- Peter Shalulile atikisa usajili Yanga SC, ndivyo unavyoweza kusema mara baada ya straika huyo kutambulishwa rasmi jangwani.
- Staa huyo wa zamani wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ametua Yanga SC, kwa ada inayokadiriwa kufikia Bilioni 1.8
- Shalulile anasubiriwa kutua rasmi Tanzania ili kuanza kazi na aliyewahi kuwa kocha wake wakiwa na Mamelodi ambaye pia ametambulishwa Yanga SC, Manqoba Mngqithi.
- Shalulile ndiye mfungaji wa muda wote wa Ligi Kuu Afrika Kusini akiwa na zaidi ya mabao 100, Makala hii inakuchambua kwa ufupi takwimu za Peter Shalulile.
Pazia la Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2026/27, linatarajiwa kufunguliwa rasmi Agosti 14 mwaka huu na timu mbalimbali zinaendelea kujiimarisha kwa kufanya usajili mkubwa. Mabingwa watetezi Yanga SC nao wameendelea kutangaza nyota wao wapya ambapo mpaka sasa tayari wamekamilisha usajili na kutambulisha wachezaji 10. Miongoni mwa Sajili zilizotikisa kwenye dirisha hili kubwa la usajili ni Yanga SC kumtambulisha mshambuliaji wa zamani wa Mamelodi Sundowns, Peter Shalulile. Makala hii inachambua kwa ufupi takwimu za Shalulile kwa kuzingatia rekodi za Transfermarket.
Je, bado hujashinda pesa? Cheza aviator ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi zaidi ya Milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Jipatie nafasi ya kujishindia milioni 800 na Aviator
Peter Shallulile atikisa usajili Yanga SC 2026/27

Shalulile amejiunga na Yanga SC, mara baada ya kuachana na Mamelodi Sundowns inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini na mabingwa watetezi wa Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika. Kabla ya kutua Yanga SC Shalulile amewahi kupita kwenye timu za Tura Magic ya Namibia, Highlands Park na Mamelodi za Afrika Kusini. Nyota huyo anaunda listi ya nyota 10 ambao tayari wamekamilisha usajili wao kujiunga na Yanga SC.
KUSOMA ZAIDI KUHUSU USAJILI MPYA YANGA SC 2026/27, SOMA HII: Usajili mpya Yanga SC 2026/27 wachezaji wafanyiwa vipimo |SportPesa Blog
Mafanikio binafsi ya Shalulile na takwimu

Akiwa na jezi ya klabu tatu alizozichezea, Shalulile ameandika rekodi ya kipekee akifanikiwa kufunga mabao 136 katika mechi 313 alizocheza. Shalulile pia ana uwezo mkubwa wa kutengeneza mabao kwa wenzake uwanjani, ambapo rekodi zinaonyesha ametoa asisti 35 katika masiha yake ya soka. Hii inamfanya straika huyo kuwa na uhusika wa jumla ya mabao 271 katika mechi 313.
Taarifa binafsi za mchezaji
Jina : Peter Shalulile
Kuzaliwa: 23/10/1993 (32)
Mahali: Eengolo, Namibia
Urefu: 1,74 m
Uraia: Namibia
Nafasi: Straika wa Kati
Klabu: Yanga SC
KUMJUA STRAIKA MPYA WA YANGA TOURE, SOMA HII: Usajili mpya Yanga SC 2026/27: Cheikh Ibrahima Toure Straika mpya, rekodi zake balaa afunga mabao 105 mechi 243
Makombe

Katika kabati la Staa huyo amefanikiwa kushinda makombe 14, ambapo mataji 5 ni ya Ligi Kuu Afrika Kusini, taji moja la African Football League. Mataji mengine ni MTN X1, Nedbank Cup Winner X1 na Ligi ya Mabingwa Afrika. Hii itamfanya kuwa mchezaji mwenye mafanikio makubwa zaidi kwenye Ligi Kuu ya NBC.
KUHUSU REKODI ZA WINGA MPYA WA YANGA, ALBERT KANGWANDA, SOMA HII: Albert Kangwanda mchezaji mpya wa Yanga SC, takwimu na timu ambazo amecheza | SportPesa Blog
Hitimisho
Ukisema Peter Shalulile atikisa usajili Yanga SC, hautakuwa umekosea kwani utambulisho wa nyota huyo umeandika rekodi ya kufuatiliwa zaidi kati ya Sajili zote zilizofanyika mpaka sasa. Mpaka Makala hii inaandikwa taarifa ya utambulisho wa Shalulile ilikuwa imependwa ‘likes’ na watu zaidi ya 172,000 na kuwa na jumbe ‘comment’ zaidi ya 29,000. Kwa ufupi takwimu za Shalulile zinamtanabaisha kama miongoni mwa nyota hatari. Je, atafanya nini akiwa na Yanga SC? Muda utatoa majibu kamili kwa sasa endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa zaidi.

