MKAZI DODOMA ASHINDA Tsh 100,000,000 BET SPINNER YA SPORTPESA
Mkazi wa Ihumwe mkoa wa Dodoma Peter Alfred Mbawala ameshinda kitita cha Tsh 100,000,000 kupitia Bet Spinner bonus ya Sportpesa kama nyongeza ya ziada katika ushindi wa mkeka wake wa multibet alioucheza wiki kadhaa zilizopita.
Akizungumza katika ofisi za SportPesa, oysterbay- Dar-es-Salaam, Peter anasema alianza kucheza na Sportpesa miaka mitano iliyopita, akivutiwa zaidi na odds pamoja na bonus za Sportpesa ambazo tangu wakati huo zilikuwa kubwa kuliko za washindani wao.
‘’Mimi nilianza kucheza na SportPesa mwaka 2017. Baada ya kuanza kucheza SportPesa namshukuru mungu nilikuwa na bahati ya kushinda laki moja, mbili mpaka tatu mara kwa mara na kujipa moyo siku moja naweza shinda kiasi kikubwa’’.
Akiongelea namna alivyoshinda Tsh 100,000,000 Peter anasema siku moja kabla ya kushinda hela hiyo, alishinda mkeka ambao aliweka mechi 4, ukampatia laki tatu.
Baada ya hapo alitoa laki mbili na kupeleka kwenye matumizi mengine na kubaki na laki moja ambayo aliweka mkeka uliompa kitita kinono cha nyongeza cha Bet Spinner SportPesa.
‘’Siku iliyofuata niliweka mkeka wa pili ambao niliweka jumla mechi 15 za multibet na kuweka laki moja iliyobaki kwenye akaunti yangu ya SportPesa. Baada ya kuuweka sikuufutilia sana matokeo ya mechi nilizocheza.
Nilikuja kuangalia matokeo ya mechi nilizobashiri jioni ya siku hiyo hiyo na kuona baadhi ya mechi ambazo tayari zilikuwa zimeshashinda.
Peter anaendelea kusema hakujisumbua kuangalia tena mkeka wake mpaka ilipofika usiku majira ya saa nne na nusu ambapo baada ya kufungua simu alikutana na sms iliyomshangaza sana.
‘’Unajua katika mkeka wangu nilitakiwa kushinda Sh 1,400,000, sasa baada ya kupata sms ya ‘’hongera umeshinda’’ ilinionyesha hela nyingi sana. Niliiangalia zile tarakimu mara mbili mbili na kuhisi ile sms imekosea njia kwa bahati mbaya.
Nilijaribu kuhamisha Sh 2,000,000 ikakubali, nikajaribu kutoa tena Sh 3,000,000 ikakubali. Sasa baada ya muda kidogo nikajaribu tena kwa mara ya tatu ikagoma. Nikajua kweli kile kiwango wamekosea. Kumbuka nilikuwa najua mkeka wangu nikishinda napata Mil 1,472,687.
Baada ya muda si mrefu nilipigiwa simu toka SportPesa na mtu aliyejitambulisha ni kutoka kitengo cha huduma kwa wateja akaniambia nimeshinda 100,000,000 kama bonus ama nyongeza kupitia Bet Spinner ambayo kwa wakati ule nilikuwa bado siielewi vizuri.
Alinieleza kwamba akaunti yangu itazuiwa kwa muda inabidi niende ofisini kwao Dar-Es-Salaam kwa ajili ya kujitambulisha na kwa ajili ya uhakiki.
Nilikubali kuja kama unavyoniona japo nilikuwa na woga kidogo.
Anamalizia kwa kusema alipofika SportPesa alipokewa vizuri na walimpa utaratibu wa kujaza fomu na kumuuliza maswali machache ya uhakiki na kuweka fedha zake kupitia benki siku iliyofuata. ‘’Kwa kweli napenda kuwashukuru SportPesa kwa sababu pesa ile ilikuwa kwenye akaunti yangu ya Sportpesa usiku ule ule.
‘’Mimi kama kijana ambaye ninajihusisha na kazi ya usambazaji ama uuzaji wa bidhaa mbali mbali pesa hii nitaitumia kufanya biashara ambazo tayari nazijua kwa kufanya kazi ambayo nimeajiriwa’’.
Napenda kuwashauri vijana wenzangu wasiache kujaribu kama nilivyofanya mimi kwani hujui mungu amekuandikia nini katika fungu lako’’. Alisema Peter
Naye Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa SportPesa Sabrina Msuya alimpongeza Peter kwa fedha liyopata na kuwataka watanzania waendelee kuiamini SportPesa kwani ina bidhaa na huduma ambazo zinaweza kutimiza ndoto zao.
‘’Nachukua nafasi hii kukupongeza na pia nawaasa watanzania kutumia fursa ya jukwaa letu la michezo mbali mbali ya kubashiri na burudani kama hii ya Multibet, Kasino, Jackpot na Supa Jackpot, Virtual, eSports na Lucky numbers ili muweze kushinda kama Peter.
Bet Spinner ni fursa inayopatikana kwa wacheaji wa multibet ama single bet pale wanapokuwa wanaweka mkeka kuna vigurudumu amavyo vinazunguka na kukuongezea nafasi ya kuongeza ama ku dabo ushindi wako.
Kwa mfano kwa huyu Peter alipata fursa ya ushindi wake kuzidishwa mara 100, hivyo ukichukua kiwango alichotakiwa kushinda cha Tsh 1,472,687 na ukazidisha mara 100 utapata hesabu kamili ambayo ni Tsh 147,268,700 na baada ya kodi amebakiwa na Tsh 123,641,830.