YANGA, SIMBA JINO KWA JINO ISHU YA ‘SOLD OUT’ 2024/25

ByJoel Thomas

August 2, 2024
HALI YA MAUZO YA TIKETIHALI YA MAUZO YA TIKETIHALI YA MAUZO YA TIKETI
YANGA
HALI YA MAUZO YA TIKETI

VITA ya kuonyeshana ukubwa kati ya Simba na Yanga msimu huu unaweza kusema ni jino kwa jino ambapo mara baada ya uongozi wa Simba kutangaza ‘Sold out’ ya manunuzi ya tiketi za tukio lao la Simba Day inayobebwa na kauli ya ‘UBAYA UBWELA’, Yanga nao muda wote watatangaza ‘Sold out’

Simba Jumamosi hii wanatarajia kufanya tukio kubwa la SIimba Day ambalo litafanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ambapo kuelekea tukio hilo Simba wametangaza kumaliza tiketi zote za watakaohudhuria tukio hilo.

Matukio makubwa yanatarajiwa kufanyika katika tukio hilo ikiweko burudani ya muziki, utambulisho wa kikosi cha Simba kwa msimu wa 2024/25 na tukio la mchezo mkubwa wa kirafiki kati bya Simba na APR ya Rwanda.

Kama sehemu ya matukio yao ya hamasa kuelekea tukio lka Simba Day, Simba msimu huu walifanya uzinduzi wa jezi zao katika hifadhi ya Wanyamapori ya Mikumi mkoani Morogoro ambapo jezi hizo zimekuja katika rangi tatu ambazo ni bluu, nyeupe na nyekundu.

Katika jezi hizo jezi ya rangi nyekundu inatarajiwa kuwa jezo ya nyumbani, jezi ya rangi nyeupe itakuwa jezi ya ugenini na jezi ya bluu ikiwa ni jezi ya tatu ‘third kit’.

Baada ya uzinduzi huo, watani zao Yanga nao wakafanya tukio kubwa la uzinduzi wa jezi zao mpya kwa ajili ya msimu ujao ambao pia ulifuatiwa na hamasa ambayo imefanyika katika maeneo mbalimbali.

YANGA KUVAANA NA RED ARROWS YA ZAMBIA

Klabu ya Yanga kupitia kwa Msemaji wake, Haji Manara imetangaza kuwa katika kilele cha wiki ya mwananchi wanatarajia kucheza dhidi ya Mabingwa wa Michuano ya CECAFA Dar Port KAGAME Cup kutokea Zambia, Red Arrows kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Niwape habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni kuwa, Mshindi wa Kagame Cup Red Arrows ndio tutakaocheza nao kwenye mchezo wa siku ya Mwananchi Pale Benjamini Mkapa. Wote mnafahamu ukubwa wa Red Arrows ya Zambia, wamesema watakuja na Ndege yao ya kijeshi kama ilivyo kawaida yao.” Amesema Haji Manara.

JUMAMOSI NI ‘SUPU DAY’ TENA

YANGA
Sabrina Msuya -TzSportPesa

Kuelekea maadhimisho ya kilele cha wiki ya Mwananchi siku ya Jumapili ya Agosti 4, mwaka huu, uongozi wa Yanga kwa kushirikiana na Kampuni ya SportPesa ambao ni wadhamini wao wakuu wametangaza tukio kubwa la Supu day siku ya Jumamosi ya Agosti 3, mwaka huu.

Yanga Jumapili hii wanatarajiwa kuwa na tukio kubwa la kilele cha wiki ya Mwananchi ambapo kupitia tukio hilo wanatarajia kutangaza rasmi kikosi chao kwa msimu ujao ambapo pia kunatarajiwa kuwa na burudani mbalimbali pamoja na kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki ambapo kwa mwaka huu wanatarajia kuvaana na Red Arrows.

Mkurugenzi wa Mahusiano wa TZ SportPesa, Sabrina Msuya amesema “Sisi kama wadhamini wakuu tutakuwa pamoja kwenye supu day siku ya Jumamosi, Kampuni ya SportPesa imeandaa supu kwa wananchi wakiwa wanajiandaa kupata burudani kwenye kilele cha wiki ya Mwananchi.”

Naye Meneja Masoko wa TZ Sportpesa, Tracy Humplick amesema “Tumeandaa Kampeni maalumu kwa mashabiki wote wa Yanga Sc, tutakuwa tunagawa jezi mpya za msimu huu kama zawadi kwa mashabiki wa Yanga Sc kuelekea kilele cha wiki ya Mwananchi”

SOLD OUT KAMA ZOTE, WADHAMINI WATANGAZWA

YANGA
HALI YA MAUZO YA TIKETI

Kama ilivyo kwa watani zao wa jadi Simba, msimu huu Yanga wamekuwa na mwamko mkubwa wa kununua tiketi ambapo mpaka sasa sehemu kubwa ya tiketi za kuingia uwanjani zimeisha na sasa muda wowote tunaweza tukatangaziwa kuisha kwa tiketi.

Uongozi wa timu hiyo tayari umewaweka wazi wadhamini wao wa tukio hilo ambapo kupitia kwa Mkurugenzi wa Sheria wa timu hiyo, Simon Patrick amesema “Tunawatangazia kuelekea kilele cha wiki ya Mwananchi, ambapo mdhamini mkuu wa wiki ya mwananchi ataendelea kuwa benki ya CRDB, lakini pia tumeongeza tumeongeza washirika wengine ambao ni Benki ya Equity pamoja na GSM Beverage.

“Tunashukuru sana Uongozi wa GSM Group kwa kutambua umuhimu wa kuongeza nguvu ya udhamini kwa klabu yetu, Kampuni hii ya vinywaji visivyo na kileo kama juisi, soda na maji itakuwa sehemu ya wadhamini wetu kwa kipindi hicho cha miaka mitano.”

KIKOSI CHAREJEA KUTOKA AFRIKA KUSINI

Kikosi cha Yanga Jumanne hii wamerejea rasmi Tanzania kutokea Afrika Kusini ambapo walikuwa kwenye ziara fupi ya maandalizi ya kabla ya msimu yaani pre-season ambapo wakiwa huko walicheza michezo mitatu wakishinda mechi mbili na kupoteza mchezo mmoja.

Yanga pia wamefanikiwa kurejea nchini wakiwa  na ubingwa wa Kombe la Toyota ambalo walilitwaa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kaizer Chiefs.

 

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.