MashakaMashaka

KITAUMANA Uwanja wa Mkapa kwenye Simba Day, Agosti 3 2024 katika tamasha linalosubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki duniani. Ikumbukwe kwamba kambi ya Mnyama ilikuwa nchini Misri ambapo huko walicheza mechi tatu za kirafiki.

Ni ushindi walipata kwenye mechi zote tatu jambo ambalo limempa furaha Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids ambaye ameweka wazi kuwa kila mchezaji anaonyesha uwezo wake uwanjani.

Ligi Kuu Bara inatarajiwa kuanza Agosti 16 2024 ambapo mabingwa watetezi wa taji hilo ni Yanga inayodhaminiwa na SportPesa. Yanga wao tamasha lao ni Agosti 4 2024 Uwanja wa Mkapa.

KITAUMANA KWA MKAPA DAKIKA 90

Mutale
KITAUMANA kwa Mkapa Agosti 3 2024 Simba Day. Source :Mutale

Kitaumana kwa Mkapa kwenye dakika 90 za kusaka ushindi kwenye mchezo wa kirafiki ambapo Simba inatarajiwa kucheza mchezo dhidi ya APR ya Rwanda. Huo ni mwanzo kuelekea msimu mpya wa 2024/25.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa maandalizi yapo vizuri na tiketi zinazidi kununuliwa kwa mashabiki ambao wanaendelea kununua pamoja na uzi mpya.

“Maandalizi kuelekea Simba Day ni makubwa huku kila mmoja akiwa tayari kwa ajili ya kushuhudia tamasha kubwa duniani na hili linaingia kwenye matamasha makubwa hivyo mashabiki mjitokeze kwa wingi.

“Kuna wachezaji wa mpira ambao wapo na wote wanafanya kazi kubwa uwanjani hasa kwenye eneo la mazoezi ilikuwa ni furaha kubwa vibaya mno na wakati ni sasa kuelekea kwenye mechi zijazo.”

HAKUNA MCHEZAJI MWENYE JINA

Mashabiki Simba
Mashabiki Simba kuelekea Simba Day Agosti 3 2024.Source: Simba.

Ipo wazi kwamba katika usajili Simba haijatikisa kwenye anga la Bongo kutokana na kuwa na wachezaji wenye majina ya kawaida tofauti na watani zao wa jadi Yanga ambao wamesajili wachezaji walioshtua na kuzua gumzo. Miongoni mwa wachezaji hao ni Mashaka Valentino, Israel Mwenda, Awesu Awesu.

Miongoni mwa wachezaji ambao walileta gumzo ndani ya Yanga ni Clatous Chama ambaye alikuwa ndani ya Simba msimu wa 2023/24 alifunga mabao 7 na pasi sita za mabao kibindoni.

Julai Mosi 2024 Chama alitambulishwa Yanga na amekabidhiwa jezi namba 17 ambayo alikuwa anaitumia akiwa Simba. Prince Dube anaingia kwenye orodha ya wachezaji walioleta gumzo na ameanza kazi kwa kuwa kwenye mechi za kimataifa za kirafiki alifunga.

MUTALE KAWAKA HUKO

Mutale
Mutale ingizo jipya ndani ya Simba kuelekea msimu wa 2024/25. Source: Simba.

Ingizo jipya ambalo linatajwa kufanya vizuri kwenye maandalizi kuelekea msimu mpya wa 2024/25 ni Mutale Joshua huyu anatajwa kuwa moja ya mchezaji ambaye amefanya vizuri katika maandalizi kambini Misri akiwa ni moja ya wanaopewa nafasi kufanya vizuri.

Ally ameweka wazi kuwa mchezaji huyo ana uwezo mkubwa na atafanya kazi kubwa kwa kushirikiana na wachezaji wengine kupata matokeo kwenye mechi za ushindani.

“Kila kitu kinakwenda sawa Mutale ni mchezaji wa mpira anakuja kuendeleza burudani, mashabiki wajitokeze kwa wingi ndani ya Simba Day ni burudani kubwa ambayo inatarajiwa kuwa na mvuto vibaya mno.”

KITAUMANA KWA KIBU

Kibu D
Kibu Dennis kiungo mshambuliaji wa Simba. Source: Simba.

Kibu Dennis kiungo mshambuliaji wa Simba bado sakata lake halijagota mwisho akitajwa kuwa kwenye hesabu za Yanga inayohitaji kuinasa saini yake. Ipo wazi kwamba Kibu ni mali ya Simba aliongeza mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba hivyo yupo hapo mpaka 2026 kwa mujibu wa Simba.

2021/22 unaingia kwenye orodha ya msimu bora kwa Kibu akiwa na uzi wa Simba alifunga mabao 8 na pasi nne za mabao baada ya kucheza mechi 21 akikomba dakika 1,607. Mara ya mwisho kuonekana uwanjani akiwa na uzi wa Simba ilikuwa Aprili 30 2024 Namungo 2-2 Simba. Kwenye mchezo huo alipata maumivu hivyo alikwama kuendelea kwenye mechi za mwisho za msimu.

JEMBE AMEMCHAMBUA MUTALE

Legend Saleh Ally, Jembe mwandishi mkongwe kwenye masuala ya habari za michezo kitaifa na kimataifa ameweka wazi kuwa Mutale ana kitu kutokana na uwezo wake uwanjani kwenye mechi za kirafiki.

Jembe alikuwa Misri kwenye kambi ya Simba alipata muda wa kutazama mazoezi na mechi ya kirafiki ya Simba ikiwa huko na tayari kambi imekamilika hivyo wanarejea Tanzania.

Jembe ameandika namna hii: “Kisukuma Mutale, maana yake ni mkubwa, ila unatakiwa kuivuta kidogo Mutaale. Huyu Mutale wa Simba kiumbo si mkubwa lakini mambo yake ni makubwa na atakuwa gumzo ninaamini.

“Kasi…nguvu…si mwoga na ana uwezo wa kuwatambuka hata walinzi watatu lakini hatari zaidi anapiga mashuti mfano bao la pili la Simba dhidi ya Wasaudi, alipokea mpira pembeni, akatembea kwa kasi na kupiga shuti kali sana likagonga mwamba na kurudi ndani.

“Wakati walinzi wanajishauri kwa kasi yake alishafika na kupiga shuti tena. Anyway ni mchezaji ambaye inaweza kuwa moja ya karata walizopata Simba na itachangia warejee.” Mchezo huo ulichezwa Julai 29 2024 Simba ilipata ushindi wa mabao 2-1 Al-Adalah FC ya nchini Saudi Arabia.

 

Share this: