Elie Mpanzu na Steve Barker watikisa Bongo:  Wazoa tuzo Ligi Kuu ya NBC Oktoba, Takwimu, Matokeo

ByJoel Thomas

November 5, 2026
MpanzuMpanzuMpanzu

Elie Mpanzu na Steve Barker watikisa Bongo:  Wazoa tuzo Ligi Kuu ya NBC Oktoba, Takwimu, Matokeo

  • Elie Mpanzu na Steve Barker kutoka Simba SC wameandika rekodi ya pekee kwenye Ligi Kuu ya NBC.
  • Hii ni baada ya, Elie Mpanzu kuibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Oktoba, huku Steve Barker akizoa tuzo ya kocha bora wa mwezi Oktoba.
  • Tuzo hizo zinakuja kufuatia mafanikio makubwa waliyoyapata katika mwezi huo, katika utekelezaji wa majukumu yao.
  • Makala hii inachambua kwa ufupi takwimu zao kwa mwezi Oktoba.

Simba SC imeandika rekodi ya pekee msimu huu, hii ni baada ya Nyota wao, Elie Mpanzu na Steve Barker kufanikiwa kuzoa tuzo za mwezi Oktoba kwenye Ligi Kuu ya NBC. Elie Mpanzu ameibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi, huku Steve Barker akizoa tuzo ya kocha bora wa mwezi Oktoba. Tuzo hizo zinakuja kufuatia mafanikio makubwa waliyoyapata katika mwezi huo, katika utekelezaji wa majukumu yao.

SOMA HII PIA: Elie Mpanzu Kibisawala: Moto wa hatari NBC Premier League, Takwimu zake hizi hap ani balaa

Kuhusu tuzo Elie Mpanzu

Mpanzu -
Mpanzu –

Mpanzu alionesha kiwango kizuri chenye mwendelezo akiwashinda Iddi Selemani wa Azam FC na Nathaniel Chilambo wa Simba, alioingia nao fainali katika mchakato wa Tuzo hiyo. Ikumbukwe mchakato huo unasimamiwa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Mchezaji huyo alitoa mchango mkubwa kwa timu yake katika michezo mitatu ambayo ilicheza mwezi huo na kushinda yote, huku nyota huyo akifunga mabao matatu.

Kuhusu tuzo ya kocha Mkuu wa Simba SC, Steven Barker

Ratiba ya Simba SC CAF Champions League 2026/27
Steve Barker (-)

Kwa upande wa Barker aliyeingia fainali na Florent Ibenge wa Azam na Juma Mgunda wa Namungo, aliiongoza Simba kushinda michezo yote mitatu iliyocheza mwezi huo. Pia aliiongoza Simba SC kupanda kutoka nafasi ya pili hadi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC. Mpaka sasa Simba wamefanikiwa kukusanya pointi 30 wakiwa na asilimia 100.

Mabao 3 bora

Eli Mpanzu Kibisawala
Eli Mpanzu Kibisawala

Kamati pia imeteua mabao matatu bora, ambayo yatapigiwa kura na mashabiki ili kupata bao bora la mwezi Oktoba. Mabao hayo ni Hassan Mubiru (Azam v Mbeya City), Elie Mpanzu (Simba v Young Africans) na Selemani Bwenzi (Simba V Mashujaa). Bao litakalopata kura nyingi litaibuka na ushindi.

Shinda Milioni 800 za SportPesa, cheza kindege ‘aviator’ gusa hapa chini

image
Win big with Sportpesa Aviator

Meneja bora wa mwezi

Kamati ya Tuzo pia imemteua Meneja wa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Jackson Mwendwa kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Oktoba. Hii ni kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.

Hitimisho

Ligi Kuu Bara inazidi kupamba moto, huku Elie Mpanzu na Steve Barker wakizidi kupaa. Je, wataendelea kusalia katika viwango hivyo kuelekea mwezi Novemba. Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa zaidi za papo kwa hapo.

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.