- Ratiba ya Simba SC kwa mwezi Juni 2026 imethibitishwa rasmi na uongozi wa timu hiyo, kupita akaunti zao rasmi za mitandao ya kijamii.
- Ratiba hiyo inaonyesha kuwa Simba SC wanatarajia kuwa na mechi 6 nzito za kufungia msimu huu wa 2025/26.
- Kati ya mechi hizo, mechi 5 ni zile za Ligi Kuu ya NBC na mechi moja iliyosalia ni ya Nusu Fainali ya mashindano ya CRDB Federation.
- Makala hii inakuchambulia ratiba hiyo
Ratiba ya Simba SC kwa mwezi Juni 2026 imetoka rasmi na kuthibitishwa na uongozi wa timu hiyo, kupita akaunti zao rasmi za mitandao ya kijamii. Ratiba hiyo inaonyesha kuwa Simba wanatarajia kuwa na mechi 6 za kufa na kupona. Kati ya mechi hizo ni mechi 5 ni zile za Ligi Kuu ya NBC, ambazo ndiyo mechi za mwisho kabla ya kufunga msimu wa 2025/26. Mechi moja iliyosalia ni ya mashindano ya Nusu Fainali ya mashindano ya CRDB Federation.
Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Ligi Kuu ya NBC 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.
Bado hujashinda? Cheza na ushinde mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa
Je, hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Aviator: High-flying wins up to 800,000,000.
Kuhusu ratiba ya Simba SC mwezi huu wa 6, 2026

Kikosi cha Simba SC tayari kimerejea kambini, Baada ya mapumziko ya takribani wiki moja. Simba SC kwa sasa wanakamatia nafasi ya 2 kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC na pointi zao 58 walizokusanya katika michezo 25. Baada ya kurejea kambini, tayari wameanza maandailzi kwa ajili ya mechi za kufungia msimu.
Simba wataanza kampeni yao ya kufungia msimu kwa kuvaana na Pamba Jiji FC, Juni 14, 2026. Juni 17, 2026 Simba watakuwa ugenini kuvaana na Mbeya City FC. Baada ya mchezo huo Simba SC itageukia kwenye CRDB Federation Cup, hatua ya nusu fainali vs Coastal Union Juni 20, 2026.
Juni 24, 2026 Simba SC watarejea tena kwenye ratiba ya Ligi Kuu NBC ambapo watavaana na Mtibwa Sugar. Baada ya hapo Simba SC watakuwa na mechi 2 za nyumbani ambazo ni vs Singida Black Stars Juni 27, 2026 kabla ya kumaliza na KMC Juni 30, 2026. Mpaka hapo hesabu za msimu huu wa 2025/26 zitakuwa zimefikia tamati, na utasalia mchezo mmoja tu wa Fainali ya CRDB Federation ikiwa Simba SC watafanikiwa kufika fainali. Jedwali lifuatalo linaelezea kwa ufupi ratiba hiyo;
Ratiba ya mechi zijazo Simba SC NBC Premier League
| Tarehe | Mechi | Uwanja |
|---|---|---|
| 14 Juni 2026 | Simba SC vs Pamba Jiji FC | KMC Complex |
| 17 Juni 2026 | Mbeya City vs Simba SC | Sokoine, Mbeya |
| 20 Juni 2026 | Simba SC vs Coastal Union (Kombe la CRDB Federation) | TBA |
| 24 Juni 2026 | Mtibwa Sugar vs Simba SC | Jamhuri |
| 27 Juni 2026 | Simba SC vs Singida Black Stars | KMC Complex |
| 30 Juni 2026 | Simba SC vs KMC | KMC Complex |
SOMA HII PIA: Ratiba ya mechi zilizobakia za Simba SC kwenye NBC Premier League 2025/26 | SportPesa Blog
Semaji Ahmed Ally afunguka kuhusu ratiba ya Simba SC

Kufuatia ratiba hiyo, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally amesema: “Kufuatia mapumziko ya takribani wiki moja kukamilika, wachezaji wetu wamerejea kambini rasmi kwa maandalizi ya mechi zinazofuata. Wachezaji waliorejea kambini ni wale ambao hawana majukumu ya kitaifa, wale ambao wana majukumu ya kitaifa wataendelea na programu huko waliko.
“Kama timu malengo yetu ni kuhakikisha, tunakamilisha msimu kwa mafanikio kwenye mechi ambazo zimebaki. Benchi la ufundi linaendelea na maandailzi hayo, katika Uwanja wa Simba Mo Arena. Ikumbukwe ratiba hii ina mechi za CRDB Federation Cup, na zile za NBC Premier League ambazo zote tunazichukulia kwa uzito mkubwa.
SOMA HII ZAIDI: Ratiba ya Simba SC NBC Premier League 2025/26 ni moto | Msimamo, Mzizima Dabi, Kariakoo Dabi
Hitimisho

Ratiba ya mechi zilizobaki za Simba ina maana kubwa kwa timu hiyo, kwani mechi 6 zilizosalia kwa mwezi huu ni za kufa na kupona. Wakiwa na pointi 58 katika michezo yao 25 waliyocheza, Simba SC ndiyo timu pekee ambayo inaonekana kuwa mpinzani mkubwa kwa Yanga SC kwenye vita ya ubingwa. Simba pia wamefuzu hatua ya Nusu Fainali ya mashindano ya CRDB Federation, mashindano ambayo ni ya pili kwa hadhi ya ukubwa nchini. Je, Simba SC watavuna nini? tusubiri na kuona panapo majaaliwa ya uhai.
SOMA HII PIA: Simba SC: Latest Results, Fixtures, Standings, Squad and Next Match

