- Colombia vs Ghana Kombe la Dunia 2026, ratiba ya mechi nyingine kali ya hatua ya 32 bora Kombe la Dunia 2026 itakayopigwa 4 July.
- Mechi hii itapigwa kwenye Uwanja wa Kansas City, uliopo USA kuanzia majira ya saa 10 na nusu Alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki.
- Mastaa James Rodriguez na Luis Diaz wataiongoza Colombia, kuvaana na Ghana wakiongozwa na Anthony Semenyo.
- Makala hii inachambua h2h, livescore, takwimu na Habari za timu za mechi hii kama ifuatavyo
Colombia vs Ghana ni karata nyingine ya wawakilishi wa Afrika na Amerika Kusini, katika jukwaa kubwa zaidi la soka Duniani. Mchezo huu unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Kansas City nchini USA, saa kumi na nusu kwa saa za Afrika Mashariki. Mshindi wa jumla wa mchezo huu atakuwa amefuzu moja kwa moja hatua ya 16, bora ya mashindano haya. Makala hii inachambua baadhi ya takwimu muhimu za mchezo huu, ikiwemo h2h, taarifa za timu, Lineups.
Hizi hapa Odds bora za SportPesa za mechi ya Colombia vs Ghana
Kwa wanaotafuta odds bora, SportPesa inatoa masoko mbalimbali ya ubashiri pamoja na malipo ya haraka. kwa sasa odds zimeboreshwa na unaweza kubashiri mechi hii sasa gusa hapo chini, ili kubashiri moja kwa moja.

Maelezo ya Mechi

| Kipengele | Maelezo |
|---|---|
| Mashindano | Mchezo huu ni wa hatua ya 32 Bora ya Kombe la Dunia la FIFA 2026, ambapo mshindi husonga mbele na mshindwa huaga mashindano. |
| Tarehe na Muda | Mechi imepangwa kuchezwa usiku wa kuamkia Jumamosi, kuanzia saa 10:30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki (EAT). |
| Uwanja | Timu hizo zitamenyana katika Uwanja wa Kansas City uliopo Kansas City, Marekani (USA), moja ya viwanja vinavyotumika kuandaa Kombe la Dunia la FIFA 2026. |
KUJUA RATIBA YA MECHI ZOTE 104, SOMA HII: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Muhtasari wa Colombia vs Ghana Kombe la Dunia 2026
Ghana ilifika katika Kombe la Dunia la FIFA ikiwa na changamoto nyingi, ikiwemo uteuzi wa kushangaza wa Carlos Queiroz na masuala ya kisheria yanayomkabili Thomas Partey. Lakini Black Stars wameonyesha ukomavu na kufanikiwa kufuzu hatua ya 32 bora ya mashindano haya. Katika hatua hii Ghana wanatarajia kuvaana na Colombia usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi kwa saa za Afrika Mashariki.
Ghana ilimaliza nafasi ya tatu Kundi L na sasa inakutana na Colombia, ambayo iliongoza Kundi K mbele ya Ureno. Ikumbukwe kocha wa Ghana, Queiroz aliwahi kuinoa Colombia kati ya mwaka 2019 na 2020. Matokeo mabaya dhidi ya Uruguay na Ecuador yalimaliza kibarua chake.
Habari za Timu na majeruhi
Antoine Semenyo alipata majeraha madogo dhidi ya Croatia, lakini anatarajiwa kurejea Uwanjani dhidi ya Colombia. Kocha, Carlos Queiroz ameonekana bado anajaribu kupata kikosi chake bora cha Ghana. Mjadala mkubwa ni nafasi ya kipa kati ya Lawrence Ati-Zigi na Benjamin Asare.
Vikosi vinavyotarajiwa Colombia vs Ghana
Colombia:
| Kipengele | Maelezo |
|---|---|
| Kipa | Camilo Vargas anatarajiwa kuanza langoni kama kipa wa kwanza wa kikosi. |
| Walinzi | Safu ya ulinzi inaundwa na Deiver Machado, Jhon Lucumí, Davinson Sánchez na Santiago Arias. |
| Viungo | Gustavo Puerta, Jefferson Lerma na Jhon Arias wanatarajiwa kuongoza eneo la kiungo. |
| Washambuliaji | Luis Díaz, Jhon Córdoba na James Rodríguez wanatarajiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji. |
Ghana:

| Kipengele | Maelezo |
|---|---|
| Kipa | Benjamin Asare anatarajiwa kulinda lango la Ghana katika mchezo huu. |
| Walinzi | Gideon Mensah, Derrick Luckassen, Jonas Adjetey na Marvin Senaya wanatarajiwa kuunda safu ya ulinzi. |
| Viungo | Caleb Yirenkyi, Thomas Partey na Issahaku Fatawu wanatarajiwa kucheza eneo la kiungo na kusimamia mchezo wa timu. |
| Washambuliaji | Ernest Nuamah, Jordan Ayew na Antoine Semenyo wanatarajiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Ghana. |
KUHUSU UCHAMBUZI WA MECHI IJAYO YA MISRI, SOMA HII: Prediction Australia vs Misri FIFA Kombe la Dunia 2026: Hatua ya 32 bora, Team news, odds, lineups
Utabiri (Colombia kushinda au sare)
Uchambuzi wa kitaalamu unatoa nafasi kubwa ya matokeo ya Colombia kushinda au sare, wababe hao wa Amerika Kusini walikuwa vinara wa Kundi K la mashindano haya mbele ya Ureno. Wamekuwa na uwiano mzuri wa kiuchezaji na matokeo waliyopata yanawapa ari zaidi. Ghana licha ya mabadiliko ya benchi la ufundi ya dharula, kabla ya kuanza kwa mashindano wameonyesha kuwa sio timu ya kubeza. Kupitia uchambuzi wa kiuhariri mchezo huu unaweza ukaisha kwa Colombia kushinda au sare, ikumbukwe haya si matokeo rasmi bali maoni ya kiuhariri, hivyo beti kistaarabu.
Colombia vs Ghana h2h

Timu hizi hazijawahi kukutana katika mashindano yoyote hapo kabla, hivyo hii itakuwa mara ya kwanza kwao. Hii inatarajiwa kuufanya mchezo huu kuwa moja ya rekodi mpya katika rekodi za soka la kimataifa. Swali ni je, Ghana wataweza kuizuia Coombia? Tusubiri dakika 90 zitatoa majibu kamili.
Hitimisho

Uchambuzi wa kitaalamu wa mchezo huu unaipa nafasi kubwa Colombia kuibuka na ushindi, hii ni kwa kuzingatia uzito na ubora wa kikosi chao. Licha ya matarajio hayo, pia inatarajiwa mchezo utakuwa mgumu na huenda tukashuhudia ‘sapraiz’ ya matokeo kutoka kwa Ghana. Huu ni mchezo wa mwisho wa hatua ya 32 bora, fuatlia SportPesa blog kwa taarifa zaidi.
KUJUA KUHUSU UCHAMBUZI WA MECHI IJAYO YA PORTUGAL, SOMA HII: Prediction | Portugal vs Croatia Kombe la Dunia 2026: Hatua ya 32 bora, Live score, h2h, odds na habari za timu

