- Mexico vs England FIFA Kombe la Dunia 2026, ni ratiba ya mechi kali ya hatua ya 16 bora ya mashindano haya itakayopigwa usiku wa kuamkia Jumatatu 6 July 2026.
- Mechi hii itapigwa kwenye Uwanja wa Mexico City, Mexico kuanzia majira ya saa tisa usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
- Mexico waandaaji wenza wa mashindano haya wakiongozwa na mastaa kama Guillermo Ochoa na Julián Quiñones watavaana na England ya mastaa Harry Kane na Decline Rice.
- Makala hii inachambua h2h, livescore, takwimu na Habari za timu za mechi hii kama ifuatavyo
Mexico walioanza kwa kishindo mashindano ya FIFA Kombe la Dunia 2026, watakuwa na mtihani mgumu nyumbani pale watakapovaana na England usiku wa kuamkia Jumatatu 6 July 2026. Mechi hii inatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Mexico City majira ya saa 9 usiku wa kuamkia Jumatatu kwa saa za Afrika Mashariki. Mechi hii kwa ufupi ni vita ya safu mbili zilizojipambanua kuwa bora sana za ushambuliaji, katika mashindano haya wakiwemoGuillermo Ochoa, Julián Quiñones, Harry Kane na Decline Rice. Makala hii inachambua baadhi ya takwimu muhimu za mchezo huu, ikiwemo h2h, taarifa za timu, Lineups.
Hizi hapa Odds bora za SportPesa za mechi ya Mexico vs England
Kwa wanaotafuta odds bora, SportPesa inatoa masoko mbalimbali ya ubashiri pamoja na malipo ya haraka. kwa sasa odds zimeboreshwa na unaweza kubashiri mechi hii sasa gusa hapo chini, ili kubashiri moja kwa moja.

Maelezo ya Mechi
| Kipengele | Maelezo |
|---|---|
| Mashindano | Mchezo huu ni wa hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia la FIFA 2026, ambapo timu zitachuana kwa mfumo wa mtoano, na mshindi pekee ndiye atakayefuzu kwenda robo fainali. |
| Tarehe na Muda | Mechi imepangwa kuchezwa usiku wa Jumapili, Julai 5, 2026 kuamkia Jumatatu 6 Julai 2026, kuanzia saa 9:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki (EAT), ambayo ni alfajiri ya Jumatatu katika baadhi ya maeneo. |
| Uwanja | Mchezo utafanyika katika Uwanja wa Azteca, uliopo Mexico City, Mexico, moja ya viwanja vinavyotumika kuandaa michezo ya Kombe la Dunia la FIFA 2026. |
KUJUA RATIBA YA MECHI ZOTE 8 ZA HATUA YA 16 BORA, SOMA HII: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 hatua ya 16 bora | Mechi zote 8 | Utabiri | Odds kubwa | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Muhtasari wa Mexico vs England FIFA Kombe la Dunia 2026

Moto utawaka kwenye Uwanja wa Mexico City nchini Mexico, katika mchezo mkali wa hatua ya 16 bora utakaochezwa 6 July 2026. Wenyeji Mexico wameushtua Umma wa soka kwa kuanza kwa kishindo mashindano hayo, baada ya kuandika rekodi ya kushinda mechi zote za hatua ya makundi nah atua ya 32 bora tena bila kuruhusu bao. Huku England nao wakionyesha kuboresha zaidi kiwango chao.
Macho yote yatakuwa yakielekezwa kwenye Uwanja wa Mexico City, ambao pia unajulikana kama Estadio Azteca usiku wa kuamkia Jumatatu. Hii ni katika kushuhudia wenyeji wenza wa mashindano hayo, Mexico wakikabiliana na England katika mxchezo wa hatua ya 16 Bora. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa England kurejea katika uwanja huo maarufu wa Mexico City, tangu mechi yenye kumbukumbu nyingi ya Kombe la Dunia ya mwaka 1986.
Katika mchezo huo ndipo tukio maarufu la bao la mkono la Diego Maradona, maarufu kama ‘hand of god’ lilifungwa. Aidha, huu utakuwa mchezo wa mwisho kwa Mexico kufurahia faida ya kucheza nyumbani, katika Kombe la Dunia la mwaka huu. Kikosi cha Mexico kinachoongozwa na kocha, Javier Aguirre kimekuwa na kampeni bora mbele ya mashabiki wao, kikishinda mechi zote 4 walizocheza bila kuruhusu bao.
Katika hatua ya 32 bora Mexico walifanikiwa kuichapa Ecuador mabao 2-0. Raúl Jiménez alifunga bao katika ushindi huo na kufikisha mabao mawili katika michezo mitatu, ya mashindano haya. Takwimu muhimu ya kuzingatia ni kwamba Mexico imepoteza mechi mbili pekee kati ya michezo 89 ya mashindano iliyocheza katika Uwanja wa Azteca.
KUANGALIA UCHAMBUZI WA MECHI IJAYO YA MISRI: Prediction Australia vs Misri FIFA Kombe la Dunia 2026: Hatua ya 32 bora, Team news, odds, lineups
Habari za Timu na majeruhi
Bado hakuna taarifa rasmi ya majeruhi wapya kutoka kambi za timu zote mbili, hivyo kila timu inatarajiwa kutumia wachezaji wake bora na walio tayari katika mcezo huu.
Vikosi vinavyotarajiwa
Mexico

| Idara | Wachezaji |
|---|---|
| Kipa | Rangel |
| Mabeki | Sanchez, Montes, Vasquez, Gallardo |
| Kiungo wa Ulinzi | Lira |
| Viungo wa Kati | Mora, Romo |
| Washambuliaji | Alvarado, Jimenez, Quinones |
| Mfumo wa Uchezaji | 4-1-2-3 |
England
| Idara | Wachezaji |
|---|---|
| Kipa | Pickford |
| Mabeki | Rice, Guehi, Konsa, O’Reilly |
| Viungo wa Kati | Anderson, Bellingham |
| Viungo Washambuliaji | Saka, Rogers, Gordon |
| Mshambuliaji | Kane |
| Mfumo wa Uchezaji | 4-2-3-1 |
KUJUA KUHUSU UCHAMBUZI WA MECHI ZOTE 104, SOMA HII: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Rekodi ya Mexico vs England H2H
Timu hizi zimekutana mara 9 katika mashindano tofauti na mechi za kirafiki, ambapo England wamekuwa bora zaidi wakishinda mechi 6. Mexico wao wameshinda mechi 2 pekee, huku mchezo mmoja uliosalia ukiisha kwa sare. Je nini kitatokea katika mchezo huu? Mashabiki wanasubiri dakika 90 za mechi.
Utabiri wa Mexico vs England (zaidi ya mabao 2 yaani over 1.5)

Kwa namna mchezo huu unavyotarajiwa kuwa Mexico italazimika kushambulia mbele ya mashabiki wake, badala ya kujilinda kwa muda mwingi. Hali hiyo itaacha nafasi ambazo England imekuwa ikizikosa katika michezo yake ya awali, na kuwapa nafasi wachezaji wao wa safu ya ushambuliaji kuonyesha uwezo wao wa kufunga.Hivyo uchambuzi wetu wa tathimini na maoni ya kiuhariri tunatabiri mechi ya mabao zaidi ya mawili. Ikumbukwe haya si matokeo rasmi, hivyo chambua odds zako na ubashiri kistaarabu.
KUHUSU UCHAMBUZI WA MECHI IJAYO YA FRANCE, SOMA HII: Prediction: Paraguay vs Ufaransa FIFA Kombe la Dunia 2026: Hatua ya 16 bora, team news, odds, h2h
Hitimisho

Uchambuzi wa kitaalamu wa mchezo huu unaipa nafasi kubwa mechi kushuhudia mabao mengi, wenyeji Mexico wana nafasi kubwa ya kufanya maajabu mbele ya mashabiki wao. Licha ya matarajio hayo, pia inatarajiwa mchezo utakuwa mgumu, kwani waandaaji wenza watataka kuandika historia mpya. Huu ni mchezo wa mwisho wa hatua ya 32 bora, fuatlia SportPesa blog kwa taarifa zaidi.

