Kapombe kimataifaKapombe kimataifa

KIMATAIFA wawakilishi wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika Simba kete ya kwanza walivuja jasho dakika 90 mbele ya Waarabu Ali Ahli Tripoli kwa kila timu kusaka ushindi ili kukata tiketi ya kutinga hatua ya makundi mwisho hakuna mbabe kati yao lakini wameweka wazi kuwa hawajakata tamaa kazi inaendelea.

Septemba 14 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Al Ahli Tripoli 0-0 Simba. Mpango mkubwa wa Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids ulikuwa kwenye kujilinda huku akifanya mashambulizi ya kushtukiza akimtumia mshambuliaji wake Leonel Ateba ambaye alianza kikosi cha kwanza.

Fadlu ameweka wazi kuwa kazi kubwa inahitajika kupata matokoe chanya kwenye mchezo ujao kutokana na aina ya wapinzan ambao wamekutana nao uwanjani kuwa na shauku ya kupata matokeo ndani ya uwanja huku wakiwa na ari kubwa kusaka ushindi.

HUYU HAPA FADLU

FADLU
KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, 2024/25. Source: Simba.

“Ulikuwa ni mchezo mgumu wenye ushindani mkubwa tumeona.Wachezaji wamejituma katika kutafuta matokeo mbele ya wapinzani wetu lakini mwisho hatujafanikiwa kushinda kwenye mchezo wetu muhimu. Kumekuwa na ugumu katika utengenezaji wa nafasi.

“Katika mchezo wetu hatukupata kutengeneza nafasi nyingi ambazo zinekuwa na faida kwetu na zile chache ambazo tulizitengeneza kwenye mchezo huo hatukuzitumia hivyo ni muda kwenda kufanyia kazi makosa ili kuwa bora kwa mchezo ujao.”

KAPOMBE SHOMARI HUYU HAPA

Shomari Kapombe
SHOMARI Kapombe beki wa Simba 2024/25. Source: Simba.

Beki wa kupanda na kushuka ndani ya kikosi cha Simba, Shomari Kapombe ambaye alianza kikosi cha kwanza katika mchezo wa kimataifa aliweka wazi kuwa walikuwa wanahitaji ushindi lakini hawajapata matokeo hayo hivyo wanajipanga kufanya vizuri mchezo ujao.

“Tulifuata maelekezo ya benchi la ufundi kwenye mchezo wetu kwa kuwa tulikuwa ugenini hivyo tulipewa mbinu ambazo tulizitumia na kuzifuata kwa umakini mwisho hatujapata ushindi.

“Kikubwa tunamshukuru Mungu tumemaliza mechi salama tunarudi kujiandaa kwa mchezo wetu wa marudio ambao tunaamini kwamba tutapata matokeo mazuri tukiwa nyumbani, inawezekana mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi.”

UKUTA ULIPIGA KAZI KWELIKWELI

Katika mchezo huo ukuta wa Simba chini ya Che Malone ulipiga kazi kwelikweli nah ii ilitokana na kushambuliwa mara kwa mara katika mchezo huo na kiongozi wao alikuwa ni Che Malone.

Miongoni mwa hatari ambazo aliokoa Che Malone aliyekuwa akipambana na Mabululu mshambuliaji wa Al Ahli Tripoli ilikuwa dakika ya 52, 54, 57, 58, 62, 74. Dakika ya 74 Che Malone aliokoa akiwa ndani ya 18 alionekana kumchezea faulo mchezaji wa timu pinzani jambo lililowafanya wachezaji wa Al Ahli Tripoli kuonekana kulalamika wakihitaji kupewa penalti lakini mwamuzi hakufanya hivyo aliamua iwe kona.

MUSSA CAMARA KIPA WA KAZI

MUSSA
MUSSA Camara kipa wa Simba aliyeanza dhidi ya Al Ahli Tripoli Septemba 15 2024. Source: Simba.

Mikono ya kipa Mussa Camara ilikuwa ya dhahabu kuzuia mapigo ya Mabululu ambaye alikuwa kwenye shauku kubwa ya kufunga ili kuipa ushindi timu yake kwenye mchezo huo wa kimataifa.

Umakini aliofanya Camara kwenye kutimiza majukumu yake akishirikiana na mabeki wengine ikiwa ni Shomari Kapombe, Mohamed Hussein Zimbwe Jr ulifanikisha lango kuwa salama ugenini kimataifa ndani ya dakika 90.

Edwin Balua kiungo wa Simba mchezo haukuwa upande wake kwa kuwa hakuwa katika ubora kama ilivyokuwa kwa Joshua Mutale ambaye hakuyeyusha dakika 90 kwenye mchezo huo kama ilivyokuwa kwa Balua mkali kwenye mapigo huru.

KIKOSI CHA KWANZA KWA FADLU KIMATAIFA

FADLU
KOCHA Mkuu wa Simba Fadlu Davids akiwa na Fernadez aliyeanza naye kwenye mchezo wa kimataifa 2024/25. Source: Simba.

Fadlu kikosi chake alichoanza nacho kwenye anga la kimataifa ikiwa ni mchezo wake wa kwanza kuongoza ndani ya Simba alianza na :-Mussa Camara, Shomari Kapombe, Mohamed Hussen, Hamza, Che Malone, Kagoma Yusuph, Edwin Balua, Deborah Fernades, Leonel Ateba, Jean Ahoua na Joshua Mutale.

WACHEZAJI WA AKIBA

Ally Salim, Kelvin Kijili, Chamou, Ngoma Fabrice, Okejapha, Kibu Dennis, Awesu Awesu, Steven Mukwala na Valentino Mashaka.

SEMAJI KICHEKO

AHMED Ally
AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari Simba. Source: Simba.

Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally licha ya timu hiyo kukosa ushindi ameweka wazi kuwa matokeo hayo ni mazuri vibaya mno ugenini hivyo watafanya kazi kubwa kwenye mchezo wa marudio Uwanja wa Mkapa kupata ushindi ndani ya dakika 90.

“Haya matokeo ambayo tumeyapata ni matokeo mazuri vibaya mno na kwenye mchezo wetu tutakaocheza nao Uwanja wa Mkapa Septemba 22 matokeo yataamuliwa hapo.”

 

Share this: