TUZO 2023/24 ILIKUWA, YANGA WAPETA, SIMBA NGOMA NZITO

ByLunyamadizo Mlyuka

August 2, 2024
Zimbwe TuzoZimbwe TuzoZimbwe Tuzo

.
TUZO za Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2023/24 zimetolewa kwa washindi na kila kitu kimekuwa wazi baada ya mpango kazi kukamilika kwenye ukumbi wa Dome Masaki huku Yanga inayodhaminiwa na SportPesa ikifanya vizuri kila kona kutokana na kutwaa tuzo nyingi.

Hapa tunakuletea orodha ya waliotwaa tuzo kwa msimu wa 2023/24 pamoja na washindani wao namna ilivyokuwa huku Aziz Ki akiwa nyota aliyekomba tuzo nyingi kwa upande wa wachezaji wa Ligi Kuu Bara.

TUZO YA KIKOSI BORA MSIMU WA 2023/24

Tuzo ya Kikosi bora
TUZO ya kikosi bora cha Ligi Kuu Bara 2023/24. Source: Yanga.

Ley Matampi wa Coastal Union kinara wa cleen sheet, (Hati Safi) 15 baada ya kucheza mechi 24 za ligi.

Yao Kouassi wa Yanga mechi 22 za ligi alicheza akikomba dakika 1,826 alitupia bao moja.

Mohamed Hussen Zimbwe Jr  wa Simba mechi 27 dakika 2,322 pasi za mabao 6.

Ibrahim Hamad wa Yanga Yanga mechi 21 dakika 1,788.

Dickson Job wa Yanga mechi 25 dakika 2,264 alitupia bao moja.

Mudathir Yahya wa Yanga mechi 25 dakika 1,730 alitupia mabao 9 asisti 2.

Kipre Junior wa Azam FC FC alitoa jumla ya pasi 9 za mabao na alitupia mabao 10

Maxi Nzengeli wa Yanga  mechi 28 dakika 2,186 mabao 11 asisti 2.

Wazir Junior wa KMC kinara wa utupiaji kwa upande wa washambuliaji mabao 12.

Feisal Salum wa Azam FC  mabao  19 pasi 7 za mabao dakika 2,442 mechi 29.

Aziz Ki wa Yanga mechi 26 pasi za mabao 8 mabao 21 dakika 2,084.

Aucho, mechi 19 dakika 1,569 asisti 2

 

WASHINDI WA TUZO

KIUNGO BORA

Aziz Ki
TUZO ya Aziz Ki 2023/24. Source: Yanga.

Mchezaji wa Yanga Sc, Stephane Aziz Ki ameshinda tuzo ya Kiungo Bora na Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/24 katika tuzo zilizotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Ki amewashinda wanzake wawili alioingia nao fainali kuwania tuzo hiyo ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa hasa kwake na mastaa wa Azam FC iliyogotea nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 na itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika wachezaji hao ni:-

  1. Feisal Salum wa Azam FC
    2. Kipre Junior wa Azam FC

TUZO YA KIPA BORA

Kwenye upande wa tuzo ya kipa bora ni Ley Matampi mlinda mlango namba moja wa Coastal Union ya Tanga ametwaa tuzo msimu wa 2023/24. Matampi alikuwa kwenye ubora wake akimshinda kwa ukaribu kipa bora wa msimu uliopita ambaye ni Diarra.

Mshindani wake mwingine alikuwa ni kipa namba moja wa Simba, Ayoub Lakred raia wa Morocco ambaye alikuwa katika ubora ndani ya Simba ambayo iliweka kambi nchini Misri.

TUZO YA BEKI BORA

BACCA
TUZO ya beki bora 2023/24 mikononi mwa Bacca. Source: Yanga.

Kwenye kipengele cha beki bora alitangazwa mwamba Ibrahim Hamad ‘Bacca’ mali ya Yanga ameshinda tuzo ya beki bora kutokana na kuwa kwenye mwendo mzuri na chaguo la kwanza la Kocha Mkuu Miguel Gamondi.

Kipengele hicho waliongia fainali walikuwa watatu na orodha ilikuwa namna hii:-

1.Yao Kouassi wa Yanga
2. Ibrahim Bacca wa Yanga
3. Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr.’ wa Simba

TUZO YA KOCHA BORA

Mbwana Sammatta
Mbwana Samatta ana tuzo yake ya mchezaji anayecheza soka la kulipwa nje. Source: Samatta.

Kwenye upande wa tuzo ya kocha bora ni Miguel Gamondi alitwaa tuzo hiyo kwa msimu wa 2023/24 kutokana na kukiongoza kikosi kilichotwaa ubingwa wa ligi kikiwa na pointi 80 baada ya kucheza jumla ya mechi 30.

Orodha ya waliotajwa kuwania tuzo hiyo ilikuwa namna hii:-

1David Ouma wa Coastal Union timu yake iligotea nafasi nne kwenye msimamo.
2. Bruno Ferry wa Azam FC timu yake iligota nafasi ya pili kwenye msimamo.
3. Miguel Gamondi wa Yanga timu yake iligotea nafasi ya kwanza kwenye msimamo.

MCHEZAJI BORA ANAYECHEZA NJE YA BONGO

Kulikuwa na kipengele cha mchezaji anayecheza soka la kulipwa nje ya Bongo ambayo alitwaa Mbwana Samatta wa Klabu ya PAOK FC ya Ugiriki na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ndiye mchezaji bora wa kiume wa soka la kulipwa msimu wa 2023/24.

HAT TRICK YA TUZO KWA KI

Aziz Ki amepiga hat trick tuzo za Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/24 kabatini akisepa na tuzo nne mazima.

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Aziz Ki ametwaa tuzo tatu kwa mpigo ikiwa ni Hat Trick kwake msimu wa 2023/24 ilikuwa ni mchezaji bora Ligi Kuu ya NBC, mfungaji bora na kiungo bora. Ipo wazi kuwa ni mabao 21 alifunga kiungo huyo chaguo la kwanza la Gamondi ambaye yumo kwenye kikosi bora cha msimu.

TUZO YA MVP

Aziz Ki
Aziz Ki wa Yanga na tuzo yake msimu wa 2023/24. Source:Yanga

Kiungo wa Yanga Stephane Aziz Ki ni mchezaji bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/24.

Orodha ya nyota aliokuwa akiwania nao tuzo hiyo hii hapa:-

1.Feisal Salum wa Azam FC alitupia mabao 19 ndani ya ligi.
2.Kipre Jr wa Azam FC alitoa jumla ya pasi 9 za mabao na alitupia mabao 10.
3. Djigui Diarra wa Yanga kipa namba moja wa Yanga alicheza mechi 23 alikomba dakika 1,935 cleen sheet 14 alifungwa mabao 10.
4. Ley Matampi wa Coastal Union kinara wa cleen sheet 15 baada ya kucheza mechi 24 za ligi.
5. Yao Kouassi wa Yanga mechi 22 za ligi alicheza akikomba dakika 1,826 alitupia bao moja.
6. Ibrahim Bacca wa Yanga mechi 21 dakika 1,788.
7. Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr wa Simba mechi 27 dakika 2,322 pasi za mabao 6.

TUZO YA MVP CRDB FEDERATION

Kiungo wa Azam FC, Feisal Salum  maarufu kama Fei Toto ametwaa tuzo ya mchezaji wa Kombe la Shirikisho la CRDB msimu wa 2023/24. Ikumbukwe kwamba taji hilo lipo mikononi mwa Yanga.

 

Share this: