Simba SC na Steve BarkerSteve Barker (-)Steve Barker (-)

Simba SC na Steve Barker
Rushine nyota wa Simba SC

Simba SC na Steve Barker: Maandalizi ya CAF Champions League 2026/27

  • Mikakati ya Simba SC na Steve Barker kwenye CAF Champions League 2026/27 inazidi kupangwa kwa hesabu kali.
  • Mnyama amepangwa Kundi C mchezo wa kwanza aatanza na Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Uwanja wa Uhuru.
  • Timu hiyo imerejea kambini ikiwajumuisha wachezaji baadhi Clatous Chama, Rushine, Elie Mpanzu, Kibabage.

Ni Simba SC na Steve Barker wanajiandaa kikamilifu kwa ajili ya mechi za hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) 2026/27. Mashabiki wa Msimbazi wana hamu kubwa ya kuona timu yao ikifanya vizuri katika mashindano haya makubwa barani Afrika.Maandalizi haya yanajumuisha mikakati mbalimbali ya kiufundi na kimbinu, huku jukumu la kocha Steve Barker likiwa muhimu sana. Klabu inalenga kuhakikisha inakuwa na kikosi imara na chenye ushindani mkubwa.

SOMA HII PIA:Ratiba ya Simba SC CAF Champions League 2026/27 | Kundi C | Msimamo | SportPesa Blog

Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha kindege kwa shilingi 1

Una nafasi yakushinda mpaka milioni 800 ukipaisha kindege sasa hivi na SportPesa. Marubani wapo hewani wanavuna mkwanja kwa kuanzia shilingi 1 tu na kuna zawadi kibao zinakusubiri. Zamu yako ni sasa bofya hapa chini uanze safari:-

image

Jukumu la Kocha Mkuu Steve Barker

Kwa upande wa Simba SC na Steve Barker wanaendelea na mikakati kufanya vizuri kwenye mechi zijazo.Baada ya kutinga hatua ya makundi hesabu kubwa ni kusonga mbele mpaka robo fainali.Haya yote yanahitaji muda na utayari.

Steve Barker amebainisha kuwa kundi ambalo wapo watapambana kupata matokeo mazuri.Ikumbukwe kwamba baada ya droo kucheza Simba SC imepangwa Kundi C. RS Berkane ya Morocco, Orlando Pirates ya Afrika Kusini na Colombe sportive ya Cameroon ni wapinzani wa mnyama.

“Jukumu kubwa ni kuona tunapata matokeo mazuri.Ushindani ni mkubwa kutokana na hatua ambayo tupo.Wachezaji na uongozi malengo makubwa ni kuona tunasonga mbele zaidi,”.

Mikakati ya Simba SC kuelekea msimu mpya

Simba SC inatarajiwa kuweka mikakati ya usajili itakayolenga kuimarisha maeneo yenye upungufu katika kikosi. Lengo ni kupata wachezaji wenye uzoefu na uwezo wa kuleta mabadiliko chanya ndani ya timu.Eneo ambalo litafanyiwa maboresho makubwa ni ushambuliaji.Ibrahim Doumbia raia wa Mali hajawa katika ubora kwa msimu wa 2026/27.

Pia, klabu itazingatia programu za mazoezi zitakazowajengea wachezaji utimamu wa mwili na stamina ya kutosha kukabiliana na ratiba ngumu ya mashindano ya kimataifa na ligi ya ndani, NBC Premier League.Timu hiyo imerejea kambini Mo Arena kwa maandalizi ya mechi zijazo.Clatous Chama, Rushine, Shomari Kapombe, Elie Mpanzu, Ibrahim Doumbia ni wachezaji waliopo kambini baadhi.

Matarajio ya mashabiki na umuhimu wa CAF Champions League

Mashabiki wa Simba SC wana matarajio makubwa ya kuona timu yao ikivuka hatua za makundi na kufika mbali zaidi katika CAF Champions League. Mafanikio katika mashindano haya huongeza hadhi ya klabu na soka la Tanzania kwa ujumla.Ushiriki mzuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika pia huwapa wachezaji fursa ya kuonyesha vipaji vyao na kujipatia uzoefu muhimu wa kimataifa.

SOMA HII PIA:Simba SC vs Orlando Pirates CAF Champions League 2026/27 | H2H | Live score

Hitimisho

Ni Simba SC na Steve Barker wapo na kibarua kikubwa kutimiza majukumu yaliyopo mbele yao.Upande wa timu jukumu kubwa kuhakikisha kila mahitaji ya benchi la ufundi yanapatikana.Benchi la ufundi litakuwa na jukumu kuwapa furaha mashabiki na matokeo mazuri uwanjani kupitia kwa wachezaji.

 

Share this: