Vilabu vya Tanzania CAFFeisal SalumFeisal Salum
Vilabu vya Tanzania CAF
Singida Black Stars

Vilabu vya Tanzania CAF: Simba SC, Yanga SC, Azam FC na Singida Black Stars

  • Simba SC na Yanga SC miongoni mwa vilabu vya Tanzania CAF kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
  • Azam FC na Singida Black Stars zinapeperusha bendera kwenye Kombe la Shirikisho Afrika zimetinga hatua ya makundi.
  •  Yanga SC watavaana na timu za; Club Africain ya Tunisia, MC Alger ya Algeria na Zamalek ya Misri timu za Kundi B.
  • Mnyama amepangwa kundi C katika kusaka tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali.

Vilabu vya Tanzania CAF vimeendelea kuonyesha ushindani mkubwa katika mashindano ya kimataifa ya CAF, vikileta matumaini kwa mashabiki wa soka nchini. Simba SC na Yanga SC zimekuwa zikifanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Azam FC na Singida Black Stars zikijitahidi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Ushiriki huu ni muhimu kwa maendeleo ya soka la Tanzania, kwani unatoa fursa kwa wachezaji kupata uzoefu wa kimataifa na kuongeza hadhi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League). Hapa tumekuletea uchambuzi wa kina kuhusu nafasi na matarajio ya vilabu hivi katika nashindano ya CAF.

SOMA HII PIA:Simba SC CAF Champions League: Fixtures, Results, Squad & Standings

Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha kindege kwa shilingi 1

Una nafasi yakushinda mpaka milioni 800 ukipaisha kindege sasa hivi na SportPesa. Marubani wapo hewani wanavuna mkwanja kwa kuanzia shilingi 1 tu na kuna zawadi kibao zinakusubiri. Zamu yako ni sasa bofya hapa chini uanze safari:-

image

Simba SC: Wawakilishi hodari wa Tanzania

Simba Sports Club, maarufu kama ‘Wekundu wa Msimbazi’, imekuwa ikifanya vizuri mara kwa mara katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Klabu hii imefanikiwa kufika hatua za juu za mashindano hayo mara kadhaa, ikionyesha uwezo mkubwa wa ushindani.

2026/27 Simba SC imetinga hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla ya mabao 9-1 15 de Agosto FC.Katika mchezo wa kwanza Oktoba 21,2026 walishinda mabao 6-1 na mshambuliaji IbrahimDoumbia alifunga mabao mawili.Mchezo wa marudio mnyama alishinda mabao 3-0, mechi zote zilichezwa Uwanja wa Uhuru.Inakuwa ni mara ya 7 Simba SC kutinga hatua ya makundi CAF.

SOMA HII PIA:Simba SC imepangwa Kundi C CAF: RS Berkane, Orlando Pirates na Colombe Sportive

Yanga SC: Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu NBC

Young Africans Sports Club, ‘Wananchi’, wamekuwa na msimu mzuri katika Ligi Kuu Tanzania Bara na wamekuwa wakifanya vizuri pia katika mashindano ya CAF. Walifanikiwa kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2022/23.Kwa sasa, Yanga SC inwakilisha Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Matarajio ni makubwa kwao kutokana na kikosi chao imara na ari ya ushindi waliyonayo.

Ilitinga hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla ya mabao 8-1 dhidi ya CFFA FC.Oktoba 17,2026 CFFA FC 0-4 Yanga SC na Oktoba 21,2026, Yanga SC 4-1 CFFA FC.Mechi zote zilichezwa Uwanja wa Azam Complex.

SOMA HII PIA:Yanga SC imepangwa Kundi B droo ya Makundi CAF Champions League | Kuvaana na waarabu Zamalek, MC Alger, Club Africain Ratiba, matokeo, Live score, taarifa za hatua ya makundi

Azam FC: Wawakilishi katika Kombe la Shirikisho Afrika

Azam Football Club, ‘Wana Lambalamba’, wamekuwa wakionyesha uimara wao katika Kombe la Shirikisho Afrika. Klabu hii ina miundombinu bora na uwekezaji mkubwa katika soka, jambo linalowapa faida katika mashindano ya kimataifa.Azam imethibitisha ushiriki wake katika hatua za makundi za Kombe la Shirikisho Afrika 2026/27.

Matajiri hawa walitinga hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla ya mabao 2-1 ZED FC.Oktoba 16,2026 ZED FC 1-1 Azam FC na Oktoba 24,2026 Azam FC 1-0 ZED FC.

Singida Black Stars waliwafungashia virago Tusker FC

Singida Black Stars imekuwa na mwendelezo mzuri katika anga la kimataifa. Ushiriki wao katika mashindano ya CAF ni hatua kubwa kwao na kwa mkoa wa Singida. Waliwafungashia virago wapinzani wao Tusker FC kwenye hatua ya mtoano.

Tusker FC 0-1 Singida Black Stars, Oktoba 18,2026.Oktoba 25,2026 Singida Black Stars 1-1 Tusker FC.Ugenini wawakilishi kutoka Tanzania walipata ushindi kimataifa wakitinga hatua ya makundi kwa jumla ya mabao 2-1.

Hitimisho

Ushiriki wa vilabu hivi vinne katika mashindano ya CAF unatoa matumaini makubwa kwa soka la Tanzania. Kila klabu ina malengo yake, lakini lengo kuu ni kuwakilisha nchi kwa heshima na kufanya vizuri kadri iwezekanavyo.Mashabiki wanatarajiwa kutoa sapoti kubwa kwa timu zao, iwe nyumbani au ugenini. Mafanikio ya vilabu hivi yataongeza hadhi ya soka la Tanzania na kuvutia wawekezaji zaidi katika mchezo huu.

 

 

Share this: