
- Cheikh Ibrahima Touré amezaliwa Septemba 22, 1996 anacheza nafasi ya ushambuliaji katika kikosi cha Yanga SC.
- Ni raia wa Senegal anacheza soka la kulipwa Tanzania 2026/27 ni msimu wake wa kwanza.
- Mchezo dhidi ya Kagera Sugar alifunga mabao mawili waliposhinda mabao 4-0 Uwanja wa KMC Complex.
Cheikh Ibrahima Touré ni jina linaloendelea kutajwa sana katika ulimwengu wa soka la Tanzania, hasa kwa mashabiki wa Yanga SC. Mshambuliaji huyu kutoka Senegal amejijengea sifa ya kuwa mfungaji hatari na mchezaji muhimu katika kikosi chake.Hapa tumekuletea wasifu kamili wa Cheikh Ibrahima Touré, tukichambua historia yake ya soka, uwezo wake uwanjani, na takwimu muhimu zinazoonyesha mchango wake tangu alipojiunga na Yanga SC kwa msimu wa 2026/2027.
SOMA HII PIA:Usajili mpya Yanga SC 2026/27: Cheikh Ibrahima Toure Straika mpya, rekodi zake balaa afunga mabao 105 mechi 243
Je, unataka kushinda mamilioni? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.
Cheikh ibrahima Touré ni nani?
Cheikh Ibrahima Touré ni mshambuliaji wa soka mwenye umri wa miaka 30, alizaliwa Kaolack, Senegal mnamo Septemba 22, 1996. Anajulikana kwa uwezo wake wa kutumia miguu yote miwili, nguvu za mwili, kasi, na uwezo mkubwa wa kufumania nyavu akiwa ndani ya eneo la hatari.
Urefu wake unampa faida katika mipira ya juu, huku akionyesha uwezo wa kipekee wa kumalizia mashambulizi. Kabla ya kutua Tanzania, Touré alikuwa akicheza soka la kulipwa katika ligi mbalimbali, ikiwemo Saudi Arabia.Ana uzito wa kg 81.
Historia yake ya soka kabla ya Yanga SC
Kabla ya kujiunga na Yanga SC, Cheikh Ibrahima Touré alikuwa akicheza soka nchini Saudi Arabia. Alimaliza mkataba wake na Klabu ya Al-Jabalain FC, ambapo alionyesha uwezo mkubwa wa kufunga magoli.Katika msimu wa 2025/2026 wa Saudi First Division, Touré alirekodi magoli 19 na kutoa assist 5. Takwimu hizi zilionyesha wazi uwezo wake wa kucheka na nyavu na kusaidia timu yake kupata matokeo, na ndizo zilizovutia vilabu vingi, ikiwemo Yanga SC.
Katika mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar alifunga mabao mawili.Ilikuwa Uwanja wa KMC Complex waliposhinda kwa mabao 4-0.Amekuwa ni mchezaji muhimu kwenye eneo la ushambuliaji.
SOMA HII PIA:Usajili mpya Yanga SC balaa: Ali Kamwe atangaza mashine mbili mpya, namba 6 yatikisa, je ni Feisal?
Mchango wake Yanga SC (msimu wa 2026/2027)
Tangu kujiunga na Yanga SC kwa msimu wa 2026/2027, Cheikh Ibrahima Touré amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika kikosi cha Wananchi. Uwezo wake wa kufunga magoli umekuwa chachu ya mafanikio kwa timu hiyo katika Ligi Kuu Tanzania na mashindano ya kimataifa.
Katika Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League), Touré amecheza mechi 9 na kufunga magoli 3, huku akitoa assist 1. Katika Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League), amecheza mechi 4 na kufunga magoli 2, akionyesha uwezo wake wa kucheza katika viwango vya juu.
Takwimu muhimu za cheikh ibrahima touré (2026/2027)
Hizi hapa ni takwimu za Cheikh Ibrahima Touré kwa msimu wa 2026/2027, zikionyesha mchango wake katika mashindano mbalimbali:
Ligi Kuu Tanzania (NBC Premier League):
Mechi: 9
Magoli: 3
Assist: 1
Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League):
Mechi: 4
Magoli: 2
Takwimu hizi zinaonyesha kuwa Touré ni mchezaji mwenye uwezo wa kuleta tofauti uwanjani, na anaendelea kuwa tegemeo kwa Yanga SC katika harakati zao za kutwaa mataji.
Cheza na ushinde na SportPesa. Kindege!
Mtindo wa uchezaji na uwezo wake
Cheikh Ibrahima Touré ni mshambuliaji wa kati anayependa kucheza kama namba tisa. Uwezo wake wa kushika mpira, kuwalinda mabeki, na kufanya harakati za kuingia kwenye nafasi za kufunga ni muhimu sana kwa timu yake.
Pia ana uwezo wa kupiga mashuti makali kutoka nje ya eneo la hatari na ana akili ya mchezo inayomwezesha kutoa pasi za mwisho kwa wachezaji wenzake. Hali hii inamfanya kuwa mshambuliaji kamili na tishio kwa mabeki wa timu pinzani.
SOMA HII PIA: <a href=”https://www.sportpesa.co.tz/blog/dabi-ya-kariakoo-historia-na-takwimu”>Dabi ya Kariakoo: Historia na Takwimu Muhimu</a>
Hitimisho
Cheikh Ibrahima Touré anaendelea kudhihirisha kuwa yeye ni mmoja wa washambuliaji bora katika Ligi Kuu Tanzania na Afrika. Mchango wake kwa Yanga SC ni mkubwa, na mashabiki wana matumaini makubwa naye katika kuleta mafanikio zaidi kwa klabu yao.
Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa habari zaidi za michezo, uchambuzi, na takwimu za wachezaji unaowapenda.

