Coastal Union 1-2 Simba SCAnicent Oura
  • Coastal Union 1-2 Simba SC NBC Premier League 2025/26 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga
  • Maabad Maabad alifunga goli la utangulizi kwa Coastal Union dakika ya 9
  • Libasse Gueye alifunga goli dakika ya 37 na Anicent Oura dakika ya 45
  • Kiungo Clatous Chama amechaguliwa kuwa Man of the Match akifikisha tuzo 5 Mei

Coastal Union 1-2 Simba SC ni matokeo rasmi mchezo wa NBC Premier League 2025/26. Wababe hawa wamekutana Mei 21, 2026 kwenye mechi kali. Magoli yamefungwa na Maabad Maulid Maabad dakika 9 kwa Coastal Union. Magoli ya Simba SC yamefungwa na Anicent Oura dakika ya 45 na Libasse Gueye dakika ya 37. Ushindi huo unampeleka mnyama kileleni akifikisha pointi 55 baada ya mechi 24.

SOMA HII: Ratiba ya mechi zilizobakia za Simba SC kwenye NBC Premier League 2025/26 | SportPesa Blog

Aviator game promotional banner featuring a red propeller plane and a jackpot of 800,000,000.

Coastal Union 1-2 Simba SC, Mei 21, 2026

Coastal Union 1-2 Simba SC
Shiza Kichuya na Ellie Mpanzu, NBC Premier League.

SOMA HII: Mapya sakata la Jonathan Sowah amerejeshwa Simba SC na kupelekwa U 20

Aviator game jackpot banner TSh 800 Million prize

Ft: Coastal Union 1-2 Simba SC kwenye mchezo wa mzunguko wa pili. Huu ni ushindi muhimu kwa mnyama akimshusha mtani Yanga SC nafasi ya kwanza. Coastal Union wamefungwa nje ndani ya Simba SC msimu huu, ule wa mzunguko wa kwanza walifungwa magoli 2-1.

Mfungaji wa kwanza Maabad alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 44 ya mchezo wa leo. Coastal Union ni pointi 25 wanasalia nazo wakiwa nafasi ya 12 kwenye msimamo baada ya mechi 24. Je mnyama atasalia kileleni kwa muda gani? Endelea kufuatilia blog ya SportPesa kwa taarifa na matokeo ya hivi punde.

Kiungo wa Simba SC, Clatous Chama amechaguliwa kuwa Man of the Match mara baada ya mchezo. Hii inatokana na mchango wake wa kuhusika katika magoli yote mawili akitoka asisti. Inakuwa ni tuzo ya 5 mfululizo ndani ya Mei, 2026.

H2H Coastal Union vs Simba SC

Coastal Union 1-2 Simba SC
Coastal Union vs Simba SC, NBC Premier League.

SOMA HII: Ligi Kuu Bara 2025/26 ratiba ya mechi kali| Matokeo, msimamo | SportPesa Blog

H2H Coastal Union vs Simba SC tangu 2011-2026 wamekutana mara 26. Kwenye michezo hiyo ushindi kwa Simba SC mechi 18, sare ni 7. Coastal Union imepata ushindi mchezo mmoja pekee.

Rekodi zinambeba mnyama mbele ya wapinzani wao. Mchezo ujao kwa wababe hawa watakutana hatua ya nusu fainali CRDB Federation Cup, Juni 20, 2026. Huu utakuwa ni mchezo wa mtoano Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Hitimisho

Mwisho ubao umesoma Coastal Union 1-2 Simba SC baada ya dakika 90 kukamilika. Mnyama ametoka nyuma ya mchezo na kuondoka na ushindi ugenini. Endelea kufuatilia Blog ya SportPesa kwa taarifa za hivi punde na matokeo.

Share this: