S-Aziz KiS-Aziz KiS-Aziz Ki
Aziz Ki (-)
Aziz Ki kiungo mshambuliaji wa Yanga SC

Stephane Aziz Ki: Wasifu, safari yake ya soka na kurejea Yanga SC | SportPesa Blog

  • Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC Stephane Aziz Ki ni raia Burkina Faso ambaye alizaliwa Ivory Coast.
  • 2025/26 alikuwa Klabu ya Wydad Casablanca amerejea katika kikosi cha Yanga SC 2026/27.
  • Alikosekana kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Simba SC uliochezwa Uwanja wa Uhuru kutokana na adhabu ya kadi nyekundu aliyopata mchezo dhidi ya Geita Gold FC.

Anaitwa Stephane Aziz Ki, kiungo mshambuliaji wa Yanga SC ameletwa duniani 6 Machi 1996, Ivory Coast ni raia wa Burkina Faso.Huyu ni mchezaji wa kitaalamu wa mpira wa miguu kwenye eneo la ushambuliaji.2026/27 ni nyota wa kwanza kuonyeshwa kadi nyekundu kwa mabingwa watetezi ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Geita Gold, Uwanja wa KMC Complex.

Makala haya yanakuletea wasifu kamili wa Aziz Ki, safari yake ya soka, na jinsi anavyoendelea kuleta mabadiliko makubwa ndani ya Klabu ya Yanga SC, hasa katika harakati za kutwaa mataji mbalimbali.

SOMA HII PIA:Aziz Ki atarejea Yanga SC | Wydad Casablanca kumtema | Tetesi za usajili

Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha kindege kwa shilingi 1

Una nafasi yakushinda mpaka milioni 800 ukipaisha kindege sasa hivi na SportPesa. Marubani wapo hewani wanavuna mkwanja kwa kuanzia shilingi 1 tu na kuna zawadi kibao zinakusubiri. Zamu yako ni sasa bofya hapa chini uanze safari:-

image

Aziz Ki: Wasifu na mwanzo wa safari yake ya soka

Kiungo Stephane Aziz Ki, raia wa Burkina Faso, amejijengea jina kama mmoja wa viungo bora wa kushambulia katika ukanda wa Afrika Mashariki. Kipaji chake kilianza kuonekana mapema, akipitia akademi mbalimbali za soka kabla ya kuanza soka la kulipwa.

Uwezo wake wa kumiliki mpira, kupiga pasi za mwisho, na kufunga mabao umemfanya kuwa mchezaji muhimu popote alipocheza. Hii imemfanya kuwa lulu kwa klabu nyingi zinazotafuta vipaji barani Afrika.Mchezo uliopita dhidi ya Mashujaa FC alitoa pasi kwa ya bao kwa Peter Shalulile, Uwanja wa KMC Complex.

Kurejea Yanga SC na malengo

Kurejea kwa Aziz Ki Yanga SC kumekuwa gumzo kubwa, hasa baada ya taarifa kuibuka kuwa ana malengo ya kutwaa mataji sita na klabu hiyo. Malengo haya yanaonyesha dhamira yake ya kuipa mafanikio Yanga SC katika mashindano ya ndani na kimataifa.2025/26 alikuwa katika kikosi cha Wydad Casablanca, amerejea kwa mara nyingine katika kikosi cha Yanga SC .

Uwezo mkubwa katika kupiga faulo na mashuti ya mbali umekuwa ukimpa nafasi kikosi cha kwanza.Ni MVP wa NBC Premier League msimu wa 2023/24.Alikuwa katika kikosi kilichotinga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho 2022/23 kabla ya kuondoka Jangwani.

SOMA HII PIA:Yanga SC vs Simba SC hawa wachezaji wakuchungwa, Prince Dube, Ellie Mpanzu

Athari yake katika nbc Premier League 2026/27

Katika msimu wa NBC Premier League 2026/27, Aziz Ki ameendelea kuwa mchezaji muhimu kwa Yanga SC. Uwezo wake wa kucheza nafasi tofauti za ushambuliaji umempa kocha chaguzi nyingi za kimbinu.Anatarajiwa kuwa mmoja wa wafungaji bora na watoa pasi za mwisho katika ligi, akichangia katika mafanikio ya Yanga SC. Mashabiki wa Yanga SC wana matumaini makubwa naye katika kuendeleza rekodi nzuri ya klabu hiyo.

Aziz Ki alikosekana mchezo wa Kariakoo Dabi

Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza Oktoba 10,2026 Ki alikosekana kwenye mchezo dhidi ya Simba SC.Sababu kubwa ilikuwa ni adhabu ya kadi nyekundu aliyopata dhidi ya Geita Gold.Adhabu hiyo imeisha na tayari amerejea uwanjani.

Kiungo huyo kwenye mechi za Kariakoo Dabi ana rekodi yakufanya vizuri.Oktoba 2022 Aziz Ki aliifunga Simba SC kwa pigo la free kick wakitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1, Uwanja wa Mkapa.Amekuwa anazungumzwa kuwa na uwezo mkubwa akikutana na mnyama kwenye mechi za ushindani.

Hitimisho

Kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki mguu wake wenye nguvu zaidi akiwa uwanjani ni ule wa kulia.Ana umri wa miaka 30 amemuoa mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobetto.Jezi anayovaa uwanjani ni namba 10 iliyokuwa inavaliwa na Pacome Zouzoua ambaye hayupo fiti anasumbuliwa na maumivu ya mguu.

Share this: