Simba SC vs TRA United: Robo Fainali CRDB Federation| Ratiba, matokeo, msimamo, utabiri, Livescore, h2h, na Habari za timu

ByJoel Thomas

May 16, 2026
Simba SC vs TRA UnitedSimba SC vs TRA UnitedSimba SC vs TRA United
  • Simba SC vs TRA United ni mechi kali ya Robo Fainali ya mashindano ya CRDB Federation itakayopigwa kesho Jumapili 17/5/2026.
  • Mechi hii inatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge, Dar es Salaam.
  • Mshindi wa mchezo huu anatarajiwa kuvaana na Coastal Union, katika hatua ya Nusu Fainali ya mashindano hayo.
  • Mnyama anaingia katika mchezo huu akiwa na kumbukumbu nzuri baada ya matokeo ya Mashujaa FC 0-3 Simba SC.

Robo Fainali ya 4 ya mashindano ya CRDB Federation kati ya Simba SC vs TRA United, itapigwa kesho Jumapili 17/5/2026. Mechi hii ngumu inatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge, Dar es Salaam kuanzia saa 12:30 jioni. Ikumbukwe mshindi wa mchezo huu anatarajiwa kuvaana na Coastal Union, katika hatua ya Nusu Fainali ya mashindano hayo. Makala hii inakuletea dondoo muhimu za mchezo huo.

Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya CRDB Federation 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.

Je, unataka kushinda mamilioni? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa

Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Aviator game promotional banner featuring a red propeller plane and a jackpot of 800,000,000.

Aviator: Paisha kindege ushinde mpaka zaidi ya 800,000,000.

Simba SC vs TRA United h2h

Simba SC vs TRA United h-h
Simba SC vs TRA United h-2-h

Timu hizi zimekutana katika mechi 6 za ushindani, ambapo Simba SC wameshinda mechi 5, na TRA United wakiwa bado haijaonja ladha ya ushindi. Mechi 1 pekee katika mikutano yao ndiyo iliisha bila kupatikana mbabe. Hivyo hii ni nafasi kwa kila timu kuandika historia mpya. Jedwali hili linaeleza takwimu hizo;

TareheMashindanoTimu ya NyumbaniMatokeoTimu ya Ugenini
9 Aprili 2026Ligi Kuu Tanzania BaraTRA United0 – 0Simba SC
22 Machi 2026Ligi Kuu Tanzania BaraSimba SC3 – 0TRA United
2 Februari 2025Ligi Kuu Tanzania BaraTRA United0 – 3Simba SC
18 Agosti 2024Ligi Kuu Tanzania BaraSimba SC3 – 0TRA United
6 Mei 2024Ligi Kuu Tanzania BaraSimba SC2 – 0TRA United
6 Februari 2024Ligi Kuu Tanzania BaraTRA United0 – 4Simba SC

SOMA HII PIA: Simba SC 3-0 TRA United highlights, H2H, standings, twakimu | Matokeo ya NBC Premier League

Simba SC, TRA United wanasemaje?

Simba SC

Simba SC vs TRA United
Chama vs Mashujaa FC

Akizungumzia mchezo huo, Meneja Habari na mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema: “Maandalizi ya mchezo wa CRDB Bank Federation Cup kati yetu dhidi ya TRA United yanaendelea, yalianzia Kigoma na yameenda vema. Wachezaji wameandaliwa kisaikolojia zaidi na kimwili, kuhakikisha wanacheza katika ubora utakaowapatia matokeo ya ushindi.

“Tuna kazi mbili ambazo ni ngumu kuzifanya kwa wakati mmoja, baada ya kuichapa Mashujaa FC ili kuliondoa ‘gap’ la alama mbili tulizoachwa na Yanga SC.  Mojawapo ya kazi hizi ni kumuangalia mpinzani wetu akipoteza alama. Point hizo mbili zinashikiliwa na timu bora, na yenye uzoefu wa kukaa kileleni.

“Tunawaita mashabiki kwenye Dimba la KMC kuelekea mchezo wao dhidi ya TRA United, robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB. Malengo yetu ni kushinda ubingwa wa michuano hiyo.

SOMA HII ZAIDI: Simba SC vs TRA United NBC Premier League | H2H, live score, prediction, lineups

TRA United

Christina Mwagala
Christina Mwagala

Naye Msemaji wa timu hiyo, Christina Mwagala amesema: “Lengo letu ni kuendelea hatua inayofuata, tumefanya maandailzi ya kutosha ya mchezo huu wa CRDB Federation Cup. Tunatarajia mchezo utakuwa wa kuvutia na wa ushindani kwa pande zote, lakini tutapambana tunabaki kwenye malengo ya Kwenda hatua inayofuata.

“Kikosi cha TRA United, kimefanya mazoezi jijini Arusha kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba SC utakaopigwa Jumapili Mei 17. Sababu za kuchelewa kuingia Dar es Salaam, hakujawa tatizo kwani tulisafiri kwa anga. Malengo ni kwenda Nusu Fainali.

SOMA HII PIA: Simba SC na kibarua kuikabili TRA United / Steve Barker kavurugwa / H2H, standings

Hitimisho

Yanga SC vs Simba SC mitambo ya magoli
Sele – simba sc

Simba SC vs TRA United ni miongoni mwa mechi zilizotoa ushindani mkubwa msimu huu, hivyo mechi ya kesho Jumapili inatarajiwa kuwa ngumu pia. Timu zote mbili zina wachezaji bora, lakini ni wazi kasi ya Simba SC kwenye michezo kadhaa iliyopita inawaongezea ari. Matokeo ya ushindio kwa TRA yatawapa nafasi ya kujiweka kwenye nafasi nzuri kushiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao.

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.