- CRDB Federation Cup 2026 rasmi imeingia hatua ya Nusu Fainali.
- Yanga SC na Coastal Union ni timu 2 ambazo tayari zimefanikiwa kutinga hatua hiyo, kwa matokeo ya JKT Tanzania 0-2 Yanga SC na Coastal Union 4-2 Singida Black Stars (Penalti).
- Yanga SC na Coastal Union sasa wanasubiri washindi wa mechi za Simba SC vs TRA United na Mashujaa FC vs Azam FC.
- Wakati hayo yakijiri joto limeanza kupanda kuhusu uwezekano wa Kariakoo dabi nyingine kwenye michuano hii, Je, Yanga na Simba SC wana nafasi ya kukutana tena?
Yanga SC imefanikiwa kutinga hatua ya Nusu Fainali ya CRDB Federation Cup 2026, hii ni baada ya dakika 90 za Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kushuhudia ubao ukiandikwa JKT Tanzania 0-2 Yanga SC. Katika hatua hiyo ya Nusu Fainali Yanga SC, wanatarajiwa kuvaana na mshindi wa mchezo wa Mashujaa FC vs Azam FC ambao utapigwa kesho Jumapili. Kitendawili Kikubwa ni Je, Yanga na Simba SC wana nafasi ya kukutana tena fainali?
Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya CRDB Federation 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.
Unataka kushinda mamilioni? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Aviator: Paisha kindege ushinde mpaka zaidi ya 800,000,000.
Kuhusu mechi ya JKT Tanzania 0-2 Yanga SC CRDB Federation Cup 2026

Hii ilikuwa ni Robo fainali ya pili ya CRDB Federation Cup 2026 ambayo ilipigwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam kuanzia saa 12:30 jioni. Mabao ya Mudathir Yahya na lile la kujifunga la, Hassan Wahabi yalitosha kupeleka kilio kwa wenyeji. Ushindi huu ulikuwa muhimu kwa Yanga SC hasa baada ya timu hiyo kutoka kwenye kipigo cha matokeo ya Dodoma Jiji 3-2 Yanga SC.
SOMA HII PIA: Timu 8 Robo Fainali CRDB Federation Cup: Simba, Yanga, Azam uso kwa uso
JKT Tanzania vs Yanga SC, H2H
Huu ulikuwa mchezo wa 20 kwa timu hizi kukutana, ambapo Yanga SC wameandika rekodi ya kushinda mechi 15, na JKT Tanzania bado haijaonja ladha ya ushindi. Mechi 5 katika mikutano yao hakukupatikana mbabe. Hivyo hii ni nafasi kwa kila timu kuandika historia mpya.
SOMA HII PIA: JKT Tanzania vs Yanga SC : Robo Fainali CRDB Federation| Ratiba, matokeo, msimamo, utabiri, Livescore, h2h, na Habari za timu
Yanga SC kukutana na Simba SC tena?

Wakati Yanga SC wakitinga Nusu Fainali, harufu ya kuweza kushuhudia dabi ya Kariakoo yaani mechi ya Simba SC vs Yanga SC kwa mara ya 5 msimu huu imezidi kuongezeka. Hii inawezekanaje? Iko hivi, Yanga SC wanatarajia kuvaana na mshindi wa mechi ya Nusu Fainali ya 3 kati ya Mashujaa vs Azam kwenye Nusu Fainali. Ikiwa watashinda watafuzu Fainali, huku upande wa pili Simba naye akishinda mechi zake 2 zijazo basi watakutana Fainali.
Ikumbukwe timu hizo zimekutana mara 4 msimu huu, ambapo unaweza sema hakuna mbabe kwani, kila timu imeshinda mechi moja huku mechi 2 zilizosalia zikiisha kwa sare. Hii itakuwa rekodi nyingine kwa wababe hao kukutana mara 5, ndani ya msimu mmoja. Muda utatoa majibu sahihi, kwa sasa mashabiki wana nafasi ya kuinjoi mechi za Robo na Nusu Fainali.
SOMA HII ZAIDI: Muonekano wa matokeo ya droo ya Robo Fainali CRDB Federation Cup
Hitimisho

Mashindano ya CRDB Federation Cup 2026 yanazidi kupamba moto, kwa sasa yameingia katika hatua ya Nusu Fainali. Tayari timu 2 ambazo ni Yanga SC na Coastal Union zimeshatangulia. Kazi sasa imesalia kwa Simba SC, Azam FC, Mashujaa FC na TRA United kuona ni timu 2 zipi zinaweza kutinga hatua hiyo.

