- Egypt vs Iran Kombe la Dunia 2026, ni ratiba itakayotoa hatima ya safari ya hatua ya mtoano ya 32 bora ndani ya kundi G.
- Mechi hii kali itapigwa kwenye Uwanja wa Seatle, 27 June 2026 saa 12 alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki.
- Hili ni miongoni mwa makundi magumu, ambayo kila mtu ana nafasi ya kufuzu hatua ya mtoano.
- Jeshi la Egypt litaongozwa na nahodha, Mohammed Salah na Omar Marmoush. Makala hii inachambua h2h, livescore, takwimu za mechi hii kama ifuatavyo
Egypt wakiwa kileleni mwa msimamo wa Kundi G watajipanga kuhakikisha wanapata ushindi, ili kujihakikisha nafasi ya kufuzu na kuongoza Kundi hilo watakapokutana na Iran. Mechi hii muhimu inatarajiwa kupigwa kwenye dimba la Seatle, Washington USA saa 12 alfajiri kwa saa za Afrika Mashiriki 27 June 2026. Ikumbukwe Iran wanakamatia nafasi ya pili, wakiwa na pointi zao 2 sawa na Ubelgiji, huku New Zealand wanaoburuza mkia na pointi yao 1.
Hizi hapa Odds bora za SportPesa za mechi ya Egypt vs Iran
Kwa wanaotafuta odds bora, SportPesa inatoa masoko mbalimbali ya ubashiri pamoja na malipo ya haraka. kwa sasa odds zimeborwesha na unaweza kubashiri mechi hii sasa gusa hapo chini, ili kubashiri moja kwa moja.

Maelezo ya Mechi

| Kipengele | Maelezo |
|---|---|
| Mashindano | Pambano la mwisho la hatua ya makundi katika Kundi G la Kombe la Dunia la FIFA 2026. |
| Tarehe na Muda | Mchezo utafanyika Jumamosi, tarehe 27 Juni 2026, ukianza saa 12:00 alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki (EAT). |
| Uwanja | Seattle Stadium, uliopo Seattle, jimbo la Washington nchini Marekani, utakuwa mwenyeji wa mchezo huu. |
| Msimamo wa Kundi G | Misri wanaongoza kundi kwa pointi 4, Iran na Ubelgiji wana pointi 2 kila mmoja, huku New Zealand wakishika nafasi ya mwisho kwa pointi 1. |
| Umuhimu wa Mchezo | Matokeo ya mchezo huu ni muhimu kwa timu zote mbili. Ushindi utaongeza nafasi ya kufuzu hatua ya mtoano, ama kwa kumaliza juu ya kundi au kupitia nafasi za timu bora zilizomaliza katika nafasi ya tatu. |
| Mchezo Mwingine wa Kundi | Wakati huohuo, Ubelgiji watamenyana na New Zealand katika mechi nyingine ya Kundi G, matokeo ambayo yanaweza kuwa na athari kubwa kwenye msimamo wa mwisho wa kundi. |
KUJUA RATIBA YA MECHI ZOTE 104, SOMA HII: Ratiba FIFA Kombe la Dunia 2026 | Mechi zote 104 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Muhtasari wa Egypt vs Iran
Kundi G linafikia tamati siku ya Jumamosi wakati Misri na Iran zitakapokutana katika Uwanja wa Lumen Field, Seattle, kwenye mechi muhimu ya Kombe la Dunia 2026. Timu zote mbili bado zina nafasi kubwa ya kufuzu hatua ya mtoano.
Misri wanaongoza kundi kwa pointi nne kuelekea mchezo wa mwisho wa makundi, huku Iran wakibaki bila kupoteza na wakijua kuwa matokeo mazuri yanaweza kuwapeleka hatua inayofuata ya mashindano.
Misri ilianza kampeni yake ya Kombe la Dunia kwa sare ya 1-1 dhidi ya Ubelgiji, matokeo yaliyowapa pointi muhimu katika moja ya mechi ngumu zaidi za Kundi G. Baadaye, Mafarao waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya New Zealand katika mchezo wa pili wa Kundi na kufika kileleni.
Misri haijawahi kuvuka hatua ya makundi ya Kombe la Dunia tangu mwaka 1990, lakini sasa hatima yao ikiwa mikononi mwao wenyewe. Mohamed Salah amekuwa nyota wa Misri katika mashindano haya, akichangia bao moja na pasi mbili za mabao katika mechi mbili za kwanza. Anatarajiwa kuwa mhimili muhimu tena katika pambano hili. Misri wanajua kuwa sare dhidi ya Iran itawatosha kufuzu hatua ya 32 bora, huku ushindi ukiwapa nafasi ya kumaliza kileleni mwa Kundi G.
Kwa upande mwingine, Iran, wanaoshika nafasi ya 20 katika viwango vya FIFA duniani, walianza kwa sare ya 2-2 dhidi ya New Zealand. Baadaye walipata sare tasa dhidi ya Ubelgiji katika moja ya maonyesho bora ya kujilinda yaliyoshuhudiwa kwenye mashindano haya. Matokeo hayo yameifanya Iran kufikisha michezo mitano mfululizo bila kupoteza katika mashindano yote.
Habari za Timu na Vikosi Vinavyotarajiwa
Kwa upande wa Egypt hofu kubwa iko juu ya kiungo wao wa ulinzi, Hamdy Fathy bado ambaye aliumia misuli ya nyuma ya paja katika mechi dhidi ya New Zealand. Ramy Rabia, ambaye aliingia kuchukua nafasi yake, anatarajiwa kuendelea kuanza pamoja na Yasser Ibrahim katikati ya ulinzi iwapo Fathy hatakuwa tayari. Misri pia huenda wakamkosa Hossam Abdelmaguid ambaye alipata majeraha katika mechi iliyopita.
Kwa Iran, hakuna majeruhi wakubwa isipokuwa Roozbeh Cheshmi ambaye amekosa michezo miwili ya kwanza na anaweza kukosa pia mchezo huu. Kocha Amir Ghalenoei anaweza kufanya mabadiliko machache, baada ya sare dhidi ya Ubelgiji. Alireza Jahanbakhsh ana nafasi kubwa ya kurejea kwenye kikosi cha kwanza baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba katika mchezo uliopita. Iwapo Jahanbakhsh ataanza, Ramin Rezaeian anaweza kusogezwa nyuma zaidi kama beki wa pembeni anayesaidia mashambulizi.
Vikosi Vinavyotarajiwa
Egypt
| Nafasi | Mchezaji |
|---|---|
| Kipa (GK) | Mostafa Shobeir |
| Beki wa Kulia (RB) | Mohamed Hany |
| Beki wa Kati (CB) | Yasser Ibrahim |
| Beki wa Kati (CB) | Ramy Rabia |
| Beki wa Kushoto (LB) | Ahmed Fatouh |
| Kiungo wa Ulinzi (DM) | Marwan Attia |
| Kiungo wa Kati (CM) | Mohamed Lasheen |
| Winga wa Kulia (RW) | Mohamed Salah |
| Kiungo Mshambuliaji (AM) | Emam Ashour |
| Winga wa Kushoto (LW) | Ziko |
| Mshambuliaji (ST) | Omar Marmoush |
Iran

| Nafasi | Mchezaji |
|---|---|
| Kipa (GK) | Alireza Beiranvand |
| Beki wa Kulia (RB) | Ramin Rezaeian |
| Beki wa Kati (CB) | Shoja Khalilzadeh |
| Beki wa Kati (CB) | Amir Nemati |
| Beki wa Kushoto (LB) | Ehsan Hajsafi |
| Beki wa Kati (CB) | Hossein Kanaani |
| Kiungo wa Kulia (RM) | Mohammad Mohebi |
| Kiungo wa Kati (CM) | Saeid Ezatolahi |
| Kiungo Mshambuliaji (AM) | Saman Ghoddos |
| Winga wa Kushoto (LW) | Alireza Jahanbakhsh |
| Mshambuliaji (ST) | Mehdi Taremi |
KUJUA RATIBA NA UCHAMBUZI WA MECHI IJAYO YA CAPE VERDE, SOMA HII: Prediction: Cape Verde vs Saudi Arabia Kombe la Dunia 2026: Live score, h2h, odds na habari za timu
Rekodi ya Mikutano (H2H)
Timu hizi zina kumbukumbu ya kukutana mara 2 ambapo kila timu imeshinda mechi moja, Egypt wao wakishinda mechi yao kwa penalty. Mechi hii inatarajiwa kuwa mechi ya kwanza ya kimataifa ya kirafiki, kwani makutano yao yaliyopita alikuwa ya kirafiki. Hivyo huu unatarajiwa kuwa mchezo wa kihistoria kwenye jukwaa kubwa zaidi la soka.
Utabiri Wetu (magoli 2 na zaidi yaani over 1.5)

Kila timu inaingia katika mchezo huu ikiwa na malengo ya kuvuna pointi tatu muhimu, ili kufuzu hatua ya mtoano. Timu zote zimeonyesha nidhamu ya kiuchezaji, na uwezo mkubwa wa kupambana dhidi ya wapinzani wa kiwango cha juu kama Belgium. Ubora wa wachezaji kama Salah na Marmoush unatarajiwa kupelekea magoli, hivyo mchezo huu unatarajiwa kuwa na mabao mengi angalau zaidi ya mawili. Kumbuka haya ni maoni ya kiuhariri, na sio matokeo halisi, hivyo chambua na Bashiri kistaarabu.
Hitimisho

Utabiri wetu wa kiuhariri unayapa nafasi kubwa matokeo ya kupatikana kwa mabao mawili au zaidi. Mechi hii itaamua nani anakwenda hatua inayofuata, ambapo timu zote zinahitaji ushindi ili kusonga mbele. Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa ratiba, matokeo, utabiri na habari za Kombe la Dunia 2026. Angalia odds za Egypt vs Iran kwenye SportPesa na ubashiri kistaarabu.
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQ)
Egypt vs Iran itaanza saa ngapi?
Mechi itaanza saa 12 alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki (EAT) Jumamosi tarehe 27 Juni 2026.
Egypt vs Iran kundi gani?
Wapo Kundi G pamoja na Belgium na New Zeeland.
KUJUA UCHAMBUZI NA RATIBA YA MECHI IJAYO YA SPAIN, SOMA HII: Prediction Senegal vs Iraq FIFA Kombe la Dunia 2026: Kundi I, h2h, team news, odds

