- Usajili wa Yanga SC kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC 2026/27 unazidi kupamba moto.
- Baada ya kukamilisha kutambulisha benchi jipya la ufundi la timu hiyo, sasa uongozi wat imu hiyo unaendelea kutangaza wachezaji wao wapya.
- Miongoni mwa Sajili ambazo zimekamilika na kutangazwa ni ya staa wa zamani wa KMC, Erick Mwijage.
Zikiwa zimebaki siku chache kuelekea kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2026/27, uongozi wa Yanga SC umeendelea kufanya usajili wa maboresho ya kikosi chao. Miongoni mwa taarifa kubwa kwa timu hiyo ni mabadiliko ya benchi la ufundi, ambalo kwa sasa linaongozwa na kocha raia Manqoba Mngqithi. Lakini tayari uongozi wa timu hiyo umekamilisha baadhi ya Sajili za wachezaji na kuwatangaza huku Nyota, Erick Mwijage akiwa ndiye mchezaji wa hivi karibuni zaidi kutangazwa. Makala hii inachambua kwa ufupi takwimu za Mwijage.
Cheza sasa ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Bado hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Kuhusu usajili wa Yanga SC na utambulisho wa Erick Mwijage
Mwijage amejiunga na Yanga SC, akisajiliwa kutoka kikosi cha KMC ambayo tayari imeshuka daraja. Mwijage ndani ya Ligi Kuu ya NBC amefanikiwa kupita ndani ya timu mbalimbali ikiwemo; Kagera Sugar na Geita Gold. Mwijage anakuwa mchezaji wa 5 kusajiliwa na Yanga SC na kutambulishwa ndani ya dirisha hili la usajili.
Taarifa binafsi za mchezaji: Umri na takwimu

Kuzaliwa: 15/11/2001 (24)
Mahali: Bukoba, Tanzania
Urefu: 1,72 m
Uraia: Tanzania
Nafasi: Winga wa kushoto
Klabu: Yanga SC
Mguu: Anatumia zaidi mguu wa kulia
KUSOMA KUHUSU MKATABA MPYA WA OKELLO, SOMA HII: Usajili Yanga SC umeanza Emmanuel Samuel asaini miwili/ Okello mkataba mpya
Tuzo binafsi za Mwijage

Akiwa na jezi ya timu ya KMC msimu uliopita Mwijage alifanikiwa kushinda tuzo mbalimbali, ikiwemo mchezaji bora wa mechi kadhaa ikiwemo dhidi ya Namungo na Kagera Sugar. Sasa ni wakati wa kuonyesha makali yake ndani ya kikosi cha Yanga SC.
KUSOMA TETESI ZA USAJILI 2026/27, SOMA HII: Tetesi za usajili 2026/27: Yanga SC inamuwinda winga wa Kaizer Chiefs, Makabi Lilepo/ Kambi na wachezaji watakaosajiliwa
Hitimisho
Usajili mpya wa Yanga SC unazidi kupamba moto na Mwijage ni miongoni mwa wachezaji bora wanaochipukia Tanzania. Nyota huyo amekuwa anazivutia klabu kubwa ndani nan je ya Tanzania. Swali ni je, Mwijage ataweza kuthibitisha uwezo wake na kupambania namba? Endelea kufuatilia SportPesa blog.

