- Usajili mpya Simba SC unaendelea kutikisa, ambapo timu hiyo imeanza balaa mapema, zikibaki siku chache kuelekea kufunguliwa kwa dirisha kubwa la usajili.
- Ligi Kuu Bara (NBC Premier League), iko karibu kumalizika, ambapo mpaka sasa zimesalia mechi 7 tu.
- Kuelekea msimu mpya wa 2016/17 Simba SC wanaonekana kupania makubwa, ambapo tayari wanaripotiwa kumalizana na baadhi ya mastaa wakubwa.
- Baada ya kuwapa mikataba mipya mastaa kama, Rushine De Ruck na Ellie Mpanzu, Simba SC sasa inaelezwa kuwageukia Clatous Chama na Abdul Sopu.
Yametimia! Tetesi za usajili mpya Simba SC zinaendelea kutikisa, hii ni kuelekea kufunguliwa kwa dirisha kubwa la usajili. Ligi Kuu Bara (NBC Premier League), iko karibu kumalizika, ambapo mpaka sasa zimesalia mechi 7 tu. Kuelekea msimu mpya wa 20216/17 Simba SC wanaonekana kupania, ambapo tayari wanaripotiwa kumalizana na baadhi ya mastaa wakubwa wakiwemo Clatous Chama na Sopu.
Fuatilia mwenendo wa usajili wa timu mbalimbali za Ligi Kuu Bara (NBC Premier League); Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.
Je, unataka kushinda mamilioni? Unaweza kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 na SportPesa
Wengi tayari wamevuna mamilioni kupitia mchezo wa Kindege yaani ‘Aviator’ ya SportPesa. Wewe unasubiri nini? Nafasi ni yako cheza Aviator na kushinda mpaka Shilingi Milioni 800 sasa kwa kubonyeza picha hii chini.

Aviator: Paisha kindege ushinde mpaka zaidi ya 800,000,000.
Tetesi za usajili mpya Simba SC
Clatous Chama

Kwa mujinu wa Mwandishi wa Habari nguli za usajili nchini, Hans Raphael ameripoti taarifa kuwa tayari, Clatous Chama amesaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Simba SC. Ikumbukwe Chama alijiunga na Simba SC katika dirisha dogo msimu huu, na kusaini mkataba wa mwaka mmoja akitokea Singida Black Stars. Kiungo huyo wa kimataifa wa Zambia ameonekana kurejesha makali ya Simba SC, akiwa miongoni mwa wachezaji bora wa kikosi hiko kwa sasa.
Hans Raphael amesema: “Taarifa mpya ni kuwa Chota Chama atasalia Sima SC. Kiungo wa Simba, Clatous Chota Chama mwenye umri wa miaka 34, amesaini mkataba wa miaka miwili kubaki Simba SC. Kıla kitu kimekamilika na Chama kasaini hadi 2028, Chama hakutaka kwenda popote zaidi ya kubaki Simba.”
Katika dirisha dogo la msimu huu taarifa za Chama kurudi Simba SC kwa wengi hazikupewa uzito mkubwa, hasa kutokana na namna ambavyo waliachana. Lakini kufuatia mwenendo wa kusuasua ambao Simba SC walikuwa nao, tetesi hizo zilitimia. Taarifa kutoka ndani ya Simba SC zimeeleza kuwa, chanzo kikuu ni familia ya staa huyo, ambayo kwa muda mrefu ilitamani kuona akirejea Msimbazi.
SOMA HII PIA: Usajili Simba SC umeanza mapema | Orodha na rekodi za wachezaji walioongeza kandarasi unyamani
Takwimu za Chama msimu huu
Chama msimu huu amefanikiwa kuhusika kwenye mabao 12, akifunga mabao 8 na kuasisti mara 4. Kwenye orodha ya wafungaji anakamatia nafasi ya tatu nyuma ya Feisal Salum wa Azam, anayeongoza na mabao 11 na Prince Dube wa Yanga mwenye mabao 9. Chama pia hivi karibuni aliandika rekodi kali ya kushinda mchezaji bora wa mechi 4 mfululizo.
Simba SC kumchomoa Sopu Azam?

Tetesi nyingine za usajili zilizoshtua, ni kuhusu uongozi wa Simba SC kuwa kwenye mipango ya kumsaini mshambuliaji wa Azam FC, Abdul Sopu. Akiwasilisha taarifa hiyo, Hans Raphael amefichua kuwa Simba SC wanakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Azam FC na timu ya taifa ya Tanzania, Abdul Hamisi Suleiman. Sopu mwenye miaka 25, alikulia kisoka ndani ya Simba SC kabla ya kutimkia timu mbalimbali, huku akifanya makubwa zaidi akiwa na Coastal Union. Simba wako kwenye hatua za mwisho kumpata Sopu na tayari makubaliano binafsi Kati ya Simba na mchezaji yamefikiwa.
SOMA HII ZAIDI: Usajili wa Chama Simba SC washtua! Mayele, Kagere, Okwi wafunguka Mazito
Hitimisho

Tetesi za usajili wa mpya Simba SC, zimeanza mapema, hii inaonyesha dhamira ya dhati ya uongozi wa timu hiyo kujenga timu bora na ya ushindani mkubwa zaidi kwa msimu ujao. Simba wapo kwenye mbio za ubingwa, ambapo kabla ya mchezo wao wa leo dhidi ya Coastal Union walikuwa wameachwa pointi 2 tu, na wapinzani wao wakuu Yanga SC. Mpaka sasa Simba tayari wameongeza mikataba ya baadhi ya mastaa wao wakiwemo Kagoma, Rushine na Mpanzu.
SOMA HII PIA: Simba SC kufanya usajili mkubwa | Maeneo yatakayoboreshwa | Mo atoa tamko zito | Ahmed atamba

