Portugal vs CroatiaPortugal vs Croatia
  • Portugal vs Croatia Kombe la Dunia 2026, ni ratiba ya vita ya timu zenye uzito mkubwa, ambayo imebeba hatima ya kujua nani atafuzu hatua ya 16 bora ya mashindano hayo.
  • Mechi hii usiku wa kuamkia Ijumaa 3 July 2026 katika Uwanja wa Toronto, Canada kuanzia majira ya saa nane usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
  • Portugal inayoongozwa na mastaa wao Cristiano Ronaldo na Bruno Fernandez watakuwa na kazi ngumu ya kuvaana na Croatia inayoongozwa na kiungo mkongwe, Luka Modrick.
  • Makala hii inachambua h2h, livescore, takwimu na Habari za timu za mechi hii kama ifuatavyo

Portugal chini ya nahodha wao, Cristiano Ronaldo watakuwa na mtihani mgumu wa kuvaana na Croatia katika mchezo muhimu wa Kombe la Dunia 2026 hatua ya 32. Mchezo huu utapigwa usiku wa kuamkia Ijumaa 3 July 2026, katika Uwanja wa Toronto, Canada. Mshindi wa mchezo huu atakuwa amefuzu moja kwa moja hatua ya 16 bora ya mashindano, makala hii inachambua baadhi ya takwimu muhimu za mchezo huu, ikiwemo h2h, taarifa za timu, Lineups.

Hizi hapa Odds bora za SportPesa za mechi ya Portugal vs Croatia

Kwa wanaotafuta odds bora, SportPesa inatoa masoko mbalimbali ya ubashiri pamoja na malipo ya haraka. kwa sasa odds zimeboreshwa na unaweza kubashiri mechi hii sasa gusa hapo chini, ili kubashiri moja kwa moja.

Portugal vs Croatia
Portugal vs Croatia

Maelezo ya Mechi

Ratiba ya Portugal FIFA Kombe la Dunia 2026
kikosi cha Portugal
KipengeleMaelezo
MashindanoMechi ya hatua ya 32 Bora ya Kombe la Dunia la FIFA 2026.
Tarehe na MudaMchezo utapigwa Ijumaa, ukianza saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki (EAT).
UwanjaBMO Field, jijini Toronto, Canada.

KUJUA RATIBA YA MECHI ZOTE 104, SOMA HII: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika

Muhtasari wa Portugal vs Croatia

Uu ni miongoni mwa michezo migumu itakayoshuhudiwa katika hatua ya 32 bora Kombe la Dunia 2026, utakaochezwa alfajiri ya Ijumaa mjini Toronto. Ureno walimaliza hatua ya makundi bila kupoteza mchezo wowote, lakini walijikuta wakishika nafasi ya pili katika Kundi K nyuma ya Colombia. Ushindi wao mkubwa wa mabao 5-0 dhidi ya Uzbekistan ndio umebaki kuwa matokeo yao ya kuvutia zaidi, kwenye mashindano haya.

Croatia wao walimaliza nafasi ya pili katika Kundi L baada ya kuanza kwa kupoteza dhidi ya England, kabla ya kupata ushindi mfululizo dhidi ya Ghana na Panama. Aidha, wamefanikiwa kufunga bao katika kila mchezo waliocheza kwenye mashindano haya. Ingawa Ureno wametajwa kuwa miongoni mwa timu zinazopewa nafasi ya kutwaa Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza, kiwango walichoonyesha hadi sasa hakijawashawishi wengi.

Habari za Timu na majeruhi

Joao Cancelo alipata maumivu madogo katika mchezo dhidi ya Colombia, endapo hatakuwa tayari kuanza, nafasi yake inatarajiwa kuchukuliwa na Diogo Dalot. Hilo ndilo linaonekana kuwa huenda likawa badiliko pekee, ambalo Roberto Martinez anaweza kulifanya. Croatia wao hawajahusishwa na taarifa yoyote ya majeruhi.

Vikosi Vinavyotarajiwa

Ureno

NafasiMchezaji
KipaDiogo Costa
WalinziJoao Cancelo, Ruben Dias, Renato Veiga, Nuno Mendes
ViungoVitinha, Joao Neves, Pedro Neto, Bruno Fernandes
WashambuliajiJoao Felix, Cristiano Ronaldo

Croatia

Croatia vs Ghana FIFA Kombe la Dunia 2026
Croatia vs Ghana
NafasiMchezaji
KipaDominik Livakovic
WalinziJosip Stanisic, Josip Sutalo, Marin Pongracic, Josko Gvardiol
ViungoPetar Sucic, Luka Modric, Mateo Kovacic, Martin Baturina
WashambuliajiAnte Budimir, Ivan Perisic

Portugal vs Croatia h2h

Timu hizi zimekutana mara 10 katika historia ya mikutano yao, ambapo Portugal wameshinda mechi 7. Croatia wameshinda mechi 1 pekee, huku mechi 2 zikiisha kwa matokeo ya sare. Hivyo hii ni nafasi ya kuandika rekodi mpya kwa kila timu.

Rekodi ya mechi 5 zilizopita Kati ya Portugal vs Croatia

TareheMechiMatokeo
18 Novemba 2024Croatia vs UrenoCroatia 1-1 Ureno
5 Septemba 2024Ureno vs CroatiaUreno 2-1 Croatia
8 Juni 2024Ureno vs CroatiaUreno 1-2 Croatia
17 Novemba 2020Croatia vs UrenoCroatia 2-3 Ureno
5 Septemba 2020Ureno vs CroatiaUreno 4-1 Croatia

Utabiri (Ureno kushinda au sare yaani Double chance 1X)

Portugal vs Croatia Kombe la Dunia 2026
Cristiano

Timu zote mbili zina ubora mkubwa katika safu ya ushambuliaji na zina uwezo wa kutengeneza nafasi za kufunga. Hata hivyo, Ureno wanaonekana kuwa na faida ndogo ya ziada kutokana na ubora wa majina waliyonayo katika kikosi chao, hivyo ubashiri wetu ni 1X. Timu zote mbili pia zina safu imara za ulinzi na haziruhusu mabao mengi, hivyo mchezo huu unatarajiwa kuwa wa ushindani na tahadhari. Ikumbukwe huu ni ubashiri wa kitaalamu na sio matokeo halisi, hivyo Bashiri kistaarabu.

Hitimisho

Kwa kuangalia ubora wa vikosi hivi viwili, haionekani kuwa kama kuna tofauti kati yao. Hata hivyo, rekodi bora ya Ureno dhidi ya Croatia katika miaka ya karibuni inawapa faida zaidi, kuelekea mchezo huu lakini Croatia wameonyesha mara nyingi uwezo wa kuwatesa vigogo wa dunia kwenye mashindano makubwa. Hivyo huu ni miongoni mwa michezo mikubwa ya hatua ya 32 bora. Fuatlia SportPesa blog kwa taarifa zaidi.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.