- Young Africans Sports Club, maarufu kama Yanga SC, ni moja ya klabu kubwa na zenye mafanikio zaidi nchini Tanzania.
- Klabu hii makao yake makuu yapo Jangwani, Dar es Salaam na mara nyingi hutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa mechi za nyumbani.
- Makala hii inakupa taarifa zote muhimu kuhusu klabu hii, kuanzia Usajili wa Yanga SC, uongozi wake, historia, makombe n.k
Young Africans Sports Club, maarufu kama Yanga SC, ni moja ya klabu kubwa na zenye mafanikio zaidi nchini Tanzania. Klabu hii makao yake makuu yapo Jangwani, Dar es Salaam na mara nyingi hutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa mechi za nyumbani. Klabu hii imejijengea heshima kubwa kupitia mafanikio ya muda mrefu ndani na nje ya nchi.
SOMA HII PIA: Yanga SC imetambulisha wapya 10 dirisha la usajili Ecua afungua Agosti / Walioongeza mikataba/ Usajili
Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Historia ya Yanga SC

Yanga SC ilianzishwa tarehe 11 Februari 1935 na tangu hapo imekuwa ikipeperusha vyema bendera ya soka la Tanzania. Imeshinda mataji 31 ya Ligi Kuu pamoja na makombe mbalimbali ya ndani. Pia imefanikiwa kutwaa Kombe la CECAFA (Maarufu Kagame Cup) mara tano. Kwa viwango vya kimataifa, Yanga SC sasa ni moja ya timu 10 bora barani Afrika.
Kihistoria Yanga SC ilianzishwa na vijana wa Tanzania waliotaka kushiriki katika ligi zilizokuwa zikitawaliwa na timu zisizo za utawala wa kikoloni. Baada ya mwanzo mgumu, kulizuka mgogoro uliosababisha mgawanyiko mwaka 1936. Kundi lililojitenga baadaye liliunda Simba SC, na hapo ndipo ushindani mkubwa kati ya timu hizi mbili ulipoanza. Katika miaka ya karibuni, hasa mwaka 2020, Yanga ilifanya maboresho makubwa ya uendeshaji kwa kuingia ubia na La Liga na kuruhusu uwekezaji binafsi.
Muhtasari wa Klabu
Jina kamili: Young Africans Sports Club (Yanga SC)
Majina ya utani: Wananchi, Vijana Stars
Ilianzishwa: 11 Februari 1935
Uwanja: Benjamin Mkapa Stadium (uwezo wa watu 60,000)
Rais: Eng. Hersi Said
Kocha Mkuu: Pedro Gonçalves
Ligi: Ligi Kuu Tanzania
Msimu wa 2024/25: Mabingwa
SOMA HII ZAIDI: Usajili 2025/26: Yanga SC imetambulisha wachezaji wapya 11 Zimbwe Jr atikisa | Benchi jipya la ufundi
Benchi la ufundi na uongozi

Kocha mkuu ni Pedro Gonçalves akisaidiwa na Filipe Pedro. Timu pia ina wataalamu mbalimbali wakiwemo kocha wa viungo, kocha wa makipa, daktari wa timu na meneja wa timu.
Kwa upande wa uongozi, klabu inaongozwa na Rais Eng. Hersi Said pamoja na viongozi wengine kama makamu wa rais, Afisa Mtendaji mkuu, na wakurugenzi wa idara tofauti.
Kikosi cha msimu wa 2025/26
Kikosi cha Yanga kinajumuisha mchanganyiko wa wachezaji wazawa na wa kimataifa:
Makipa: Djigui Diarra, Abdutwalib Mshery, Hussein Masaranga.
Mabeki: Mohamed Husseini, Dickson Job, Kouassi Attohoula, Chadrack Isaka, Bakari Mwamnyeto na wengine.
Viungo: Pacôme Zouzoua, Mudathir Yahya, Duke Abuya, Damaro, Allan Okello, Kouma, Maxi Nzengeli na wengine.
Washambuliaji: Clement Mzize, Prince Dube, Depu, Buba
SOMA HII PIA: Matokeo ya Yanga SC CAF Champions League 2025/26/ Standings, fixture
Matokeo ya hivi karibuni

Licha ya changamoto kadhaa katika matokeo ya hivi karibuni, Yanga SC kwa ujumla imeonyesha kiwango katika michezo yake mingi. Imepata ushindi mwingi dhidi ya timu mbalimbali na ndio vinara wa Ligi Kuu Bara. Huku pia ikionyesha ukuaji na mapambano ya kweli kwenye mashindano ya kimataifa.
Ratiba ya mechi zijazo za Yanga SC
Baadhi ya mechi muhimu zijazo za Yanga SC ni pamoja na;
Yanga SC vs Tanzania Prisons, Aprili 4,2026
Pamba Jiji FC vs Yanga SC, Aprili 8,2026
Yanga SC vs Mbeya City, Aprili 16,2026
KMC Fc vs Yanga SC, Aprili 16,2026
Yanga SC vs Coastal Union, Aprili 30,2026
Simba SC vs Yanga SC, Mei 3,2026
Dodoma Jiji FC vs Yanga SC, Mei 6, 2026
Yanga SC vs Dodoma Jiji FC, Mei 15,2026
Yanga SC vs Namungo FC, Mei 19,2026
Mashujaa FC vs Yanga SC, Mei 23,2026
Msimamo wa ligi (kwa ufupi)
Yanga SC ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara baada ya kukusanya pointi 38 katika michezo yao 16 wakiyocheza mpaka sasa. Nafasi ya pili inakamatiwa na Azam FC waliokusanya pointi 32 katika michezo 16, huku Simba SC wao wakiwa wamekusanya pointi 31 katika michezo 14. Ikumbukwe Simba SC leo Alhamisi watashuka Uwanja wa Jenerali Isamuhyo kuvaana na Coastal Union.
Wadhamini

Kwa sasa mdhamini mkuu wa klabu ni SportPesa, Pamoja nao wapo wadhamini wengine ambao ni GSM Group, ambao pia wanahusika na vifaa vya timu.
Usajili wa wachezaji

Katika dirisha kubwa la usajili, Yanga ilisajili wachezaji kadhaa wapya kama Mohamed Doumbia, Andy Boyeli, Israel Mwenda, Celestine Ecua, Lassine Kouma, Offen Chikola, Balla Conte, Casemiro na wengine huku dirisha dogo wakiwaleta, Buba, Depu, Masaranga.
Pia kulikuwa na baadhi ya wachezaji walioondoka wakiwemo Khalid Aucho, Ecua, Doumbia.
Thamani ya klabu ni kiasi gani?
Hivi karibuni kupitia mkutano mkuu wa mwaka wa Wanachama Yanga SC ilitolewa taarifa kuwa, timu hiyo kwa sasa inakadiriwa kufikia thamani ya takribani shilingi bilioni 100. Katika mchakato wa hisa wanachama wanamiliki asilimia 51, na wawekezaji binafsi asilimia 49. Tayari wawekezaji kadhaa akiwemo GSM, wameonyesha nia ya kununua hisa za timu hiyo.
Hitimisho
Yanga SC inaendelea kuwa moja ya klabu bora nchini ikiwa na kikosi imara na chenye malengo makubwa. Msimu wa 2025/26 unaonekana kuwa na ushindani mkali, lakini timu ina kila sababu ya kufanya vizuri na kuendelea kuleta furaha kwa mashabiki wake. Hii ina maana kazi kubwa inapaswa kufanyika kuwashinda washindani wake hususani Simba SC na zam FC.

