skip to Main Content
Mkazi Moshi Alamba Sh. 6,069,063 Jackpot Bonus Ya SportPesa
Maduhu-Bonus-Winner-

Mkazi Moshi alamba Sh. 6,069,063 Jackpot Bonus ya SportPesa

Unaweza kusema Peter James Maduhu ni mmoja wa watanzania wenye bahati ya mtende. Akiwa anajiandaa na msimu wa sikukuu Peter alimua kucheza Jackpot ya kati kati ya wiki ya SportPesa na kujishindia Jackpot bonus ya Sh 6,069,063, baada ya kupatia kwa usahihi mechi 12 kati ya 13.

Akizungumza katika ofisi za SportPesa baada ya uhakiki na makabidhiano ya mfano wa hundi ya ushindi wake Peter anasema alianza kucheza na SportPesa kuanzia Mwaka 2020, wakati huo akiwa Morogoro.

‘’Mimi nilianza kucheza na SportPesa 2020, wakati huo nilikuwa nimetoka Moshi na kwenda Morogoro kufanya biashara ya nafaka ambako nilikuwa na fremu yangu pale Morogoro mjini.

Siku mmoja nikiwa pale nje ya duka langu, kulikuwa na vijana wengi ambao walikuwa wanaweka ubashiri na SportPesa wakaniambia, Peter vipi mbona umekaa bila kutafuta hela ya ziada, wakati sisi tunapiga hela kwenye simu.

Kwa kweli sikuwaelewa, lakini kadiri nilivyokuwa ninakutana nao siku nyingine walikuwa wanashinda hivyo nilikuwa nawaona. Baada ya kama wiki mbili nilianza kuwasumbua wanifundishe na walikubali na kunifundisha’’. Anasema Peter.

Anaendelea kwa kusema tangu ameanza kucheza na SportPesa amewahi kushinda kuanzia 140,000, 30,000, 50,000 na viwango vingine vya kawaida ambavyo alikuwa anashinda kupitia mechi za multibet.

Jackpot bonus message‘’Najiona ni mtu mwenye bahati kidogo, naweza kusema Mungu ni mwema kwa kuwa tangu nimeanza kucheza au kujua kubashiri nimekuwa napata japo kidogo.

Kama nilivyoshinda hii Jackpot bonus ya katikati ya wiki, siku za nyuma nilikuwa nashinda kupitia mechi nyingi ninazocheza’’.

Peter anasema mkeka wake ulioshinda hii Jackpot bonus ya SportPesa ya kati kati ya wiki aliuweka kuanzia Jumatatu, Jumanne na Jumatano ya wiki iliyopita.

Kwa kifupi Peter hutumia muda wa chakula cha mchana akiwa kazini kuchambua na kuweka mikeka.

‘’Huwa nikipata nafasi majira ya mchana, muda wa kula najaribu kuweka mkeka mmoja ama miwili. Sasa kwa mkeka huu nilioshinda niliweka mikeka mitatu, lakini huu mmoja ndio uliobahatika’’.

Baada ya kuweka mkeka wake ulioshinda Peter anasema alilianza kufuatilia matokeo kwa simu yake janja.

Aanaelezea kwa kusema siku ya kwanza mkeka wake ulitoa timu nane. Siku hiyo anakumbuka ilikuwa Jumatano iliyopita.

‘’Naweza nikasema mkeka huu pamoja na kuushinda umenitesa kidogo. Siku ya Alhamisi kulikuwa na mechi za usiku sana kwani kulikuwa na timu za kule Brazil. Nilibahatika kupatia mechi 2. Hapo nilichanganyikiwa kwani kesho yake nikapata timu mbili tena na kufikisha timu 12.

Wakati nimetulia nafikiria nifanye nini, sms ya hongera kutoka SportPesa iliingia. Baada ya ile sms nilijaribu kutaka kuhamisha pesa nikashindwa.

Hapo nilichanganyikiwa kidogo. Hali ilikuwa mbaya zaidi kwani siku za nyuma nilikuwaga na namba ya SportPesa ya huduma kwa wateja nikaitafuta, lakini sikufanikiwa kuiona.

Baada ya muda kupita, nilikumbuka kwamba SportPesa wanaweka matangazo, pamoja na mechi za Jackpot kwenye magazeti. Nilisubiri mpaka kupambazuke asubuhi, na kwenda kununua gazeti, na kupata namba za kitengo cha huduma kwa wateja’’. Alisema Peter

Niliwasiliana nao wakaniambia ni kweli nimeshinda na itabidi nije Dar-Es-Salaam kwa ajili ya uhakiki ili akaunti yangu iendelee kutumika.

Nilisubiri mpaka Pasaka imeisaha na nimefunga safari kutoka Moshi na kuja kwa ajili ya uhakiki ambao tayari nimeshafanya na kukabidhiwa mfano wa hundi ya ushindi wangu.

Jackpot bonus WinnerAnamalizia kwa kuwaasa watanzania kuiamini na kucheza na SportPesa kwani hata yeye mwenyewe hakuwa anaamini mara ya kwanza alipoanza kucheza.

‘’Sina maneno mengi ya kusema zaidi ya kuwaomba watanzania kucheza na SportPesa hasa hasa Jackpot ya kati kati ya wiki na ile ya mwisho wa wiki, kwani bonus zao ni za viwango vya juu sana.

Akimpongeza mshindi kwa niaba ya SportPesa, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Sabrina Msuya alimtaka Peter aendelee kucheza bila kuchoka, kwani kuna siku anaweza kushinda Jackpot ya kati kati ya wiki au ile ya mwisho wa wiki Supa Jackpot na kuwa Bilionea mpya mjini.

‘’Nikupe hongera kwa ushndi huu wa Jackpot bonus ya kati kati ya wiki, na pia nikuase uendelee kucheza kwani huwezi jua una bahati kwa kiasi gani.

Niwaombe watanzania wenzangu ambao kila mara narudia kuwaasa kuendelea na wao kucheza kwani SportPesa hakuna longo longo la malipoa na pesa ipo ya kutosha.

Jackpot yetu ya kati kati ya wiki imesimamia Tsh 544,830,140

Share this:
Back To Top