- Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 hatua ya 16 bora tayari imethibitishwa kwa baadhi ya mechi, hii ni baada ya kuelekea ukingoni kwa hatua ya 32 bora.
- Hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia 2026 inatarajiwa kuanza kutimua vumbi siku ya Jumamosi, huku mchezo wa kwanza wa hatua hiyo ukiwa ni Canada vs Morocco.
- Ikumbukwe toleo la Kombe la Dunia la FIFA 2026 linafanyika kwa ushirikiano wa nchi 3, ambazo ni; Marekani (USA), Canada na Mexico.
- Mechi 8 zitapigwa baina ya timu 16 zilizofuzu kutoka hatua ya 32 bora ya mwaka huu, ambazo ni: Canada, Brazil, Paraguay, Morocco, Norway, France, Mexico, England, Belgium na United States, makala hii inakuletea ratiba ya mechi zote 8 zitakazochezwa, muda zitakapochezwa na viwanja vitakavyotumika na utabiri.
Ratiba ya FIFA Kombe la Dunia 2026 hatua ya 16 bora itaanza kutimua vumbi rasmi siku ya Jumamosi 4 July 2026. Ikumbukwe haya ni mashindano makubwa zaidi ya soka duniani, ambayo hufanyika kila baada ya miaka 4, mwaka huu Kombe la Dunia litafanyika kwa ushirikiano wa maandalizi ya nchi 3, ambazo ni; Marekani (USA), Canada na Mexico. Mpaka Makala hii inaandikwa tayari timu 10, zilikuwa zimefuzu hatua ya 16 bora hii ambazo ni: Canada, Brazil, Paraguay, Morocco, Norway, France, Mexico, England, Belgium, United States na zimesalia timu 12 zinazopambania nafasi 6 zilizobaki. Makala hii inakuletea ratiba ya mechi zote 8 zitakazochezwa katika hatua ya 16 ya mashindano haya, utabiri, muda zitakapochezwa na viwanja vitakavyotumika.
Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Kombe la Dunia 2026; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog na ushinde mamilioni kwa kubashiri kupitia odd kubwa za SportPesa. Unaweza kuwea ubashiri wako moja kwa moja kwa kubonyeza mchanganuo wa odds kubwa chini ya kila picha.
Kuhusu mechi za FIFA Kombe la Dunia 2026 hatua ya 16 bora
Hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia la FIFA 2026 inatarajiwa kuanza kwa kishindo Jumamosi 4 July 2026, ambapo tayari kuna michezo mikubwa yenye hadhi ya Robo Fainali. Baadhi ya mataifa yenye nguvu na ubora kisoka yamefuzu hatua hiyo, huku pia kukiwepo baadhi ya timu zilizoshangaza wengi.
Paraguay vs France (5 July 2026 saa 6 usiku)


Utabiri: Ufaransa kushinda
Hii inaonekana kuwa moja ya mechi kubwa zinazosubiriwa kwa hamu, hasa baada ya Paraguay kuishtua Dunia kwa kuiondosha Ujeruani. Ufaransa wanaingia katika mchezo huu utakaopigwa Uwanja wa Philadelphia, wakitajwa kuwa timu bora zaidi ya mashindano haya ikichagizwa na safu kali ya ushambuliaji inayoundwa na; Kylian Mbappé, Michael Olise na Ousmane Dembélé.
Wachezaji wa kufuatilia
Kylian Mbappé
Michael Olise
Ousmane Dembélé
Kujua ratiba ya mechi zote 104 soma hii: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Canada vs Morocco (4 July 2026 zaa 2 usiku)


Utabiri: Morocco kushinda
Wengi walidhani Uholanzi wangeidhibiti Morocco, lakini imekuwa tofauti kwani wababe hao wa Afrika wamezidi kuonyesha hawachekeshi. Canada kama taifa mwandaaji mwenza, nao wanaonekana kutaka kuandika rekodi, hivyo sit imu ya kubeza. Atakayechanga karata vizuri katika mchezo huu utakaopigwa Uwanja wa Houston, USA bila shaka atapata matokeo.
Wachezaji wa kufuatilia
Ismael Saibari
Alphonso Davis
Jonathan Davis
Achraf Hakimi
USA vs Belgium ( 7 July 2026 saa tisa usiku)
Utabiri: USA kushinda
Wenyeji wa mashindano haya USA wamekuwa sehemu ya sapraiz baada ya kuonyesha kiwango bora kwa kushinda mechi 2 za Makundi. Mchezo huu utapigwa Uwanja wa Seattle, nchini USA.

Wachezaji wa kufuatilia
Jérémy Doku
Lomelo Lukaku
Kevin De Bruyne
Christian Pulisic
Weston McKennie
Soma hii: Prediction: Paraguay vs Ufaransa FIFA Kombe la Dunia 2026: Hatua ya 16 bora, team news, odds, h2h
Brazil vs Norway (5 July 2026 saa tano usiku)


Utabiri: Brazil kushinda
Hii ni mechi ambayo mashabiki wa soka wangependa sana kuiona. Mastaa kama, Erling Haaland na Martin Ødegaard, watavaana uso kwa uso na Brazil iliyo na Vinicius Jr na Matheus Cunha.
Wachezaji wa kufuatilia
Vinícius Júnior
Neymar
Rodrygo
Erling Haaland
Martin Ødegaard
England vs Mexico (6 July 2026 saa tisa usiku)
Utabiri: Mexico kushinda
Kucheza mechi ya mtoano nyumbani kwenye Uwanja wa Mexico City kutawapa Mexico mazingira yenye kelele na hamasa kubwa, kutoka kwa mashabiki wao. Hivyo ni wazi England watakuwa chini ya presha kubwa, lakini ni wazi wana nafasi kubwa pia hasa baada ya kupindua matokeo mbele ya DR Congo.

Wachezaji wa kufuatilia
Harry Kane
Jude Bellingham
Bukayo Saka
Santiago Giménez
Edson Álvarez
Mechi zilizobaki kutoa taswira ya 16 bora


Argentina vs Cape Verde

Spain vs Austria
Australia vs Egypt
Switzerland vs Algeria
Colombia vs Ghana
Mechi hizi zitatoa washindi 6 ambao wataungana na timu 10 zilizofuzu, ili kukamilisha idadi ya timu 16.
Hitimisho
Ratiba kamili ya robo fainali ya FIFA Kombe la Dunia 2026 inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabuiki wote. Kwa mashabiki wengi ratiba hii inaonekana kuwa ingekuwa ya kuvutia sana kama mastaa wakubwa kama Kylian Mbappé, Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Neymar watafuzu. Tusubiri na kuona vita itakayojiri.

