Leicester City vs Manchester CityLeicester

Jumamosi hii kwenye dimba la Etihad majira ya saa 1.30 Usiku kwa saa za Afrika Mashariki, Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England Manchester City watakuwa kibaruani kuwakabili Mabingwa wa zamani wa Ligi hiyo Leicester City ikiwa ni muendelezo wa EPL inayoelekea ukingoni.

Manchester City walio katika kiwango bora kabisa hivi sasa wakishika nafasi ya 2 katika msimamo wa Ligi wanajivunia matokeo mazuri ya hivi karibuni wakiwa wameshinda mechi tano mfululizo za EPL na alama zao 67 wanaikabili Leicester City ambayo hali yao ni mbaya kwani wapo katika nafasi ya 19 wakiwa na alama 25 baada ya michezo 30 walizocheza hadi sasa.

Matokeo ya Leicester City yamewalazimu kulifumua benchi la ufundi la kikosi chao baada ya kumtimua kazi Brendan Rodgers ambaye hadi anaondoka aliwaongoza The Foxes kushinda mechi 7 pekee katika michezo 29,sare michezo 4 huku wakipokea vipigo 19 katika EPL,wakiruhusu mabao 52 huku wao wakifunga mabao 20,takwimu ambazo hazikuwa na taswira nzuri kwa timu hiyo.

Kutokana na matokeo hayo, Leicester City wamempa kibarua aliyewahi kuwa Kocha wa Aston Villa, Dean Smith aambaye amepewa Mkataba wa muda mfupi hadi mwisho wa msimu akiwa na jukumu la kuwanusuru kushuka daraja.

Akizungumza mara baada ya kutambulishwa,Dean Smith amesea’’Ni changamoto iliyopo mbele yangu lakini ninaamini kwa idadi ya michezo iliyosalia na uzoefu wangu na washirika wangu bila kusahau ubora wa wachezaji waliopo nafikiri ni jambo ambalo linawezekana’’

Dean Smith ana uzoefu wa michezo 114 aliyofanya kazi katika Klabu za Aston Villa na Norwich City hivyo ni kigezo ambacho kimetumiwa na Leicester kumpa jukumu hilo na kibarua chake cha kwanza ni dhidi ya Manchester City.

Mchezo huo ni mgumu kwa Leicester kwakuwa wanakutana na  Manchester City ambayo haijapoteza katika mechi 13 zilizopita,wakishinda mechi 9 mfululizo huku wakiwa kwenye mbio za kuzisaka alama ambazo zitaendelea kuwafanya waisogelee Arsenal ambao wapo kileleni dhidi yao kwa tofauti ya alama 5.

Takwimu zinaonyesha katika mechi 3 za mwisho walizokutana ,Manchester City wameshinda zote dhidi ya Leicester City huku stori mbaya kwa The Foxes ni kwamba The Citizen katika mechi 9 za mwisho,wameshinda zote na kufunga mabao 31,tafsiri yake safu ya ushambuliaji ya kikosi cha Pep Guardiola ipo katika kiwango bora ikiongozwa na Erling Braut Haaland.

Katika mechi ya mbili za mwisho,Haaland amefunga mabao matatu, na katika Ligi ya mabingwa Ulaya,mshambuliaji huyo alifunga dhidi ya Bayern Munich na kufikisha idadi ya mabao 45 kwenye mashindano yote na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka EPL kufikisha idadi hiyo akiwapiku Mohamed Salah aliyefikisha mabao 44 katika msimu mmoja.

Leicester City vs Manchester CityPep Guardiola anajivunia takwimu za Haaland ambaye tayari ameshafunga mabao 30 katika EPL na amekuwa na kiwango bora ikiwa ndio msimu wake wa kwanza katika Ligi Kuu ya England,hivyo anatumaini kuwa ubora wake utaendelea kuwa sehemu ya chachu ya ushindi katika mechi dhidi ya Leicester City ambayo safu yao ya ulinzi imekuwa dhaifu msimu huu.

Kuelekea mchezo huo Pep amesema’’ninafurahia changamoto na tunapaswa kufanya kazi tutakapoikabili Leicester City,tushinde ili tuweke matumaini kisha tuifunge Arsenal ndipo tutakuwa katika nafasi nzuri ya kushinda mataji matatu msimu huu,EPL,Ligi ya mabingwa na FA,na hiyo ndiyo furaha yangu ikifanikiwa’’.

Ikumbukwe timu ya mwisho kutwaa Treble ni Manchester United mwaka 1999 ilipokuwa ikinolewa na Sir Alex Ferguson hivyo Pep Guardiola anajaribu kufanya hivyo na kuwa timu ya kwanza kutwaa EPL,UCL na FA tangu The Red Devils wafanye hivyo.

Ushindi dhidi ya Leicester utawafanya Man City wafikishe alama 70 wakiwa na idadi sawa ya michezo na Arsenal wenye alama 73,wakati ushindi kwa Leicester utawafanya wafikishe alama 28 na watachupa hadi nafasi ya 17 wakizishusha Everton na Nottinhgam Forest wenye alama 27 na itategemea nao watapata matokeo yapi wikiendi hii.

Niwakumbushe kwamba kwa mara ya mwisho Leicester City kupata ushindi ilikuwa mnamo mwezi februari mwaka huu walipoichapa Tottenham Hotspurs bao 4-1 na baada ya hapo wameendelea kupitia msoto,lakini upande wa pili Manchester City wao katika mechi mbili zilizopita wameshinda huku wakifunga mabao 7.

Leicester City vs Manchester CityNyota wa kuchungwa wa Manchester City ni Haaland mwenye mabao 30, wakifuatiwa na Phil Foden mwenye bao 9 na Juaa Alvarez mwenye bao 7, Jack Grealish ambaye tangu kombe la Dunia amefunga bao 5 na pasi za usaidizi 4 katika EPL naye mfalme wa kutoa pasi za usaidizi ni Kevin de Bruyne ambaye anaongoza kwa kutoa pasi za usaidizi katika Ligi Kuu ya England (17).

Upande wa Leicester City nyota wenye takwimu bora ni Harvey Banner mwenye bao 10, mwenye bao 9, Patson Daka mwenye bao 4 huku nyota bora zaidi ni James Maddison mwenye bao 9 na pasi za mabao 6 katika msimu huu,je kipi kitatokea?

Kama kawaida yetu SportPesa tayari tumekuwekea mechi hii katika tovuti yetu.

Ili kucheza tembelea sportpesa.co.tz, piga *150*87#au download APP sasa!

Share this: