- Umewekwa wazi mkakati wa usajili mpya Simba SC 2026/27, watatu wametambulishwa tayari
- Mbavy ya kulia Nathaniel Chilambo kutoka Azam FC ipo kwenye changamoto mpya unyamani
- Kelvin Nashon kiungo mkabaji kutoka Pamba Jiji FC ni mnyama
- Ukweli kuhusu Oura, Gueye na Loemba kuondoka huu hapa
Hatimaye umewekwa wazi mkakati wa usajili mpya Simba SC 2026/27 mara baada ya dirisha kufunguliwa Julai 6,2026. Ni Kelvin Nashon kiungo mkabaji alikuwa wa kwanza kutambulishwa unyamani. Msimu wa 2025/26 alikuwa Pamba Jiji FC.Tayari yupo kambini akiwa na timu nchini Rwanda ilipoweka kambi kwenye maandalizi ya Kagame Cup.
Ratiba ya Simba SC: Ratiba ya Simba SC mwezi huu wa 6, 2026 | Ligi Kuu NBC na CRDB Federation Cup, Takwimu |Mechi 6 za kufa na kupona | SportPesa Blog
Bado hujashinda? Cheza na ushinde mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa
Je, hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Mkakati wa usajili Simba SC 2026/27, Ahmed Ally afunguka

Hii hapa ratiba ya NBC Premier League: Ratiba ya Ligi Kuu ya NBC 2026/27: Mechi zote 240 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano amebainisha mkakati wa usajili mpya Simba SC 2026/27 namna unavyoendeshwa. Kiongozi huyo amebainisha kuwa wamefanya kazi kubwa kufuatilia wachezaji hivyo mashabiki wawe tayari. Aliongeza kwamba hakuna mchezaji mzuri atakayeondoka kwenye kikosi ikiwa wanamuhitaji.
“Kipindi cha usajili wa taifa kubwa Simba SC, tumeshatangaza wachezaji watatu. Tumewasajili sababu wameaminiwa na Simba SC waende wakafanye kazi. Sisi ndio tunafahamu ubora, thamani na kiwango chao.
“Usajili bado haujakamilika, tunaendelea kusajili na tunaendelea kutambulisha. Yupo mchezaji mmoja tunapata wasiwasi kumtangaza maana dunia itabadilisha tabia yake kwahiyo tunapata mashaka tunaweza kuathiri dunia lakini hakuna namna tutamtambulisha watu waone mali halali ya Simba SC.
Libasse na Oura wanauzwa?
“Kumekuwa na maneno mengi kwamba Libasse anauzwa, Oura anauzwa au Loemba anaondoka lakini nawatangazia kwamba hakuna mchezaji hata mmoja ambaye anaondoka. Yoyote bora ambaye unamfahamu bado ataendelea kuwepo.
Simba Day itafanyika wapi?
“Simba Day 2026 itafanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, kutokana na ukubwa wa tamasha hili duniani tunatamani kufanyika kwenye Uwanja wa Mkapa lakini kwa sasa upo kwenye matengenezo hivyo uwanja ambao utatumika ni Uwanja wa Uhuru. Tayari tumefanya ukaguzi na kupokea maelekezo kutoka kwa wasimamizi. Tamasha hilo litatumika pia kuadhimisha miaka 90 ya Simba SC,” alisema Ahmed Ally.
Wachezaji wapya Simba SC

Mchezaji wa kwanza kutambulishwa Simba SC ni Kelvin Nashon alikuwa Pamba Jiji FC, mchezaji wa pili ni Nathaniel Chilambo alyekuwa Azam FC. Nyota wa tatu kutambulishwa ni Bakari Msimu aliyekuwa Coastal Union ya Tanga.Wachezaji hawa wapo na timu Rwanda ambapo imeweka kambi huko kwenye maandalizi ya Kagame Cup.
Hitimisho
Ni mkakati wa usajili mpya Simba SC 2026/27 inayonolewa na Kocha Mkuu, Steve Barker. Timu hiyo ilimaliza msimu wa 2025/26 ikiwa nafasi ya pili.Itafungua pazia kwa kumenyana na Kagera Sugar iliyopanda daraja, Agosti 16,2026.

