
Azam FC Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika 2026/27 | SportPesa Blog
- Ni Azam FC hatua ya makundi Kombe la Shirikisho imerejea kwa mara nyingine tena kuperusha bendera ya Tanzania.
- Timu hiyo inanolewa na Kocha Mkuu, Florent Ibenge mara ya kwanza ilikuwa 2025/26 ilipangwa Kundi B.
- 2026/27 tena imepangwa Kundi B itapambana na Al Hilal Tripoli, AS FAR na Durban FC.
Azam FC hatua ya makundi imefanya kweli kwa mara nyingine tena. Klabu hiyo yenye maskani yake Chamazi, Dar es Salaam, imefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya pili mfululizo katika historia yake. Mafanikio haya yamekuja baada ya kuiondoa ZED FC ya Misri kwa jumla ya mabao 2-1.Mara ya kwanza ilikuwa 2025/26 tangu klabu hiyo ianzishwe 2004 na ilipangwa Kundi B ikimaliza nafasi ya 3 na pointi 9.
Safari hii ya kihistoria inatoa matumaini mapya kwa soka la Tanzania na inaiweka Azam FC kwenye ramani ya klabu kubwa barani Afrika.Inanolewa na Florent Ibenge aliyekiongoza kikosi msimu wa 2025/26 kushinda mechi 3 na kupoteza mechi 3. Mashabiki wa Azam FC sasa wana hamu kubwa ya kujua nini kitafuata katika hatua hii ya makundi.
SOMA HII PIA:Azam FC:Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika na hesabu robo fainali
Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha kindege
Una nafasi yakushinda mamilioni ukipaisha kindege sasa hivi na SportPesa. Marubani wapo hewani wanavuna mkwanja. Zamu yako ni sasa bofya hapa chini.
Jinsi Azam FC ilivyofuzu hatua ya makundi
Azam FC ilianza kampeni yake ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kishindo. Baada ya kuiondoa KMKM SC kwa jumla ya mabao 5-0 katika raundi ya kwanza, walikabiliana na kibarua kigumu dhidi ya ZED FC ya Misri.
Katika mchezo wa mkondo wa kwanza, Azam FC ilianza na sare ya kufungana 1-1 ugenini. Kisha, katika mchezo wa marudiano, walifanikiwa kupata ushindi wakiwa nyumbani wakafanikiwa kuvuka salama kwa jumla ya mabao 2-1. Hii inathibitisha ubora na maandalizi mazuri ya kikosi hicho.
Athari za kufuzu kwa Azam fc
Kufuzu kwa hatua ya makundi ni hatua kubwa kwa Azam FC. Kwanza, inawawezesha kupata uzoefu muhimu wa mashindano ya kimataifa, jambo ambalo litasaidia kukuza wachezaji wao na kuongeza ushindani katika Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League).Huku ushindani ni mkubwa vinara wakiwa ni Simba SC,Yanga SC mabingwa watetezi na Azam FC nafasi ya 3.
Pili, mafanikio haya yataongeza hadhi ya klabu na kuvutia wadhamini zaidi, jambo litakalosaidia katika uendeshaji wa klabu. Pia, ni fursa kwa wachezaji wa Azam FC kujionyesha kwa skauti wa kimataifa.
SOMA HII PIA:Azam FC watatoboa Makundi CAFCC? Ratiba, matokeo, mashindano ya CAF 2026/27
Hitimisho
Mafanikio ya Azam FC kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ni jambo la kujivunia kwa Tanzania. Ni matumaini kuwa wataendelea kufanya vizuri na kuwakilisha nchi yetu kwa heshima katika mashindano haya makubwa.Chini ya Kocha Mkuu, Florent Ibenge ina kazi ya kusaka tiketi kutinga hatua ya robo fainali.


