MATOKEO CBE Vs YANGAMATOKEO CBE Vs YANGA

Wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Yanga ambao wanadhaminiwa na Kampuni bora ya michezo ya kubashiri SportPesa muda mchache uliopita wamefanikiwa kuibuka na ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya CBE SA ya Ethiopia.

Katika mchezo huo goli pekee la Yanga limefungwa na straika wa kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube mwishoni mwa kipindi cha kwanza.

MCHEZO ULIKUWAJE?

YANGA
Clatous Chama wa Yanga dhidi ya Walinzi wa CBE (Source: Yanga)

Licha ya kucheza kwa kasi ya chini kjulinganisha na kawaida yao, Yanga walionekana kutawala sehemu kubwa ya mchezo huo na kufanikiwa kutengeneza nafasi zaidi ya tano za wazi ambazo wachezaji; Clatous Chama, Stephanie Aziz Ki, Prince Dube, Maxi Nzengeli walishindwa kuzitumia wakikosa mabao ya wazi na kufanya mchezo umalizike kwa ushindi huo mwembamba kwa Yanga wa bao 1-0.

NINI KINAFUATA?

Kwa matokeo hayo Yanga sasani kama wametanguliza hatua moja kuelekea hatua ya makundi ya mashindano hayo na sasa wanahitaji angalau matokeo ya sare tu, katika mchezo wa marudiano ili kujihakikishia tiketi ya kucheza hatua ya makundi.

SIMBA KINAWAKA UTRUKI KESHO JUMAPILI

YANGA
Edwin Balua (Source: Simba)

Mara baada ya kuwa na siku tatu za programu ya maandalizi baada ya kufika nchini Libya, wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika Simba kesho Jumapili wanatarajia kushuka uwanjani kuvaana na wenyeji wao Al Ahly Tripoli.

Ikumbukwe kikosi cha Simba kiliondoka nchini usiku wa kuamkia Jumatano na kufika nchini uturuki ambapo walipumzika kabla ya Alhamisi asubuhi kuanza tena safari ya kutoka Uturuki na kuelekea Libya.

CAMARA, ZIMBWE MAMBO SAFI

Baadhi ya wachezaji wa Simba ambao walikuwa wameungana na vikosi vya timu za Mataifa yao kwa ajili ya ratiba ya michezo ya kimataifa kusaka tiketi ya kufuzu kushiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), tayari wameungana na wenzao kwa ajili ya mchezo huo, mastaa hao ni; Ally Salim Mohamed Hussein, Edwin Balua waliokuwa na timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars na kipa, Moussa Camara ambaye alikuwa na timu ya Taifa ya Guinea.

AL AHLY TRIPOLI NI TIMU YA AINA GANI?

YANGA
Ahmed Ally

Akizungumzia ubora wa wapinzani wao, meneja wa habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema wanakabiriwa na kibarua kigumu mbele ya Walibya hao kutokana na ubora wao katika miaka ya karibuni na uwekezaji walioufanya kupitia usajili.

“Wana Simba tumjue vema mpinzani wetu tunaecheza nae mechi ya Kombe la Shirikisho. Ahly Tripoli ni klabu ya pili kwa mafanikio Nchini Libya, lakin ndio klabu yenye mafanikio zaidi kimataifa nchini kwao. Mafanikio yao makubwa ni kucheza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Afrika mwaka 2022 na Robo fainali ligi ya mabingwa Afrika 2017.

“Msimu uliopita walimaliza nafasi ya tatu, Kufuatia kutoridhishwa na matokeo hayo, wakafanya usajili mkubwa ili kurejesha heshima yao. Miongoni mwa usajili wa kushtua walioufanya ni ule wa Mabululu ambae amesajiliwa kwa dau la makadirio ya Bilioni 4 na inatajwa kuwa ndio usajili mkubwa zaidi katika historia ya klabu hiyo. Kwa maelezo haya machache ni ishara kuwa tunaenda kukutana na mpinzani mgumu kweli kweli hivyo basi Wana Simba tuanze kujipanga vema kwa vita hii.

“Mechi ya kwanza ni Septemba 15, Mechi hii ya ugenini tunawategemea zaidi wachezaji wetu wapambane kadri ya uwezo wao. Mechi ya pili ni Septemba 22, mwaka 2024 Benjamin Mkapa hii inatutegemea sisi Mashabiki kuipeleka Simba yetu hatua ya makundi. Katika Matawi yetu, Makundi yetu, Vijiwe vyetu mipango ya kuuvamia Uwanja wa Mkapa ianze sasa. Tuanze kuhamasishana kwenda Uwanjani Sept 22.

“Maamuzi ya kwenda Makundi yapo mikononi mwetu wana Simba, mengi zaidi tutajulishana muda ukifika lakini nimedokeza tuu ila hamasa ianze mapema kwenye maeneo yetu ‘Ubaya Ubwela + Pumzi ya Moto.”

HIKI HAPA KIKOSI CHA SIMBA KILICHOWAFUATA WALIBYA

Makipa

  1. Aishi Manula
  2. Moussa Camara
  3. Ally Salim

 

Walinzi

  1. Shomari Kapombe
  2. Kelvin Kijiri
  3. Mohamed Hussein
  4. Valentin Nouma
  5. Che Malone Fondoh
  6. Karaboue Chamou
  7. Abdurazack Hamza

 

Viungo

  1. Augustine Okejepha
  2. Debora Fernandes
  3. Awesu Awesu
  4. Yusuph Kagoma
  5. Joshua Mutale
  6. Edwin Balua
  7. Fabrice Ngoma
  8. Jean Chalres Ahoua
  9. Kibu Denis

 

Washambuliaji

  1. Steven Mukwala
  2. Leonel Ateba
  3. Valentino Mashaka

 

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.