AishaAishaAisha

Kilimanjaro Wonders Queens 0-3 Simba Queens
Aisha Munanka

Kilimanjaro Wonders Queens 0-3 Simba Queens:Ligi Kuu ya Wanawake 2026/27

  • FT:Kilimanjaro Wonders Queens 0-3 Simba Queens, 28 Oktoba 2026, Uwanja wa Ushirika, Moshi.
  • Aisha Munanka mchezaji wa kwanza kufungua akaunti ya mabao ndani ya ligi kikosi cha Simba Queens.
  • Mussa Mgosi,Kocha Mkuu wa Simba Queens awapongeza wachezaji kwa kupambana uwanjani.

Mchezo mkali wa Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) wa ufunguzi matokeo ni Kilimanjaro Wonders Queens 0-3 Simba Queens. Pambano hilililipigwa  Oktoba 28,2026.Mabingwa watetezi, Simba Queens wamefungua pazia kwa ushindi mchezo wa kwanza, Uwanja wa Ushirika,Moshi.Aisha Munaka alifungua akaunti ya mabao kwenye mchezo huo akkifuatiwa na Senaf huku bao la tatu la pointi tatu wapinzani walijifunga.

SOMA HII PIA:Simba Queens: Kikosi, Ratiba, Matokeo na Historia

Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha kindege kwa shilingi 1

Una nafasi yakushinda mpaka milioni 800 ukipaisha kindege sasa hivi na SportPesa. Marubani wapo hewani wanavuna mkwanja kwa kuanzia shilingi 1 tu na kuna zawadi kibao zinakusubiri. Zamu yako ni sasa bofya hapa chini uanze safari:-

image
 

Kilimanjaro Wonders Queens 0-3 Simba Queens taarifa

Kipengele Maelezo
Mashindano TWPL
Matokeo Kilimanjaro Wonders Queens 0-3 Simba Queens
Uwanja Ushirika, Moshi
Tarehe 28/10/2026
Timu mwenyeji Kilimanjaro Wonders Queens

Maoni ya Musa Mgosi

Mara baada ya ubao kusoma Kilimanjaro Wonders Queens 0-3 Simba Queens Kocha Mkuu wa Simba Queens, Mussa Mgosi amesema ni furaha kuvuna pointi tatu ugenini.Aliongeza kuwa pongezi zinarudi kwa wachezaji kutimiza majukumu.Alibainisha mpango mkubwa ni kufanikisha malengo ya kutetea ubingwa.

“Furaha kubwa ni kuona tumeanza kwa kupata pointi 3 muhimu.Kila mchezo tunauchukulia kwa umuhimu kutokana na ushindani uliopo.Huu ni mwanzo wa msimu hivyo tutaendelea kupambana kwa mechi zinazofuata,”.

Nahodha Fatuma Issa ataja kilichowapa ushindi

Fatuma Issa maarufu kwa jina la Fety Densa, nahodha wa Simba SC amebainisha kuwa kilichowapa ushindi ni kufuata maelekezo.Fety amesema ni furaha kwa kila mchezaji kuona wanapata ushindi ugenini.Ameongeza kwa kuwashukuru mashabiki na benchi la ufundi.

“Kikubwa ilikuwa ni kuona tunaanza vizuri.Tumefurahi kwa kupata pointi tatu ugenini.Hii ilitokana na kufuata vema maelekzo ya benchi la ufundi hivyo tunawashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi kutushangilia,”.

Hitimisho

Ni Kilimanjaro Wonders Queens 0-3 Simba Queens mchezo mkali wa ufunguzi msimu wa 2026/27.Mabingwa watetezi wamerejea Dar kwa maandalizi ya mechi zinazofuata.Pambano linalofuata kwa Simba Queens itakuwa dhidi ya Fountain Gate Princess ugenini Novemba 4,2026.

Share this: