Clatous Chama ni mchezaji wa kwanza kushinda tuzo 5Chama Clatous
  • Ni Clatous Chama ni mchezaji wa kwanza kushinda tuzo 5 mfululizo NBC Premier League 2025/26
  • Coastal Union 1-2 Simba SC alitoa pasi mbili za magoli na kuchaguliwa kuwa Man of the Match akifikisha tuzo yake ya 5
  • Goli lake alilowafunga Yanga SC lamfikia mchezaji wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand

Kiungo wa Simba SC Clatous Chama ni mchezaji wa kwanza kushinda tuzo 5 mfululizo za Man of the Match.Mwamba wa Lusaka mwenye miaka 34 usajili mpya dirisha dogo amekuwa katika ubora wake. Hii ni rekodi mpya katika historia ya soka la Tanzania ndani ya Ligi Kuu Bara ya NBC. Goli alilofunga dhidi ya Yanga SC limetabiriwa kutwaa tuzo ya goli bora na mchezaji wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand. Mchezo uliopita ubao wa Uwanja wa Mkwakwani ulisoma Coastal Union 1-2 Simba SC, alitwaa tuzo yake ya 5 mfululizo.

Je, unataka kushinda mamilioni? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa

Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

SOMA HII: Usajili mpya Simba SC balaa: Clatous Chama, Sopu, Mpanzu watikisa tena

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

Mwamba Clatous Chama ni mchezaji wa kwanza kushinda tuzo 5 NBC Premier League 2025/26

Clatous Chama ni mchezaji wa kwanza kushinda tuzo 5
Chama vs Diarra

SOMA HII: Clatous Chama usajili wake umelipa | Takwimu na timu alizocheza CAF Champions League

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

Historia imeandikwa kiungo wa Simba SC, Clatous Chama ni mchezaji wa kwanza kushinda tuzo 5 NBC Premier League mfululizo bila kupumzika. Katika mechi 5 za ligi mara baada ya dakika 90 kiungo huyo alitwaa tuzo hiyo baada ya kuchaguliwa na jopo la kamati. Hii ni tuzo maalumu ambayo hutolewa kwenye kila mechi kwa lengo la kuongeza wachezaji kujituma uwanjani.

Kwenye mechi za Mei 2025/26 Chama amekuwa katika ubora kila mchezo. Alianza Mei 3, 2026 dhidi ya Yanga SC alipofung goli bora na kutoa pasi Uwanja wa Meja Jeneral Isahmuyo. Katika mchezo huo ubao ulisoma Simba SC 2-2 Yanga SC, wawili hawa waligawana pointi mojamoja.

Orodha ya mechi ambazo alichukua tuzo Chama

TareheMechiUwanjaMagoliAssist
3 Mei 2026Simba SC 2-2 Yanga SCMeja Jeneral Isahmuyo11
6 Mei 2026Simba SC 1-0 JKT TanzaniaMeja Jeneral Isahmuyo10
10 Mei 2026Simba SC 4-0 Tanzania PrisonsKMC Complex10
14 Mei 2026Mashujaa FC 0-3 Simba SCLake Tanganyika20
21 Mei 2026Coastal Union 1-2 Simba SCMkwakwani02

Ahmed Ally maoni yake kuhusu Clatous Chama

Clatous Chama ni mchezaji wa kwanza kushinda tuzo 5
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari Simba SC.

SOMA HII: Clatous Chama aongeza presha Yanga SC | Takwimu, mechi | SportPesa Blog

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa Chama ni mchezaji anayeendeleza ubora kila wakati. Kwenye mechi tano mchezaji huyoametwaa tuzo jambo ambalo sio jepesi. Aliongeza kuwa anawachanganya kila siku.

“Clatous Chota Chama ni mchezaji anayeonyesha ukubwa na ubora kwenye mechi zote. Unaona katika mechi tano mfululizo amekuwa bora. Sio jambo jepesi mchezaji kutwaa tuzo mechi 5 mfululizo huu ni ubora na mwendelezo kwa kila mechi,”.

Rio Ferdinand maoni yake kuhusu goli la Chama

Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Rio Gavin Ferdinand mwenye miaka 47 amelitaja goli la Chama kuwa na hadhi ya kutwaa tuzo ya goli bora. Beki huyo alikuwa Tanzania kwa wito maalumu na Wizara ya Habari na Michezo. Kwenye mahojiano na mtangazaji wa Clouds Media, Meena Ally alitaja goli hilo kuwa bora.

“Ninaona hili ni goli bora kwenye ligi kutokana na namna mfungaji alivyofunga. Kwa maoni yangu linastahili kuwa goli bora la msimu. Limefungwa kwa ustadi na linafurahisha,” alisema Rio.

Msikie Chama Clatous mwenyewe

Kiungo Chama ambaye amefunga magoli 8 kwenye ligi amesema bado kuna kazi kubwa itaendelea kufanyika kwa mechi zijazo. Chama amesema tuzo hizo ni kwa ajili ya mashabiki. Aliongeza kwa kuwaomba kushirikiana kila wakati.

“Kikubwa ni ushirikiano kutoka kwa wachezaji kwenye kila mchezo. Maelekezo kutoka benchi la ufundi na kupenda kuona timu inapata matokeo.Kupewa tuzo sio kitu chepesi kwani kuna wachezaji wengi nao wanafanya vizuri, mashabiki ninawaomba waendelee kuwa nasi kwenye kila mchezo,”.

Hitimisho

Clatous Chama ni mchezaji wa kwanza kushinda tuzo 5 NBC Premier League 2025/26. Je rekodi hiyo itavunjwa na mchezaji gani msimu huu? Endelea kufuatilia Blog ya SportPesa kwa taarifa za hivi punde.

Share this: