein
- Valentin Nouma
- Che Malone Fondoh
- Karaboue Chamou
- Abdurazack Hamza
Viungo
- Augustine Okejepha
- Debora Fernandes
- Awesu Awesu
- Yusuph Kagoma
- Joshua Mutale
- Edwin Balua
- Fabrice Ngoma
- Jean Chalres Ahoua
- Kibu Denis
Washambuliaji
- Steven Mukwala
- Leonel Ateba
- Valentino Mashaka
ISHU YA KAGOMA PASUA KICHWA

Kufuatia taarifa mbalimbali ambazo zimeripotiwa katika mitandao ya kijamii kuhusu vuta nikuvute ya mkataba wa kiungo wa Simba, Yusuph Kagoma na klabu za Yanga na Fountain Gate, uongozi wa Yanga kupitia Mkuu wa kitengo chao cha sheria Wakili, Simon Patrick wametoa ufafanuzi mzito kuhusu jambo hilo wakisisitiza kuwa mchezaji huyo ni mali yao.
“Tulianzisha maongezi ya muda mrefu na Singida Fountain Gate ilikusudi Yanga imnunue rasmi Yusuf Kagoma. Masharti waliyotupa Singida ni kulipa million 30, na sisi tulisema tutalipa kwa awamu mbili na tarehe 30 mwezi wa nne tuliilipa Singida Fountain Gate pesa yote.
“Baada ya kufanya malipo klabu ya Yanga iliruhusiwa kufanya mazungumzo na mchezaji kwa ajili ya maslahi binafsi na baada ya hapo, Yanga ilimtumia Yusuph kagoma tiketi ya ndege ili aje kusaini mkataba na hivyo Kagoma aliwakilishwa na Wakili wake Bwana Léonard na yeye mwenyewe akaweka saini. Kwahiyo tunaweza kusema Kagoma bado ni mchezaji wetu,” amesema mwanasheria wa Yanga, Simon Patrick

